Kijana jitahidi usijipoteze ukiwa na umri kati ya miaka 20-30

Feb 4, 2024
67
204
KIJANA JITAHIDI USIJIPOTEZE UKIWA NA UMRI KATI YA MIAKA 20-30

Katika makuzi kuna mgawanyo wa hatua takribani nne ambapo karibu kila mtu kwa kudra za mwenyezi Mungu huzipitia, Vipindi hivyo hugawanywa kwa kuzingatia umri na matukio yake na pia kila kipindi ni muhimu zaidi katika kuandaa kipindi kingine hivyo kumbe hutegemeana. Japo hatua hizo za makuzi hutegemeana ila ipo hatua yenye changamoto nyingi na iliyomuhimu sana na mtu usipokuwa makini utajikuta unajipoteza na ukiwa makini zaidi utajipata.

UMRI KATI YA MWAKA 1 MPAKA MIAKA 18.
Huu ni umri wa kujidanganya sana na kutengeneza malengo ya ukubwani na kwanini kujidanganya? Kwa sababu unakuwa unaona kila kitu kitawezekana bila kusubiriwa kwa mfano: Utaona utamaliza shule mpaka chuo na baada ya kumaliza tu utapata kazi ya kuajiriwa na pengine ukipata kazi tu utalipa fadhila kwa waliokusomesha /kukusaidia na kisha utaoa/kuolewa na ndani ya mwaka huo huo utapata mtoto wako wa kwanza.

Hivi ndivyo wengi tulipanga tukiwa na umri huo na walio kwenye umri huo pia wapo wanapanga wakiamini maisha ni mstari mnyoofu hivyo kila kitu kitaenda bila shaka yoyote, Je ni vibaya kupanga?

Sio vibaya ndio maana awali nikatangulia kusema kuwa huu ndio umri wa kujiona ukiwa mkubwa utakuaje, Kwanini ni umri wa kujidanganya? Tuone hatua ya pili kisha hili jibu litapatikana.

UMRI KATI YA MIAKA 20- 30 (UMRI WA UHALISIA)
Huu ndio umri wa kuona vitu kwa vitendo kwa namna kijana alivyojichora akiwa na miaka 18 kurudi nyuma. Kwenye umri huu ndio utaona maisha ni mstari mnyoofu ama ni mstari wenye kona nyingi? Katika umri huu kwa wale ambao walienda shule wengi humaliza elimu zao mpaka za vyuoni na kikawaida ndipo wanakaribishwa rasmi mtaani na hapa ndipo uhalisia unaonekana.

Katika umri huu mambo mengi yanakuja kinyume na namna mtu alivyofikiri japo yanatimia ila kuna kitu kinaitwa Subira ndio hasa kinafaa kitumike kwenye umri huo kwa sababu ukiwa mtu wa pupa lazima utakata tamaa na kuona maisha ni magumu sana.

Sio ajabu kumaliza shule ukajikuta unapata kazi baada ya miaka mitano tofauti na ulivyojiona kuwa utamaliza leo na kesho utaitwa kazini.
Sio ajabu ukaoa/ kuolewa nje umri uliojipangia kwa mfano ulijua utamaliza tu chuo utaingia kwenye familia ila unamaliza unakaa tena miaka mitano mbele ndio unaanza familia.

Sio ajabu ukaingia kwenye familia mapema tu ila ukakutana na changamoto za uzazi ukajikuta unapata mtoto wa kwanza baada ya miaka 7 ya ndoa tofauti na ulivyoona ukiingia tu leo kwenye ndoa basi kesho tayari mimba na hata usijaliwe kupata maana yote ni mipango ya Mungu.

Sio ajabu ukavuka miaka 20 bila kuwa na kiwanja wala nyumba ukiwa bado umepanga au hata kuishi kwa wazazi tofauti na ulivyojiona kumiliki nyumba na usafiri ukiwa kati ya miaka 20 tu.
Hayo ni baadhi ya matukio ambayo yapo na wengi huyapitia na ndio inakuja ile sababu ya huu umri kuitwa umri wa UHALISIA, na huu umri unatufundisha kuwa maisha sio mstari mnyoofu na kutokuwa mstari mnyoofu haimaanishi kuwa malengo hayawezekani la hasha bali subira inatakiwa sana katika umri huo la sivyo utajipoteza kwa kuwa mtu mwenye haraka na mwisho wa siku unaishi maisha yasiyo ya uhalisia wako kwa mfano ulihisi utapata nyumba na gari haraka sasa ili kutaka yawezekana unaingia kwenye wizi au kwa waganga wa kienyeji wanakwambia utoe kafala mwisho wa siku unaishia gerezani.

