Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Mambo ya 50/50 binafsi mnitoe siyatakiiii

Kwa mwanaume kila kitu kinaeleweka. Twende na mfumo dume au usawa wa kijinsia mwanaume lazima alete kitu mezani. Kwahiyo shida sio mwanaume unaemuandama wewe. Shida ni mwanamke ambae bado hajajua achague kipi kati ya usawa wa kijinsia au mfumo dume for once and for all.
Nadhani unavichanganya hivyo vitu kwa makusudi ama kwa kutokujua, usawa wa kijinsia ni muhimu kwa sababu una mpa haki sawa kila mmoja na katika haki hizo ikiwemo kila mmoja kusimama kwenye majukumu yake kulingana na nature yake, usawa wa kijinsia sio wa kukandamiza bali kuweka mizani sawa,

Mfumo dume ni mfumo kandamizi juu ya mwanamke lakini katika huo huo mfumo bado haujayatoa majukumu ya kila mmoja wao, mwanaume asimamie misingi yake na mwanamke pia.
 
Mahusiano yetu kizamani,, lakini kenge wangu pamoja na yote mapito ye anasimama katika ubaba.

Ubaba kwa maana ya kuhudumia!!!! Mi miaka yote sijawahi kuambiwa changia hili au sijui hii jukumu lako.
Nikiona kakwama sana natoa au naachia asote hata kama Hela ninayo.
Ndo ukanilia buyu expert!
 
Guys kuna raha kua Mwanamke na raha ya Mwanamke kuhudumiwa,
acheni sasa niwaambie mimi ni yule mwanamke hata nikipata mshahara sasa hivi, bado nitapiga simu kwa kaka zangu (wananipenda sana lastborn wao) wanitumie hela ya chips au icecream,
Siwezi kwenda lunch na kuna wanaume halafu mimi nilipe bill hata kama ni yangu, hapana nitatulia tuliii wanaume walipie,😐

Kuna siku ilikua lunch na co-workers sasa bill ilivyofika mdada mmoja naona anafungua wallet weeh acha nimpige kofi la bega, akashtuka nikamwambia "tulia ufurahie uanamke wako" akacheka akaweka wallet chini,🙃

Tukija nyumbani ndio kabisaaaa siwezi kubeba majukumu ya kununua chakula na kulipa bills, nope! labda kununua vitu vidogo vidogo kama chumvi na viberiti au snacks zangu, lol

Haya mambo ya 50/50 yaishie kwenye mabiashara hukooo ila kwenye mahusiano hapana jamani kila mtu asimamie majukumu yake yanayomuhusu, mimi jukumu langu ni kuleta utulivu, nuru na amani nyumbani,
Mtauliza sasa wewe mshahara wako unaufanyia nini sawa nitajibu, nanunua vitu vidogo vidogo kama mapambo ya ndani, kufix issues ndogo ndogo zitakazojitokeza na kuspend kwenye mambo yangu,🥰 wanawake tuna vitu vingi jamani na pesa kwetu haijawahi kutosha,😂

Ewe mwanamke unayejiita mwanamke wa shoka, unayevuja jasho na damu ili kuhudumia familia kwanza nakupongeza sana ila kama ukipata nafasi ya kufanyiwa jiachie ufanyiwe, Mwanamke ni pambo la dunia, kaumbiwa kutunzwa, kudekezwa, kupendwa, kubembelezwa, mwanamke anatakiwa awe laini laini sio wanaume wapo wewe mwanamke unabeba ngazi unaparamia ukuta kuweka umeme au unapanda kwenye stuli kufunga kamba za nguo jamani mtakuja kutenguka nyonga mshindwe kutoa raha kwa my zenu,🙄

Binafsi hizo 50/50 zenu pelekeni hukoooooooo mimi ni old school naelewa uanamke wangu unathamani kiasi gani.
Tchaooooo
VIzuri sana, lakini bado hujataja majukumu yako, kwsbb anayeleta utulivu na Amani ni Mungu
Wewe majukumu yako ni yapi kwenye ndoa?
 
