Maisha yangu nimeyaharibu mwenyewe

Adriel Vin

Senior Member
Jun 25, 2020
148
748
Habari wanaJF, bila shaka kila anayesoma hapa ni mzima na afya, na kama sio Mungu akupe lililo hitaji la moyo wako🙏

Mimi ni kijana wa miaka 30. Nimezaliwa mkoa wa Mwanza, nimepata elimu yangu ya msingi huko mkoani Mwanza. Nilimaliza kwa ufaulu wa kawaida lakini nilifanikiwa kuchaguliwa na kuendelea na elimu ya sekondari huko huko mkoani Mwanza.

Mimi ni mtoto wa 2 kati ya 3 ambao tumelelewa kwa pamoja, japo nna dada zangu wengine wawili ambao hatukukuwa pamoja muda mwingi (Baba alikuwa na watoto wawili kabla hajaoa) so jumla yetu tuko watano (5)

Maisha ya nyumbani yalikuwa ya kawaida tu sio matajiri na sio masikini. Na nimekua kwenye malezi ya maadili ya kiafrika kabisa.

To cut it short

Kwenye kukua kwetu hatukuwa tukiomba hela kwa baba maana tulikua tunamwogopa, mzee alikua mkali balaa so kila kitu tulikua tukiongea na mama. Mama alikua mtu mwenye upendo sana kwa wanae na alipambana kwa namna yoyote kuhakikisha watoto wake tunasoma na kuwa vijana bora. Pesa ya kula shule, nauli, madaftari na kila kitu tulikua tukipewa na mama. Sio kwamba Baba hakuwa anatoa chochote kabisa lakini najaribu tu kuonyesha kwamba Mama ndo alikuwa rafiki yetu sana kuliko mzee. Japo fimbo na vibao vingi tumepigwa na mama kuliko mzee.

Nilipomaliza darasa sa saba, Kaka yangu alikuwa form 2 kwa wakati huo na alikuwa akisoma shule ya private. Kwa upande wangu matokeo ya darasa la saba sikuweza kuchaguliwa first selection. (Sikuwa na alama za kutosha) kama nilivyosema hapo juu nilifaulu kawaida ntafafanua mbele.

Mama alinipeleka shule ya private ambayo kaka yangu anasoma kwa wakati huo na nilifanya interview na kupewa majibu ndani ya siku 2 kuwa nimefaulu naweza kujiunga na shule hiyo ili kuendelea na elimu ya sekondari.

Nakumbuka baada ya mwezi hivi (sina uhakika sana) second selection ilitoka na nilikuwa nimechaguliwa shule flani iko wilaya ya Ilemela (Jina nahifadhi). Ilikuwa ni shule mpya kabisaa kwa kipindi hicho ziilikuwa na jina maarufu zikiitwa shule za kata. So nilichaguliwa shule ya kata.

Mama alisema niendelee kusoma kwenye shule hiyo ya private lakini niliona kama hayuko sahihi maana hali yake ya uchumi haikuwa nzuri hata ada najua alikopa. Ila kwa umri ule nisingeweza kumshauri kitu zaidi ya kusema sawa mama. Na maisha yaliendelea.

Mama yangu alikuwa mtu wa upendo sana na mchakarikaji. Niseme tu nilikuwa nampenda sana mama na nilikuwa ni yule mtoto wa mama (mamaz boy). Ilipita wiki kadhaa na mama alianza kuumwa serious. Alikuwa akilalamika siku za nyuma lakini wakati huu alisisitiza kuwa hajisikii vizuri hivyo alituaga na kuondoka kwenda hospital kwa matibabu.

Aliondoka majira kama ya saa sita nakumbuka na aliahidi angerejea baada ya matibabu.
Kuna hospital moja ipo Mwanza kwa kipindi hicho ilikua ikiitwa Mission, iko maeneo ya Ghana kama sikosei, sina hakika kama bado iko pale hadi leo.

