Simulizi ya Operesheni Mauaji(1970) na Habiba Shaban

thatHUMBLEguy

JF-Expert Member
Nov 25, 2023
223
522
Miaka ya 1970, kulitokea wimbi la mauaji ya waganga wa kienyeji mikoa ya Mwanza na Shinyanga. Wengi wa washukiwa waliachiwa huru baada ya kufikishwa mahakamani. Ndipo, Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa hiyo chini ya Uenyekiti wa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, waliagiza wote walioshukiwa na Mauaji hayo wakamatwe na kuhojiwa. Wenye ushahidi wa kutosheleza wapelekwe mahakamani na usiojitosheleza waendelee kushikiliwa. Operation hii iliitwa Oparesheni Mauji na ilisimamiwa na maafisa Usalama kutokea Makao Makuu, Dar Es Salaam.

Opaeresheni hii iliacha makovu makubwa sana. Mkoani Shnyanga, watuhumiwa 524 huku Mwanza 374 walikamatwa. Mahojiano yalihusisha mateso yasiyoelezeka. Mfano, Shinyanga, watu 10 walifariki katika mahojiano hayo, huku 109 wakishikiliwa. Wengine wengi walibaki vilema. Huku Vigogo wawili wa Usalama Mkoa, wakishitakiwa kwa mauji.

Habiba Shabani, muhanga wa Oparesheni hii anasimulia.

Tulikamatwa na kupelekwa kwa gari kwenda Kituo cha Polisi Shinyanga. Tulilala pale kituoni, na Siku iliyofuata tulipelekwa Mahakamani. Sikupata nafasi ya kumuuliza Askari kuhusu kesi yangu sababu walikuwa wakali, wasioruhusu kuhojiwa. Mahakamani kesi ilisomwa, tukituhumiwa sisi watano, tumemuua Mwanamke ambaye jina lake halikutajwa. Iliamuliwa tuendelee kusalia mahabusu tukisubiri siku nyingine ya kutajwa kwa kesi. Tulipelekwa Gereza la Shinyanga. Sikumbuki tulikaa hapo gerezani kwa siku ngapi hadi tulipopelekwa tena mahakamani ambapo kesi ilipelekwa tena mbele kwa madai upelelezi unaendelea.

Mwezi mzima, tulikaa Gereza la Shinyanga. Kisha tukaondolewa hapo kupelekwa Mwangh'ola. Tulikuwa wanawake 9 na wanaume takribani 40. Asubuhi gari aina ya Tipper, lilikiwa na Askari Polisi, lilituchukua. Kwanza Tulielekea gereza la Malya. Tulipofika pale, tuliambiwa gereza limejaa hivyo wakaamua kutupeleka Mwangh'ola. Tukiwa njiani kuelekea Mwangh'ola, kuna Motokali ilitusimamisha. [Mkuu wa Upelelezi Wilaya], CID alituambia kuwa wachoka kupiga watu. Hivyo ikaamuliwa kuwa gari igeuze na kurudi gereza la Malya ambapo tulifika mida ya saa 10 jioni. Bahati mbaya tulikuta wafungwa wameshamaliza kula, hivyo tulilala pale gerezani bila kula.

Kulipokucha baada ya kunywa uji, tulipelekwa tena Mwangh'ola. Gari ile ile Tipper ilitupeleka huko, ambapo tulifika majira ya saa mchana. Eneo hilo la Mwangh'ola liko Porini ambapo kulikua na maghala mawili ya Pamba yaliyotelekezwa na jengo jingine dogo. Tuliamrishwa kusimama nje ya majengo hayo tukitazama mlango. Vijana wawili walipelekwa ndani. Tuliwasikia wakiwa wanatwanga. Kumbe walikuwa wakitwanga Pilipili. Wakati huo Polisi walikuwa na Fimbo na Bunduki wakituambia; 'Kila mtu asalie mtume wake. Umefika wakati wa Kujieleza'. Walituambia tutapigwa hata hadi tufe au tulemae.