Nadhani unavichanganya hivyo vitu kwa makusudi ama kwa kutokujua, usawa wa kijinsia ni muhimu kwa sababu una mpa haki sawa kila mmoja na katika haki hizo ikiwemo kila mmoja kusimama kwenye majukumu yake kulingana na nature yake, usawa wa kijinsia sio wa kukandamiza bali kuweka mizani sawa,

Mfumo dume ni mfumo kandamizi juu ya mwanamke lakini katika huo huo mfumo bado haujayatoa majukumu ya kila mmoja wao, mwanaume asimamie misingi yake na mwanamke pia.
Equal rights comes with equal responsibilities. Kama mwanzo ulikua unawekwa pembeni kwenye suala la ajira ni sahihi kwa mwanaume kuwajibika na bill zote. Ila kwa sasa na wewe unajumuishwa kwenye suala la ajira maana yake bill zinagawanywa.

Kuwa na ajira maana yake automatically unaondolewa kwenye kundi la watu tegemezi. Utawajibika kujuhudumia mwenyewe na kuchangia kila unachotumia. Embu niambie nini maana ya mwanamke kuwa na kipato kama mahitaji yake na bill zote ni juu ya mwanaume. Acheni ubinafsi.
 
50/50 imeletwa kuja kuondoa utulivu kwenye taasisi ya Ndoa

Kwa maoni yangu, ndoa inaweza kutulia iwapo mke na mume wakaishi kama ilivyokuwa wanaishi Wazee wetu miaka ya 1970/1980

Mke ni Mama wa nyumbani, na Mume ni provider wa kila kitu

Hayupo mwanaume ambaye anaweza kuvumilia mke wake anatoka saa 12 asubuhi anawahi kazini na yeye anatoka muda huo kwenda ofisini halafu mwisho wa siku mke anaomba hela ya chakula nyumbani ama hela ya kujaza gesi

Ukitaka hivyo, mke unatakiwa kubaki mama wa nyumbani, mume akuhudumie kila kitu huku wewe ukibeba jukumu la kumzalia mumeo na kumlelea watoto wenu

50/50 ndiyo kaburi la ndoa nyingi, ndiyo chanzo cha usaliti huko makazini, ndiyo chanzo cha mke kumzalia mumewe mtoto mmoja ama wawili kisa kubanwa na kazi
 
Mbona nimeshasema huko juu, mwanamke ana vitu vingi sana na pesa haijawahi kutosha, kila kiungo cha mwanamke kina gharama kinatakiwa kigharamiwe kuanzia nywele hadi nyayo, suala la kununua vitu vya ndani, kulipa bills na ada za watoto ni vya mwanaume kama unataka heshima lakini kama unataka wote muwe makambale ndani baba ndevu mama ndevu basi gawaneni hizo huduma, ndio maana tunaona ndoa nyingi sasa hivi watu wanaishi kwa mashindano.
 
50/50 imeletwa kuja kuondoa utulivu kwenye taasisi ya Ndoa

Kwa maoni yangu, ndoa inaweza kutulia iwapo mke na mume wakaishi kama ilivyokuwa wanaishi Wazee wetu miaka ya 1970/1980

Mke ni Mama wa nyumbani, na Mume ni provider wa kila kitu

Hayupo mwanaume ambaye anaweza kuvumilia mke wake anatoka saa 12 asubuhi anawahi kazini na yeye anatoka muda huo kwenda ofisini halafu mwisho wa siku mke anaomba hela ya chakula nyumbani ama hela ya kujaza gesi

Ukitaka hivyo, mke unatakiwa kubaki mama wa nyumbani, mume akuhudumie kila kitu huku wewe ukibeba jukumu la kumzalia mumeo na kumlelea watoto wenu

50/50 ndiyo kaburi la ndoa nyingi, ndiyo chanzo cha usaliti huko makazini, ndiyo chanzo cha mke kumzalia mumewe mtoto mmoja ama wawili kisa kubanwa na kazi
Kumbe 50/50 inaingia kwenye mwanamke kufanya kazi! kwa maana ilitakiwa mwanamke asisome wala asifanye kazi, hapana mnakosea mwanamke kupata elimu ni HAKI yake na mwanamke kufanya kazi ni HAKI yake pia, mwanamke kuolewa ni HAKI yake na kulea watoto na mume wake ni WAJIBU wake, mwanaume kutunza familia ni WAJIBU wake bila kuangalia nini mkewe anaingiza, siku akikwama mke atamboost lakini sio mke na mume mkae mezani muanze kugawana majukumu ya kutunza familia, hapana huo ni ukandamizaji wa mwanamke abebe mimba, azae kwa uchungu na bado alipie majukumu ya familia, HAPANAAAAAA
 
Back
Top Bottom