Kuna wanawake Wana roho mbaya, aibu hawana na kujificha hawawezi

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,485
99,214
Wakuu,

Mimi Ni baba wa watoto 5 na mtoto wangu wa mwisho wa miaka 2 kasoro anaumwa na Yuko Kwny dozi ya sindano, anatakiwa kupelekwa dispensary kuchomwa kila saa 12 jioni.

Sasa Leo nilishinda nyumban Siku nzima, ilipofika saa 1 kasoro usiku nikawauliza vp mbona mtoto leo hajapelekwa kuchomwa sindano? KILA mtu nyumbani akawa anamtupia mpira mwenzie. Nikaona isiwe kesi, ntampeleka mwenyewe.

Nmejiandaa,nmempakia na nmeenda nae dispensary na keshachomwa sindano, nikaona Ni mapema Sana kurud nyumbani, ukzingatia nilishinda home Siku nzima (sio kawaida yangu).ikabd niende kwa Mchepuko wangu kupoteza poteza muda Kisha baadae ndo ntarud nyumban.

Nmefika kwake kanipokea kwa furaha sn na bashasha zote na kunambia leo nmeamua kumsapraizi maana tangu azaliwe uyu mwanangu hajawai kumuona laivu Zaid ya kuona picha zake tu kwenye simu yangu. Basi tukacheka na kufurahi wote.

Akaniuliza aniandalie nn mpenz wake, Nikamwambia chochote kile Cha Moto Moto, akasema Basi ngoja aniandalie supu ya ng'ombe, Kuna nyama mbichi Kwny friji ilibaki, Nikamwambia itakua vzur Sana.

Sasa akiwa kaenda jikoni kuandaa supu, nami nikawa sebleni naangalia tv, mwanangu akaenda Kwny showcase ya tv kachukua mdoli wa dubu kaanza kuuchezea, kamkuta anachezea mdoli na Kwenda kuchumban kwake kamletea midoli mingine miwili ili achezee Zaid, Kisha karud zake jikon kuendelea kuandaa supu.

Supu imeiva kaniletea mezani na nyingine kdg kampakulia Mtoto ili anywe, anampozea Kwny kijiko na kumuwekea mdomoni, nikamwona mwanangu kama ana mafua mengi Sana puani.

Nikamwambia, " kwanza mfute mafua Ayo mtoto,unampaje supu na unaona kabisa ana makamasi kibao puani?" Akasema "POA". Kainuka na Kwenda nje kibarazani Kisha karudi na dekio mkononi, analigeuza geuza na kulichambua ili kupata sehemu Safi ili amfutie mtoto mafua.

Nikamuuliza,
"Are you serious unataka kumfutia mwanangu mafua na hilo dekio lako la kudekia humu ndani? Huna kitenge au khanga ya kumfutia Mtoto mafua?"

Akanijibu
"vitenge nilivyonavyo vyote ni vya kutokea, khanga nilizonazo zote za kuogea, labda kamnunulie leso tumfute, ulitakiwa utembee na leso mwanao uyu ana mafua makali Sana"

Nikamuuliza,
"Kwaiyo mwanangu ana mafua makali Sana mpk unaona kinyaa kumfutia na iyo khanga yako ulojifunga sio? "

Akasema
"Ayo umesema wewe, ila Hii kanga au zilizokabatini kwnagu siwezi kumfutia mwanao, zote Ni safi, lete buku tukanunue leso ya Mtoto, Kama utaki Basi, atakunywa supu na mafua yake"

Nikamwambia,
"Isiwe kesi, ntamfuta TU na shati langu" kweli nmeenda chumbani nilikovulia shati, nmerud nalo na nmemfuta mafua na mtoto kaendelea kunywa supu na stori nyngn zikaendelea.

Kamaliza kunywa supu, vyombo vimetolewa, mamaJ kaenda jikoni kupeleka vyombo vichafu Kisha kaja na ndoo ya maji yenye sabuni kusafisha mezani na chini alipokua analia Mtoto.

Akiwa anafuta chini ikabd amwinue Mtoto Ili asafishe na pale alikokaa Mtoto, ndo kustuka kumbe Mtoto kanya. Akanambia "mwanao kajinyea, kumbe ukumfunga pampasi?". Nikamjibu "nilimkurupua TU baada kua kila mtu home anajishauri kumpeleka Kwny sindano". Akaitikia Kisha kumrudishia alikokaa na kuendelea kusafisha sehem nyingine.

Alipomaliza akarud Kwny Kochi na kunilalia mapajani akachukua simu yake na kuingia tiktok, nikamwambia muweke sawa Kwanza Mtoto ndo uendelee na hizo tiktok zako.

Kweli kainuka na Kwenda nje na kuchukua Lile dekio na kuja nalo pale, kamvua Mtoto suruali kaiweka pembeni na kumfuta mavi na dekio. Kisha kumrudisha pale pale alipokaa.Nguo yenye mavi na dekio vyote vikapelekwa nje.

Aliporudi kapitiliza Moja kwa Moja jikoni kunawa Kisha karudi kunilalia mapajani Kwny sofa akiendelea na ticktok yake, nikamuuliza "ndo ushamsafisha Mtoto tayar au bado?". Akasema "kwani uoni, kwani unaona bado ana mavi? "

Nikamuuliza,
"Yaan umeshindwa hata kumsuuza mtoto na maji, safi Zaid ya kumfuta na Hilo dekio lako ?"

Akanijibu,
"Jamani,kwani kumleta mwanao kwangu imekua nongwa ivo? nifanye yote Ayo kwani utalala nae apa uyu mwanao? Usafi Zaid Si watamfanyia uko nyumbani ukienda? Au leo unalala Hapa?"

Nikamwambia,
"Haijalishi nalala au silali, Afu huoni ata aibu Mtoto ushamfuta mavi na dekio chafu la sakafu, bado unamwacha akalie tiles za baridi chini na matako matupu kweli"

Akajibu,
"Kha! Una KISIRANI wewe, mbona mshari Sana?, Mi nmeshakwambia Sina khanga chafu za kushindia, zote nilizonazo Ni Safi na za kuogea na nmeshaziweka kabatini. Wee Kama huelewi Basi bhana" akaendelea na tiktok yake.

Kiukweli nilijiskia vibaya sana,
Nikamwambia ainuke nikamsafishe mwanangu mwnyw, kweli nmeinuka nmempeleka chooni nmemsafisha vzur na maji safi, nmemfuta na shati langu kabaki mkavu na nmeaga na nmetoka nje nielekee kwangu.

Anakuja mbio na kuniulizia vp umesahau,ujaacha ela ya kula ya kesho, nmempa elfu 10 anashukuru na kumbusu mwanangu shavuni kinafiki na kumwabia "bye bye" wakati hata kamasi lenyewe kagoma kumfuta puani.

Kiukweli nmetoka pale namuwazia mengi Sana uyu mwanamke ana roho mbaya ya namna gani, hata Kama huenda anamchukia mke wangu, ila sio kwa wanangu niliowazaa Mimi.

Amenifanya niwaze mengi Sana ambayo nilikua siwazii kabisa kua endapo mke wangu imetokea tumetengana au kafariki dunia, ndo nmemuoa mamaj na nmemkabidhi wanangu awalee, Sijui watakua na Hali gani

Nawasilisha
 
Nmefika kwake kanipokea kwa furaha sn na bashasha zote na kunambia leo nmeamua kumsapraizi maana tangu azaliwe uyu mwanangu hajawai kumuona laivu Zaid ya kuona picha zake tu kwenye simu yangu. Basi tukacheka na kufurahi wote.

Akaniuliza aniandalie nn mpenz wake, Nikamwambia chochote kile Cha Moto Moto, akasema Basi ngoja aniandalie supu ya ng'ombe, Kuna nyama mbichi Kwny friji ilibaki, Nikamwambia itakua vzur Sana.

Sasa akiwa kaenda jikoni kuandaa supu, nami nikawa sebleni naangalia tv, mwanangu akaenda Kwny showcase ya tv kachukua mdoli wa dubu kaanza kuuchezea, kamkuta anachezea mdoli na Kwenda kuchumban kwake kamletea midoli mingine miwili ili achezee Zaid, Kisha karud zake jikon kuendelea kuandaa supu.

Supu imeiva kaniletea mezani na nyingine kdg kampakulia Mtoto ili anywe, anampozea Kwny kijiko na kumuwekea mdomoni, nikamwona mwanangu kama ana mafua mengi Sana puani.

Nikamwambia, " kwanza mfute mafua Ayo mtoto,unampaje supu na unaona kabisa ana makamasi kibao puani?" Akasema "POA". Kainuka na Kwenda nje kibarazani Kisha karudi na dekio mkononi, analigeuza geuza kupata sehemu Safi amfutie mafua Mtoto.
dekio?
 
Nikamwambia,
"Haijalishi nalala au silali, Afu huoni ata aibu Mtoto ushamfuta mavi na dekio chafu la sakafu, bado unamwacha akalie tiles za baridi chini na matako matupu kweli"

Akajibu,
"Kha! Una KISIRANI wewe, mbona mshari Sana?, Mi nmeshakwambia Sina khanga chafu za kushindia, zote nilizonazo Ni Safi na za kuogea na nmeshaziweka kabatini. Wee Kama huelewi Basi bhana" akaendelea na tiktok yake.

Kiukweli nilijiskia vibaya sana,
Nikamwambia ainuke nikamsafishe mwanangu mwnyw, kweli nmeinuka nmempeleka chooni nmemsafisha vzur na maji safi, nmemfuta na shati langu kabaki mkavu na nmeaga na nmetoka nje nielekee kwangu.

Anakuja mbio na kuniulizia vp umesahau,ujaacha ela ya kula ya kesho, nmempa elfu 10 anashukuru na kumbusu mwanangu shavuni kinafiki na kumwabia "bye bye" wakati hata kamasi lenyewe kagoma kumfuta puani.

Kiukweli nmetoka pale namuwazia mengi Sana uyu mwanamke ana roho mbaya ya namna gani, hata Kama huenda anamchukia mke wangu, ila sio kwa wanangu niliowazaa Mimi.

Amenifanya niwaze mengi Sana ambayo nilikua siwazii kabisa kua endapo mke wangu imetokea tumetengana au kafariki dunia, ndo nmemuoa mamaj na nmemkabidhi wanangu awalee, Sijui watakua na Hali gani

Nawasilisha
Bro pole Sana, kwa harakaharaka Visa vya mama j vimejaa drama Sana, abapenda pesa kuliko kitu kingine,.

Najaribu kuunganisha dot naona kabisa siku ukifulia utakuta boksa zako nje. Kisa Cha yeye kwenda Dom kikazi gari yao ikaharibika, akafosi umtumie pesa kwa makubaliano kuwa akilipwa pesa zake atarudisha, akalipwa na asirudishe.

Kisa kingine Ni kile Cha wewe kumtoa out, kufikia bar akakutana na marafiki zake, akaanza kuwapa anarula ukizonunua, kuwaokotea na kuwapelekea nyama, mwisho nao akawaagizia, akakuingiza kwenye matumizi yasiyo ya lazima.

Kwa kifupi mama j anataka uanguke kiuchumi ili apate kukuacha. Hakuoendi,. anapenda pesa zako. Zingatia neno hakuoendi. Lakini pia Ni wazi kuwa hawezi kuhudumia au kutoa mchango chanya kwa yeyote miongoni mwa watoto wa mke wako. Take note.
 
Back
Top Bottom