Kisha tukaambiwa tuingie kulw ghalani walipokua wakitwanga ambapo tuliwekwa pamoja wanawake na wanaume. Tuliingia kwa kukimbia. Kwa kweli mimi nilidondoka kwenye msongamano ule. Wanawake wote waliingia. Kisha tukaamuliwa tuvue nguo zetu haraka na tusimame ukutani kwa kupanga mstari. Mzee mmoja, aliyekuwa mbele yangu, aliambiwa alale chini, alale chali[kulalia mgongo]. Alitii. Mmoja wetu aliamuliwa amuwekee yule Mzee Maji ya pilipili machoni, puani, mdomoni na sehemu za siri. Alikuwa hajahiriwa, govi lake lilivutwa nje na kuwekewa maji ya pilipili. Huku akipigwa na askari, aliamriwa asimame na kusogea pembeni. Mzee yule alikuwa akilia kwa maumivu ya pilipili na alipigwa ili aache kupiga kelele.

Zamu yangu ilifika. Niliamriwa kulala chali. Nilitii. Nami, niliwekewa pilipili mdomoni, machoni, masikioni, na sehemu za siri. Walichukua pilipili wakazibumba mithili ya mkate na kuzizamisha kwenye uke wangu. Kijana aliyekuwa akinizamishia pilipile zile, aliamrishwa aniwekee pia sehemu ya haja kubwa. Kijana yule alikuwa ni Mhaya. Hakua na namna zaidi ya kutii. Maumivu yalikuwa ni makali sana. Nilipojaribu kuzitoa pilipili, nilipigwa. Wote tuliwekewa pilipili. Na kuamriwa kuendelea kulalia mgongo huku Mguu mmoja tukiwa tumeuinua. Kisha tuliitwa jina mmoja mmoja na kuamriwa kuingia kwenye ghala la pili.

Niliitwa. Njiani kuelekea kwenye ghala la pili, kulikuwa na askari, lakini wamevaa kiraia. Mmoja alikuwa na fimbo na mwingine ana pilipili. Niliamriwa kukaa na kutanua miguu yangu na mikono. Nilitii. Nilipigwa kipigo kikali, mikononi na miguuni. Nikaulizwa: 'umepata wapi mali? Jangiri wee! Huku nikipigwa na kifimbo. Nikawaeleza namna nilivyopata mali zangu. Nikaulizwa Honda[pikipiki] yangu nimeipata vipi?. Nikawajibu kuwa niliinunua. Nikaachwa na kurudishwa kwenye jengo la pilipili huku nikiendelea kupigwa njia nzima. Na nikaamriwa kuchukua nguo zangu. Nikazichukua.

Kuna mmoja wetu aliitwa Kang'ombe Kaliji. Nilimfahamu, baada ya kuwa amepigwa na kushinswa kupanda gari mwenyewe. Jina lake nililifahamu, sababu askari walikuwa wakimuita na kumtaka aendelee kupigwa kama hataki kuinuka. Alikuwa akilia sana na kulalamikia maumivu makali. Ilibidi askari wenyewe wamnyanyue na kumpakia kwenye lori. Kabla ya vipigo, wote tuliweza kupanda kwenye lori wenyewe.

Hata alipopandishwa, Kang'ombe hakuweza kukaa kwenye seat mwenyewe. Ilibidi asaidiwe. Tulirudishwa kwenye gereza la Maswa. Tulipofishwa tuliamriwa kwenda kula. Sijui kama tulifika wote, maana kwa hofu sikuweza kutazama. Pale gerezani hatukukaa muda mrefu. Baada ya kula tuliondoka kuelekea Shinyanga. Kang'ombe tulikuwa naye, lakini alikuwa akitapika damu na alifia njiani. Tulipofika shinyanga, tulipelekwa gerezani. Tulishushwa na Mwili wa Kang'ombe uliwekwa kwenye mlango wa gereza. Lakni, Askari Magereza alikataa kuupokea mwili ule kuwa wao hawapokei maiti. Tuliuacha mwili ule pale mlangoni, na kupelekwa ndani ya gereza. Ilikuwa siku ya jumamosi. Tulikaa pale gerezani hadi jumatatu tulipoachiwa.

Kwa kweli tulifanyiwa matendo ya kikatili sana, mguu wangu wa kushoto ni mlemavu hadi sasa na sifurahii tenda tendo la ndoa. Uke wangu ulikuwa na majeraha kwa miaka karibu miwili na hadi sasa una makovu. Hamu ya ngono, nilishaipoteza.

Credit: Prof Issa Shivji.

