Mambo muhimu ya kufanya pindi tu unapopokea taarifa za msiba wa mzazi wako au ndugu yako wa karibu

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,865
12,297
Habari zenu wana JF wenzangu

Bila kupoteza muda ndugu zangu inajulikana wazi kuwa kila binadamu yupo hapa duniani kwa siku zake maalum za kuishi, na baada ya siku hizo kuisha atakufa na kurudi kule alipotokea.

Sasa basi.. ingawa kifo kipo lakini hakuna anaependa kufa au kufiwa. Hii ni kwa sababu kwanza ukishakufa haurudi kuwa hai, pili hakuna anaejua kwa macho yake mwenyewe kwamba baada ya kufa anakwenda wapi, tatu dini zimekuwa zikitueleza kuhusu adhabu iliyopo mbele yetu baada ya vifo vyetu kutokana na matendo yetu.

Kwa vile hakuna binadamu aliekamilika, kwahiyo kila mmoja wetu anajiona ana makosa mbele ya Mungu, hivyo kuogopa kufa mapema na kwenda kukutana na adhabu zake.

Halikadhalika pia hakuna anaependa kufiwa. Hii ni kwa sababu mfiwa anajua kwamba huyo baba yake, mama yake, mtoto wake au ndugu yake aliefariki hatopata tena chance ya kuonana nae katika maisha ya duniani. Yani ndio unakuwa mwisho wao kuongea pamoja, kucheka pamoja, kuishi pamoja, kusaidiana, kupendana, kuonana nk.
Hivyo basi mfiwa huumia kwa namna ambavyo alimpenda au kuwa na ukaribu na marehemu.

Maumivu ya kufiwa, au kufa kwa yule anaekiona kifo chake huwa ni makubwa sana. Mfano mama anapoona kwamba ugonjwa alionao hauwezi kupona, na pengine anakaribia kufa huku akiwaacha watoto wake wakiwa bado wadogo mno wenye kumuhitaji na kuhitaji malezi yake, ni lazima ataumia sana tena sana ila hatokuwa na la kufanya zaidi ya kuomba dua Mungu amsaidie kumlelea watoto wake kupitia mtu fulani, (labda bibi, mamdogo, shangazi nk) pindi tu atapochukua roho yake.

Mimi nimesha experience kufiwa na mzazi ambae tulimpenda sana, na yeye alitupenda mno watoto wake. So i know how it feel kuondokewa ghafla au hata kwa maradhi na mzazi au ndugu, lakini kuna njia ambayo ukiitumia kipindi cha msiba huo mzito itakusaidia kwa kiwango fulani kupunguza maumivu utayopata wewe mfiwa.

Je unatakiwa ufanyaje baada ya kushuhudia kwa macho yako kifo cha baba yako, mama yako, au ndugu yako, au pengine kuletewa habari za kifo chake.

1) Jambo la kwanza kama ni Mkristo unatakiwa hapo hapo useme ama kwa hakika bwana wewe ndio ametoa na wewe ndio umetwaa, jina lako lenye nguvu kuliko majina yote lihimidiwe daima milele AMEN

Kama ni Muislamu unatakiwa kusema Inna lillah Wainna Illayhi rajiun (Hakika sisi wote ni wa kwako Mola wetu mtukufu, na kwako wewe Mola wetu mtukufu sisi sote tutarejea)

Kwa wale wasiofatilia kauli hizi za dini unaweza kusema sisi tulimpenda, lakini wewe Mungu ndio umempenda zaidi.

Hii itakupa faraja kubwa mfiwa kwani itambidi ukubaliane na ukweli kwamba Mungu mwenyewe ameamua kuchukua kilicho chake, kwahiyo huna budi kukubaliana na hali hiyo hata kama hukutarajia au kupendezewa nacho.

2) Jambo la pili unatakiwa umuombe Mungu kwa imani yako akuongoze katika kipindi hiki kigumu kwako, lakini pia akupe subira na ustahamilifu, na pia kukuepusha na kufuru. Hii ni kwa sababu kuna baadhi ya watu wakifiwa na watu wao wa karibu huluzi fasta control na kupelekea wengine kukufuru Mungu kwamba "kwanini umemchukua mama yangu tu na sio mama wa kina Nusrat, Jessica, Abdallah, John nk" sijui "nimekukosea nini Mungu hadi kunipa msiba huu mzito ambao unajua kabisa siwezi kuubeba", "Eeh Mungu wangu kwanini umemchukua mwanangu mkubwa ambae ndio alikuwa tegemeo langu, je maisha yangu yatakuaje baada ya kumchukua mwanangu huyu mwenye msaada mkubwa kwangu nk. Yani inafika kipindi mtu anasahau kwamba kila kiumbe hapa duniani ni cha Mungu, kwahiyo hakuna mwenye uwezo au ruhusa ya kumzuia kukichukua, iwe leo, kesho au siku yoyote aitakayo yeye muumbaji.
Kumbuka Mungu huwa hakosei na wala haonei. Kila analofanya limekamilika tangu enzi na enzi.