Umri huu hutakiwi kuwa na haraka bali kuwa na juhudi tu za kupambania ndoto zako na sio lazima zije kwenye mstari mnyoofu ila ikitokea zinakuja kwenye unyoofu basi shukuru Mungu kwa hilo maana upo kwenye kundi la wachache ambao mambo yao yanakuwa kwenye unyoofu pasi na chenga.Usikubali ujipoteze hapa kwa sababu ukijipoteza kuna uwezekano mkubwa nyakati zitazofuata zisikusaidie kujipata tena.

UMRI KATI YA MIAKA 40- 55.
Huu ni umri wenye matukio mawili makubwa la kwanza ni kukubali matokeo huku ukilazimisha uendelee kuonekana kijana wa miaka 30 ,hii ni wale ambao walikata tamaa na kuona maisha ndio haya haya hivyo wanaamua kuridhika lakini changamoto nyingine inayowakabiri ni kupingana na umri yaani hawataki kukubali kuwa wao ni watu wazima na utajigundua hivyo pale ukianza kuona unalazimisha kufanya vitu visivyo endana na umri wako, kitaalamu hiki kipindi kinaitwa mid age crisis (kuupinga utu uzima).

Tukio la pili ni wale ambao hawakukata tamaa hivyo wanaendelea kujitafuta na uwezekano wa kujipata upo.

Changamoto kubwa kwenye umri huu ni kuwa majukumu yanakuwa mengi sana hivyo utegemezi unakuwa mkubwa hivyo kama hukujipanga vizuri utakuwa unapata pesa ila zinaishia kwa wategemezi wako.

UMRI KUANZIA MIAKA 60 KUENDELEA.
Hapa ni uzee tu na kupumzika ijapo bado kuna wengine wataendelea na kutafuta tu kama matokeo ya kushindwa kutumia ujana wao vyema au kushindwa kuweka mikakati mizuri ujanani.

Makala hii imeandikwa na Mwanasayansi Saul kalivubha
+255652 134707
 
Mbona matajiri wengi wanakufa 70's ...Labda uwe unategemea ajira za mshahara 3.5 mil kushuka chini...Ila una mikiki ya biashara ndefu hata miaka 80 unafika tena ukiwa bado na malengo
 
Umri sio kitu Ila wakati Wa MUNGU ndo kila kitu
WATU wanapata stress kisa ni kutafuta mafanikio kwa kutumia umri wakati umri upo out of your control.

Mtegemee MUNGU ishi Katika haki na UPENDO age is just a number
Kufanya kazi Kwa bidiii na kumtegemea Mungu. huwezi kuusubiria wakati wa Mungu wakati uko umekaa nyumbani,amka fanya kitu na Mungu atakuonekania huko kazini.
 
Umri sio kitu Ila wakati Wa MUNGU ndo kila kitu
WATU wanapata stress kisa ni kutafuta mafanikio kwa kutumia umri wakati umri upo out of your control.

Mtegemee MUNGU ishi Katika haki na UPENDO age is just a numbe

Umri sio kitu Ila wakati Wa MUNGU ndo kila kitu
WATU wanapata stress kisa ni kutafuta mafanikio kwa kutumia umri wakati umri upo out of your control.

Mtegemee MUNGU ishi Katika haki na UPENDO age is just a number
Kumtegemea MUNGU ni haki na wajibu
 
Kuna mahala nikutana na statement

" life begin at forty"

Maana yake ni kwamba watu wengi pale Wanapofika miaka arobain huanza kuishi uhalisia wa maisha yao: kuvaa kulingana na kipato, kutokufwata mkumbo, kuwa na maamuzi, kutokufake life, kutokuishi kwa ajili ya kuridhisha wengine.
 
Back
Top Bottom