Cc: Pascal Mayalla JokaKuu zitto junior Mshana Jr bagamoyo Yericko Nyerere
 
Miaka ya 1970, kulitokea wimbi la mauji ya waganga wa kienyeji mikoa ya Mwanza na Shinyanga. Wengi wa washukiwa waliachiwa huru baada ya kufikishwa mahakamani. Ndipo, Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa hiyo chini ya Uenyekiti wa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, waliagiza wote walioshukiwa na Mauji hayo wakamatwe na kuhojiwa. Wenye ushahidi wa kutosheleza wapelekwe mahakamani na usiojitosheleza waendelee kushikiliwa. Operation hii iliitwa Oparesheni Mauji na ilisimamiwa na maafisa Usalama kutokea Makao Makuu, Dar Es Salaam.

Oparesheni hii iliacha makovu makubwa sana. Mkoani Shnyanga, watuhumiwa 524 huku Mwanza 374 walikamatwa. Mahojiano yalihusisha mateso yasiyoelezeka. Mfano, Shinyanga, watu 10 walifariki katika mahojiano hayo, huku 109 wakishikiliwa. Wengine wengi walibaki vilema. Huku Vigogo wawili wa Usalama Mkoa, wakishitakiwa kwa mauji.

Habiba Shabani, muhanga wa Oparesheni hii anasimulia.

Tulikamatwa na kupelekwa kwa gari kwenda Kituo Cha Polisi Shinyanga. Tulilala pale kituoni, na Siku iliyofuata tulipelekwa Mahakamani. Sikupata nafasi ya kumuuliza Askari kuhusu kesi yangu sababu walikuwa wakali, wasioruhusu kuhojiwa. Mahakamani kesi ilisomwa, tukituhumiwa sisi watano, tumemuua Mwanamke ambaye jina lake halikutajwa. Iliamuliwa tuendelee kusalia mahabusu tukisubiri siku nyingine ya kutajwa kwa kesi. Tulipelekwa Gereza la Shinyanga. Sikumbuki tulikaa hapo gerezani kwa siku ngapi hadi tulipopelekwa tena mahakamani ambapo kesi ilipelekwa tena mbele kwa madai upelelezi unaendelea.

Mwezi mzima, tulikaa Gereza la Shinyanga. Kisha tukaondolewa hapo kupelekwa Mwangh'ola. Tulikuwa wanawake 9 na wanaume takribani 40. Asubuhi gari aina ya Tipper, lilikiwa na Askari Polisi, lilituchukua. Kwanza Tulielekea gereza la Malya. Tulipofika pale, tuliambiwa gereza limejaa hivyo wakaamua kutupeleka Mwangh'ola. Tukiwa njiani kuelekea Mwangh'ola, kuna Motokali ilitusimamisha. [Mkuu wa Upelelezi Wilaya], CID alituambia kuwa wachoka kupiga watu. Hivyo ikaamuliwa kuwa gari igeuze na kurudi gereza la Malya ambapo tulifika mida ya saa 10 jioni. Bahati mbaya tulikuta wafungwa wameshamaliza kula, hivyo tulilala pale gerezani bila kula.

Kulipokucha baada ya kunywa uji, tulipelekwa tena Mwangh'ola. Gari ile ile Tipper ilitupeleka huko, ambapo tulifika majira ya saa mchana. Eneo hilo la Mwangh'ola liko Porini ambapo kulikua na maghala mawili ya Pamba yaliyotelekezwa na jengo jingine dogo. Tuliamrishwa kusimama nje ya majengo hayo tukitazama mlango. Vijana wawili walipelekwa ndani. Tuliwasikia wakiwa wanatwanga. Kumbe walikuwa wakitwanga Pilipili. Wakati huo Polisi walikuwa na Fimbo na Bunduki wakituambia; 'Kila mtu asalie mtume wake. Umefika wakati wa Kujieleza'. Walituambia tutapigwa hata hadi tufe au tulemae.