3) Jambo la tatu ni kumuomba Mungu akupe muongozo wa maisha yako mapya ambayo utaishi bila kuwa karibu na yule alieondoka.

4) Jambo la nne tumia muda mwingi kumuombea marehemu ili apate makazi mema au Mungu aipokee roho yake na kuiweka katika roho za walio wema.

Kifupi ya kwangu ni hayo tu, ila kama kuna mungine anayo ya zaidi ya haya basi ruhusa kuyaorodhesha hapo chini kwenye comments.

Hii ni kwa wale tunaoamini uwepo wa Mungu, bila kujali dini ya mtu. Ila wasioamini uwepo wa Mungu naomba wasome tu lakini wasiandike chochote kuharibu uzi huu.

Karibuni ndugu zangu.
 
chadema wanakazi ya kulaumu hadi marehemu
Kila mtu aandike historia ya kusomwa baada ya kufa.
Ukifanya uhuni/usela mavi wacha watu waseme ukweli kuhusu mhusika halikadhalika mtu akifanya mema naye ni vyema watu wakasema kuhusu wema wake.
Ni tabia mbaya sana kusifia marehemu hata kama alifanya mabaya,kupambwa kwa sifa nzuri na za kuvutiwa kwa kigezo kuwa marehemu hasemwi kwa ubaya.
 
Kabla sijawahi kufikwa na msiba wowote mkubwa kwangu nilikuwa nachukulia jambo la kufiwa ni simple sana hadi nikawa najiuliza eti mwanaume mzima unaliaje msibani.

Picha la kutisha likaja kunitokea mimi mwenyewe tarehe 30/08/2012 saa 11 alfajiri mama yangu akatwaliwa na Bwana, ninachokumbuka hadi mara ya mwisho ilikuwa ni kupokea simu iliyonipa taarifa hiyo, baada ya hapo nilijikuta naanza kusikia kwa mbaaaaaaali watu wanasema "eh afadhali amezinduka tungewapoteza wawili"......NILIZIMIA KWA ZAIDI YA MASAA MANNE.

Tangu hapo hadi sasa ni miaka 11 imepita lakini haiwezi kupita wiki moja sijamuota, huo ni msiba ulioteteresha sana akili yangu.

NB; SIYAPINGI MAWAZO YAKO LAKINI NIKUJULISHE TU KWAMBA HAKUNA MSIBA MWEPESI.
 
Juzi napokea taarifa dada yangu amepata ajali amepoteza fahamu wamempeleka hospitali yawezekana hata amepoteza uhai!!!!!!! Nikakata simu nikwamuomba MUNGU nikamwambia MUNGU kama YESU KRISTO alikufa msalabani na akafufuka akaushinda umauti na huyu dada anyanyuke hata sasa AMENI.

Nikampigia simu shemeji ananiambia nipo nae namrudisha nyumbani jion nampigia dada anasema ameanza na mazoezi.

Nimeamini Ukiomba kwa imani lolote linakuwa.
 
We umeongelea mambo ya kiroho. Yapo ya kimwili au kidunia. Ukifiwa usipipoteze mwelekeo.
Kwanza funga milango watu wakusanyike nje au kibarazani.

Pili usilielie, angalia nyendo za ndugu zako maana wengine wanatumika kipindi cha msiba kufanya hujuma kwenye familia.

Tatu kama eneo lako kuna utaratibu wa kuendesha misiba na jumuia, ukoo, vyama vya kuzikana n.k waachie wafanye majukumu yao.

Nne hakikisha wasichana na aki na mama wa ndani wanakuwa sehemu moja usiku na mchana ili wasifanye uchafu kipindi cha msiba.
 
Ushauri mzuri ktk kipindi kigumu, ila sijui kwenye item 4 kutumia muda mwingi kumuombea marehemu alazwe pema una tumia reference ya imani ipi? Nasema hivi kwakuwa baadhi ya imani say wakristo, wewe mwenyewe ukiwa hai kwa matendo yako ndio utakua unajiamulia uende wapi Bwana akikutwaa!

Naamanisha ibada tunayofanyia wafu ni utaratibu na utu kufanya hivyo otherwise haibadili hatma yako ie. Chapter yako inakua closed kwa namna ulivyoishi.

