Asilimia kubwa ya Watanzania wanajua usafi wa mwili na mazingira yao ila wengi ni wachafu na wasio na kinyaa kabisa!

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,023
144,381
Haihitaji kufanya utafiti bali kutazama tu jinsi jamii inayokuzunguka inavyoishi katika suala zima la usafi hasa usafi wa kitu kinachoingia mdomoni mwako na jinsi jamii isivyojali kabisa.

Watanzania wengi usafi wanaojua ni ule wa kuoga, kufua, kudeki na kufagia mazingira yanayozunguka nyumba zao na usipofanya haya jamii itakuwa mchafu na utasemwa tena sana lakini ni jamii hio hio isiyojali kabisa usafi wa kile kinachoingia mdomoni wala kuwa na kinyaa zaidi ya kinyaa cha kuona kinyesi tu.

Nitaeleza hapa kwa kutaja mifano kadhaa na ambayo hata wewe msomaji ni shahidi mzuri tena bila shaka na wewe ukiwa ni mmoja wa watu wenye tabia hizo.

Table manners
Ukiacha mambo mengine yanayohusiana table manners kama kusali kabla ya kuanza kula, kukaa mezani, n.k, kuna hii tabia mbaya ya kuongea wakati wa kula. Hapa ndio watu hulisha mata huku hakuna anaejali kabisa. Mtu mdomoni umejaza chakula huku mnaongea na tena mmekaa karibu karibu na huoni hata watu wakishituka.

Kwenye mabaa wanakokula nyama choma na bia au kitimioto na bia, hawa ndio kabisa hulishana mate kuliko fisi wanaogombania mzogo poroni. Yaani mtu mdomni anatafuna nyama halafu anatupia kinywaji huku anaongea basi ni mnvua ya mate kwenda mbele ila cha ajabu watu wanafurahia tu kama hakuna kinachotokea.

Binafsi kama naenda bar, napenda kukaa meza ya peke yangu na wakija watu natafuta sababu nahama nawachia meza hasa nikiona ni kundi la wanywa pombe(walevi) maana mambo ya kurushiana mate mimi siyawezi.

Kutonawa mikono baada ya kutoka chooni
Hili ndio tatizo kubwa miongoni mwa watanzania wengi na hii ni kwasababu hawana kinyaa. Unaweza kumuona mwanaume yuko smart kwelikweli au mwanadada mrembo sio kidogo ila akitoka chooni hana habari ya kunawa mikono na akinawa, basi ni mazingira yamemlazimisha kwa maana ya kuwa choo kipo sehemu ya public na akiingia au kutoka, anaonekana huku maji ya kunawa yakiwa nje ya choo hapo anakuwa hana ujanja vinginevyo hanawi.

Hata hivyo, unawaji wenyewe unaweza kuwa ni kichekeso kingine, kwani anafungua tu bomba ushahidi na kupitisha maji juu juu tena haraka haraka na sababuni anaweza asitumie kabisa hasa akiona hakuna anaemfuatilia halafu mkikutana mtaani anakupa mkono eti tusalimiane kumbe anakusambazai uchafu.

Ukitaka kuyaona haya,tembelea vyuoni (vyuo vikuu vikiwemo), nyumba za kupanga, kwenye nyumba za kupanga, vyoo vya njiani muwapo safarini, n.k.

Maajabu zaidi ni pale mtu huyo anatoka chooni anasuhuza mikono kisha anakamata tunda anakula na kama ni msichana wa kazi anaingia jikoni kwenda kupika au hata mama nyumbani anamtawaza mtoto kisha anasuhuza tu mikono na kuingia jikoni kuendelea na shughuli zake kama hakuna kilichotokea.

Kupiga chafya hadharani bila kuziba pua na mdomo
Hii tabia nayo ni moja ya kero kubwa sana miongoni mwa watanzania wengi. Mtu yuko sehemu ya public na amezungukwa na wenzake mfano ofisini, darasani, mezani,n.k ila anapiga chafya kama vile yuko pekee yake na wala hazibi pua wala mdomo. Cha kushangaza zaidi, katika watu kumi, unaweza kujikuta uko peke yako unaekereka wenzio wanaona sawa tu utadhani sio binadamu bali ni kikundi cha mifugo kama vile mbuzi, kondoo .n.k mmoja wao ndio kapiga chafya.

Kingine kinachokera ni tabia ya kupiga chafya kwa kutumia kiganja cha mkono badala ya kiwiko hivyo kusambaza uchafu kwa kila unaempa mkono au kwa kila anaetumia kifaa cha ku-share kama mouse, pen, n.k. Katika hili, pengine wa kulaumiwa zaidi ni yule mtu alieleta utamaduni wa kupiga chafya na kuziba pua na mdomo kwa kutumia kiganja na bila shaka hii tabia ilichangia sana kwenye kusambaza ugonjwa wa corona.

Kwa Mama Ntile na kwenye mighahawa

Hayo niliyoyaeleza hapo juu unaweza kuyaona na kuyadhibitisha katika sehemu wanzouza chakula kama vile kwa Mama Nile na kwenye mighahawa kwa ujumla.

Kwa mfano, ni kawaida kuona Mama Ntile anasukuma chapati kisha anapokea hela halafu anachukua chapati anakupatia au anasukuma chapati huko anakohoa (hakohilii pembeni) huku anaendelea kuhudumia huku wateja nao wakipiga nae strory wakiwa comfortable kabisa kama hakuna kinachotokea na wewe utaehoji, ukiondoka tu unapigwa jungu kwa unajifanya msafi, n.k.

Kwa kifupi, haya ni machache na hawa ndio watanzania ambao usipofua, usipofagia mazingira au kudeki nyumba hata kwa siku moja au mbili, watakusema kuwa wewe ni mchafu, ila hayo mengine kwao ni sehemu ya maisha na ukihoji utaambiwa unajifanya msafi (alietuloga kwa hakika alikuwa fundi).

Katika hili, tusisingizie umasikini au mazingira magumu wakati wengi hii ni hulka tu na ndio maana hata vyuo vikuu utayaona mambo kama haya hata kama mazingira kwenye mabweni, vyuoni na sehemu za kula ni rafiki kwa watu kunawa mikono kabla ya kula, baada ya kula na hata watokapo chooni.

Wasanii acheni kuimba nyimbo za mapenzi tu bali imbeni nyimbo za kukemea hizi tabia ila sijui itawezekana vipi kwa hili kutokea wakati wasanii wenyewe ni sehemu ya hiyo jamii.

Tuna safari ndefu sana.
 
Ukweli mchungu huu,

Kero nyingine nisiyoipenda; mtu anakusogelea kuanza kukunong'oneza huku ananuka mdomoni dah!

Mimi Huwa sipendi sana hili jambo,

Ukitaka kumnong'oneza mtu ziba kidogo mdomo wako kwa kiganja Cha mkono huku ukiwa na umbali wa sentimita 15 hivi Toka sikio lake.
 
Ukweli mchungu huu,

Kero nyingine nisiyoipenda; mtu anakusogelea kuanza kukunong'oneza huku ananuka mdomoni dah!

Mimi Huwa sipendi sana hili jambo,

Ukitaka kumnong'oneza mtu ziba kidogo mdomo wako kwa kiganja Cha mkono huku ukiwa na umbali wa sentimita 15 hivi Toka sikio lake.
Hii inakera sana aisee
 
Back
Top Bottom