Taarifa za mama kuumwa hazikuwa nzuri kwangu maana Mama hakufanikiwa kurejea nyumbani siku hiyo.
Mimi (Nijiite Amani…Sio jina halisi) nilikua yule mtoto ambaye hata mama akitoka ikifika saa 3 usiku hajarudi basi wasiwasi na uoga ulikua unakua mwingi.

Sasa hii siku mama hakurudi kabisa na nilikuwa na wasiwasi sana hadi hapo mama mdogo alipokuja home majira ya jioni ya kutupa habari kuwa mama amelazwa katika hospital hiyo ya Mission. Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri ilikuwa ni weekend.

Maisha yaliendelea na tulikuwa tukienda kumwona mama. Jumatatu tulienda shule kama kawaida, nilikuwa nikiondoka na kaka yangu kwani alikuwa ananizidi madarasa 2 hivyo alikuwa ananiongoza vyema tu. Kaka yangu aliwahi sana kujitambua hivyo hakuwa msumbufu sana kwa mama kama mimi.

Mimi nilikuwa hata nikitoka shule sina muda wa kusoma, ni michezo hadi usiku so hata maendeleo yangu shule hayakua mazuri sana ukiringanisha na kaka yangu.

Mama aliendelea kupatiwa matibabu kama siku 3 hivi lakini hakuonyesha nafuu hivyo alipewa rufaa kwenda Hospital ya Bugando.

Nilikuwa na ratiba kila nikitoka shule naunga moja kwa moja hadi Bugando kwenda kumsalimia mama. Nilikuwa natoka shule saa nane na nusu hivyo hadi kufika saa kumi muda wa kuona nilikuwa nimeshafika pale Hospital.

Kuna muda nilikuwa nazuiliwa na walinzi maana kwa kipindi hicho walikuwa na utaratibu wa kuzuia watoto kwenda kuona wagonjwa. Sasa mimi na umbo langu dogo dogo nilikuwa naonekana mdogo so kuna muda sikuwa nafanikiwa kuingia hadi niwe na mtu mzima.

Hali ya mama haikuwa nzuri kwakweli maana baada ya kama siku kumi hivi, Nakumbuka hiyo siku nilienda kumwona mama nikakuta amewekewa mashine ya Oxygen, ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza naona mtu kawekewa ile mirija puani.

Nakumbuka nilianza kulia pale na mama mdogo alinitoa nje maana nilikuwa nalia alafu mama ananiangalia wakati huo alikuwa hawezi hata kutoa sauti ukaisikia so alikua ananiangalia na nilikua naona kabisa anaumia kuona nalia.

Tulirudi nyumbani siku hiyo na usingizi ulikua wa shida sana nawaza mama amekuwaje. Hali ya home pia haikua nzuri kwani kwa kipindi chote hicho mama hakuwepo nyumbani.

Pale nyumbani tulikuwa na kiduka ambacho kilikuwa kinaendeshwa na mama na ndipo hapo tulikua tukipata hela ya nauli pamoja na ile ya kula shule. So wakati wote ambao mama hakuwepo hata mapato dukani yalipungua kwani bidhaa nyingi zilikua zimeisha usimamizi hakua mzuri.

Ni baada ya kama siku 2 tu nikiwa nimetoka hospital kumwona mama. Wakati huo sikua naruhusiwa tena kwenda kumwona kutokana na kile kitendo cha kulia.

Hii siku nilitoka shule nikaenda moja kwa moja home lakini ilipofika jioni baadhi wa watu waliotoka hospital walinipa taarifa kuwa hali ya mama bado si nzuri.

Usiku wake baba alipigiwa simu akiambiwa mama hali yake ni mbaya na alienda moja kwa moja hospital.
Baada ya masaa kama mawili nilishtuka kwa kelele za vilio kutoka kwa mama zangu wadogo.
Mama alikua amefariki tayari

NITAENDELEA… Leo Leo

Usiku wake baba alipigiwa simu akiambiwa mama hali yake ni mbaya na alienda moja kwa moja hospital.
Baada ya masaa kama mawili nilishtuka kwa kelele za vilio kutoka kwa mama zangu wadogo.
Mama alikuwa amefariki tayari
 
Nakupa elimu ndogo kabisa, Ni baba yenu ndie alikuwa anatafuta hela za kuwalipia ada shuleni, nguo, chakula, n.k. mama yenu alikuwa anapewa ila mkimuona anavyowalipia / kuwapa mnadhani ni zake.