Yote kwa yote, umefanya vizuri kushauri namna ya kujipanga msiba unapotokea ukizingatia KIFO HAKIZOELEKI!
 
Kila mtu aandike historia ya kusomwa baada ya kufa.
Ukifanya uhuni/usela mavi wacha watu waseme ukweli kuhusu mhusika halikadhalika mtu akifanya mema naye ni vyema watu wakasema kuhusu wema wake.
Ni tabia mbaya sana kusifia marehemu hata kama alifanya mabaya,kupambwa kwa sifa nzuri na za kuvutiwa kwa kigezo kuwa marehemu hasemwi kwa ubaya.
Hahaha haya mkuu nafikiri uliem quote atakuwa kakuelewa.
 
Nimesoma taratibu ili nione mahali ambapo unashauri muda wote mtu ajiandae kifedha sijaona, ama kwa kuhifadhi au kupitia insurance
 
Kabla sijawahi kufikwa na msiba wowote mkubwa kwangu nilikuwa nachukulia jambo la kufiwa ni simple sana hadi nikawa najiuliza eti mwanaume mzima unaliaje msibani.

Picha la kutisha likaja kunitokea mimi mwenyewe tarehe 30/08/2012 saa 11 alfajiri mama yangu akatwaliwa na Bwana, ninachokumbuka hadi mara ya mwisho ilikuwa ni kupokea simu iliyonipa taarifa hiyo, baada ya hapo nilijikuta naanza kusikia kwa mbaaaaaaali watu wanasema "eh afadhali amezinduka tungewapoteza wawili"......NILIZIMIA KWA ZAIDI YA MASAA MANNE.

Tangu hapo hadi sasa ni miaka 11 imepita lakini haiwezi kupita wiki moja sijamuota, huo ni msiba ulioteteresha sana akili yangu.

NB; SIYAPINGI MAWAZO YAKO LAKINI NIKUJULISHE TU KWAMBA HAKUNA MSIBA MWEPESI.
Dah pole sana mkuu, hayo hata mimi yalinifika tena mwaka jana, mida hiyo hiyo ya saa 11 alfajiri ya ijumaa fulan nilipopokea sim nikiwa nje ya nchi.

Hakika taarifa ile ni moja kati ya taarifa ambayo sitakuja kuisahau katika maisha yangu. Mimi baada ya kupokea taarifa nilikaa kama dakika 5 nisielewe wala kufahamu kile nilichosikia kutoka kwa mtu alienipigia sim.
Baada ya dakika 5 ndo ile sauti ikanirudia tena ikisema kwamba nimeondokewa na mzazi wangu, nikaanza kufanya hayo niliyoyaorodhesha hapo juu kwa kufuata process zote 4. Kisha ndio nikakaa chini na kuanza kutoa chozi, huku mama watoto akiuliza kilichonisibu. Nilipomwambia na yeye akaanza kuangua kilio kikubwa kilichosababisha na mimi sasa nishindwe kustahamili na kuanza kusaidizana kulia, hadi na watoto pia walitusaidia kulia.
Ila baada ya muda nikakubaliana na hali halisi kwamba sisi wote ni wa Mungu na kwake yeye tutarejea tu. Kuna rafiki angu ambae ni kama dada yangu yupo humu mtandaoni sipendi kumtaja, alikuwa mmoja wa watu walionifariji sana katika msiba huo, japo kwa kipindi hicho tulikuwa tuko katika nchi mbali mbali ila alinifariji kupitia whatspp message na calls.
Imagine unapokea msiba wa mzazi ukiwa nje ya nchi, na hamkuonana nae kwa takriban miaka 3 au 4 iliyopita, huo uchungu wake nafikiri unauona.

Kuhusu wewe ndugu yangu, kwa vile msiba ulishatokea muda mrefu uliopita, basi nafikiri ushauri namba 2, 3 hadi 4 unakufaa sana. Jaribu kuyafanyia kazi hayo matatu. Nina imani utaona mabadiliko katika fikra na hisia zako.
 
Leo nimemkumbuka baba yangu hadi chozi kukaribia kunitoka alafu nakutana na mada kama hii.

Uchungu wa kufiwa unatofautiana ndugu, na mbinu za kumfariji mfiwa pia haziwezi kuwa sawa
 
Nimesoma taratibu ili nione mahali ambapo unashauri muda wote mtu ajiandae kifedha sijaona, ama kwa kuhifadhi au kupitia insurance
Mkuu ndomaana nikasema kama kuna mtu mungine ambae atakuwa na ya kuongezea mengine basi aandike hapa chini kwenye comment.
 
Back
Top Bottom