Kisha tukaambiwa tuingie kulw ghalani walipokua wakitwanga ambapo tuliwekwa pamoja wanawake na wanaume. Tuliingia kwa kukimbia. Kwa kweli mimi nilidondoka kwenye msongamano ule. Wanawake wote waliingia. Kisha tukaamuliwa tuvue nguo zetu haraka na tusimame ukutani kwa kupanga mstari. Mzee mmoja, aliyekuwa mbele yangu, aliambiwa alale chini, alale chali[kulalia mgongo]. Alitii. Mmoja wetu aliamuliwa amuwekee yule Mzee Maji ya pilipili machoni, puani, mdomoni na sehemu za siri. Alikuwa hajahiriwa, govi lake lilivutwa nje na kuwekewa maji ya pilipili. Huku akipigwa na askari, aliamriwa asimame na kusogea pembeni. Mzee yule alikuwa akilia kwa maumivu ya pilipili na alipigwa ili aache kupiga kelele.

Zamu yangu ilifika. Niliamriwa kulala chali. Nilitii. Nami, niliwekewa pilipili mdomoni, machoni, masikioni, na sehemu za siri. Walichukua pilipili wakazibumba mithili ya mkate na kuzizamisha kwenye uke wangu. Kijana aliyekuwa akinizamishia pilipile zile, aliamrishwa aniwekee pia sehemu ya haja kubwa. Kijana yule alikuwa ni Mhaya. Hakua na namna zaidi ya kutii. Maumivu yalikuwa ni makali sana. Nilipojaribu kuzitoa pilipili, nilipigwa. Wote tuliwekewa pilipili. Na kuamriwa kuendelea kulalia mgongo huku Mguu mmoja tukiwa tumeuinua. Kisha tuliitwa jina mmoja mmoja na kuamriwa kuingia kwenye ghala la pili.

Niliitwa. Njiani kuelekea kwenye ghala la pili, kulikuwa na askari, lakini wamevaa kiraia. Mmoja alikuwa na fimbo na mwingine ana pilipili. Niliamriwa kukaa na kutanua miguu yangu na mikono. Nilitii. Nilipigwa kipigo kikali, mikononi na miguuni. Nikaulizwa: 'umepata wapi mali? Jangiri wee! Huku nikipigwa na kifimbo. Nikawaeleza namna nilivyopata mali zangu. Nikaulizwa Honda[pikipiki] yangu nimeipata vipi?. Nikawajibu kuwa niliinunua. Nikaachwa na kurudishwa kwenye jengo la pilipili huku nikiendelea kupigwa njia nzima. Na nikaamriwa kuchukua nguo zangu. Nikazichukua.

Kuna mmoja wetu aliitwa Kang'ombe Kaliji. Nilimfahamu, baada ya kuwa amepigwa na kushinswa kupanda gari mwenyewe. Jina lake nililifahamu, sababu askari walikuwa wakimuita na kumtaka aendelee kupigwa kama hataki kuinuka. Alikuwa akilia sana na kulalamikia maumivu makali. Ilibidi askari wenyewe wamnyanyue na kumpakia kwenye lori. Kabla ya vipigo, wote tuliweza kupanda kwenye lori wenyewe.

Hata alipopandishwa, Kang'ombe hakuweza kukaa kwenye seat mwenyewe. Ilibidi asaidiwe. Tulirudishwa kwenye gereza la Maswa. Tulipofishwa tuliamriwa kwenda kula. Sijui kama tulifika wote, maana kwa hofu sikuweza kutazama. Pale gerezani hatukukaa muda mrefu. Baada ya kula tuliondoka kuelekea Shinyanga. Kang'ombe tulikuwa naye, lakini alikuwa akitapika damu na alifia njiani. Tulipofika shinyanga, tulipelekwa gerezani. Tulishushwa na Mwili wa Kang'ombe uliwekwa kwenye mlango wa gereza. Lakni, Askari Magereza alikataa kuupokea mwili ule kuwa wao hawapokei maiti. Tuliuacha mwili ule pale mlangoni, na kupelekwa ndani ya gereza. Ilikuwa siku ya jumamosi. Tulikaa pale gerezani hadi jumatatu tulipoachiwa.

Kwa kweli tulifanyiwa matendo ya kikatili sana, mguu wangu wa kushoto ni mlemavu hadi sasa na sifurahii tenda tendo la ndoa. Uke wangu ulikuwa na majeraha kwa miaka karibu miwili na hadi sasa una makovu. Hamu ya ngono, nilishaipoteza.

Credit: Prof Issa Shivji.

Cc: Pascal Mayalla JokaKuu zitto junior Mshana Jr bagamoyo Yericko Nyerere
Ni unyama saana
 
Back
Top Bottom