Nani kama mama ni misemo ya watoto / vijana ambao bado hawana familia zao kujua mfumo kamili wa jinsi mambo yanavyokwenda
 
Habari wanaJF, bila shaka kila anayesoma hapa ni mzima na afya, na kama sio Mungu akupe lililo hitaji la moyo wako

Mimi ni kijana wa miaka 30. Nimezaliwa mkoa wa mwanza, nimepata elimu yangu ya msingi huko mkoani mwanza. Nilimaliza kwa ufaulu wa kawaida lakini nilifanikiwa kuchaguliwa na kuendelea na elimu ya sekondari huko huko mkoani mwanza.

Mimi ni mtoto wa 2 kati ya 3 ambao tumelelewa kwa pamoja, japo nna dada zangu wengine wawili ambao hatukukua pamoja muda mwingi (Baba alikua na watoto wawili kabla hajaoa) so jumla yetu tuko watano (5)

Maisha ya nyumbani yalikua ya kawaida tu sio matajiri na sio masikini. Na nimekua kwenye malezi ya maadili ya kiafrika kabisa.

To cut it short

Kwenye kukua kwetu hatukuwa tukiomba hela kwa baba maana tulikua tunamwogopa, mzee alikua mkali balaa so kila kitu tulikua tukiongea na mama. Mama alikua mtu mwenye upendo sana kwa wanae na alipambana kwa namna yoyote kuhakikisha watoto wake tunasoma na kuwa vijana bora. Pesa ya kula shule, nauli, madaftari na kila kitu tulikua tukipewa na mama. Sio kwamba Baba hakua anatoa chochote kabisa lakini najaribu tu kuonyesha kwamba Mama ndo alikua rafiki yetu sana kuliko mzee. Japo fimbo na vibao vingi tumepigwa na mama kuliko mzee.

Nilipomaliza darasa sa saba, Kaka yangu alikua form 2 kwa wakati huo na alikua akisoma shule ya private. Kwa upande wangu matokeo ya darasa la saba sikuweza kuchaguliwa first selection. (Sikua na alama za kutosha) kama nilivyosema hapo juu nilifaulu kawaida… ntafafanua mbele.

Mama alinipeleka shule ya private ambayo kaka yangu anasoma kwa wakati huo na nilifanya interview na kupewa majibu ndani ya siku 2 kuwa nimefaulu naweza kujiunga na shule hiyo ili kuendelea na elimu ya sekondari.

Nakumbuka baada ya mwezi hivi (sina uhakika sana) second selection ilitoka na nilikua nimechaguliwa shule flani iko wilaya ya ilemela (Jina nahifadhi). Ilikua ni shule mpya kabisaa kwa kipindi hicho zilkua na jina maarufu zikiitwa shule za kata. So nilichaguliwa shule ya kata.

Mama alisema niendelee kusoma kwenye shule hiyo ya private lakini niliona kama hayuko sahihi maana hali yake ya uchumi haikua nzuri hata ada najua alikopa. Ila kwa umri ule nisingeweza kumshauri kitu zaidi ya kusema sawa mama. Na maisha yaliendelea.

Mama yangu alikua mtu wa upendo sana na mchakarikaji. Niseme tu nilikua nampenda sana mama na nilikua ni yule mtoto wa mama (mamaz boy). Ilipita wiki kadhaa na mama alianza kuumwa serious. Alikua akilalamika siku za nyuma lakini wakati huu alisisitiza kuwa hajisikii vizuri hivyo alituaga na kuondoka kwenda hospital kwa matibabu.
Aliondoka majira kama ya saa sita nakumbuka na aliahidi angerejea baada ya matibabu.
Kuna hospital moja ipo Mwanza kwa kipindi hicho ilikua ikiitwa Mission, iko maeneo ya Ghana kama sikosei, sina hakika kama bado iko pale hadi leo.

Taarifa za mama kuumwa hazikua nzuri kwangu maana Mama hakufanikiwa kurejea nyumbani siku hiyo.
Mimi (Nijiite Amani…Sio jina halisi) nilikua yule mtoto ambaye hata mama akitoka ikifika saa 3 usiku hajarudi basi wasiwasi na uoga ulikua unakua mwingi. Sasa hii siku mama hakurudi kabisa na nilikua na wasiwasi sana hadi hapo mama mdogo alipokuja home majira ya jioni ya kutupa habari kuwa mama amelazwa katika hospital hiyo ya Mission. Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri ilikua ni weekend.

Maisha yaliendelea na tulikua tukienda kumwona mama. Jumatatu tulienda shule kama kawaida, nilikua nikiondoka na kaka yangu kwani alikua ananizidi madarasa 2 hivyo alikua ananiongoza vyema tu. Kaka yangu aliwahi sana kujitambua hivyo hakuwa msumbufu sana kwa mama kama mimi.
Mimi nilikua hata nikitoka shule sina muda wa kusoma, ni michezo hadi usiku so hata maendeleo yangu shule hayakua mazuri sana ukiringanisha na kaka yangu.

Mama aliendelea kupatiwa matibabu kama siku 3 hivi lakini hakuonyesha nafuu hivyo alipewa rufaa kwenda Hospital ya Bugando.
Nilikua na ratiba kila nikitoka shule naunga moja kwa moja hadi Bugando kwenda kumsalimia mama. Nilikua natoka shule saa nane na nusu hvyo hadi kufika saa kumi muda wa kuona nilikua nimeshafika pale Hospital.
Kuna muda nilikua nazuiliwa na walinzi maana kwa kipindi hicho walikua na utaratibu wa kuzuia watoto kwenda kuona wagonjwa. Sasa mimi na umbo langu dogo dogo nilikua naonekana mdogo so kuna muda sikua nafanikiwa kuingia hadi niwe na mtu mzima

Hali ya mama haikua nzuri kwakweli maana baada ya kama siku kumi hivi, Nakumbuka hiyo siku nilienda kumwona mama nikakuta amewekewa mashine ya Oxygen, ndo ilikua mara yangu ya kwanza naona mtu kawekewa ile mirija puani. Nakumbuka nilianza kulia pale na mama mdogo alinitoa nje maana nilikua nalia alafu mama ananiangali wakati huo alikua hawezi hata kutoa sauti ukaisikia so alikua ananiangalia na nilikua naona kabisa anaumia kuona nalia.

Tulirudi nyumbani siku hiyo na usingizi ulikua wa shida sana nawaza mama amekuwaje. Hali ya home pia haikua nzuri kwani kwa kipindi chote hicho mama hakuwepo nyumbani.
Pale nyumbani tulikua na kiduka ambacho kilikua kinaendeshwa na mama na ndipo hapo tulikua tukipata hela ya nauli pamoja na ile ya kula shule. So wakati wote ambao mama hakuwepo hata mapato dukani yalipungua kwani bidhaa nyingi zilikua zimeisha usimamizi hakua mzuri.

Ni baada ya kama siku 2 tu nikiwa nimetoka hospital kumwona mama. Wakati huo sikua naruhusiwa tena kwenda kumwona kutokana na kile kitendo cha kulia.
Hii siku nilitoka shule nikaenda moja kwa moja home lakini ilipofika jioni baadhi wa watu waliotoka hospital walinipa taarifa kuwa hali ya mama bado si nzuri.
Usiku wake baba alipigiwa simu akiambiwa mama hali yake ni mbaya na alienda moja kwa moja hospital.
Baaba ya masaa kama mawili nilishtuka kwa kelele za vilio kutoka kwa mama zangu wadogo.
Mama alikua amefariki tayari…..

NITAENDELEA… Leo Leo
😩 so sad.
 
Wakati nasoma hii story yako machozi yalikuwa yananilengalenga.

Anyway, pole sana kwa tukio hilo.

Sent from my V2207 using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom