Haya ni mambo muhimu kuyaelewa pindi unapopata ugonjwa sugu

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Jan 9, 2022
449
1,009
Habari JF, nimeandika kuandika haya ili kuzuia madhara yatokanayo na ufuatiliaji duni wa magonjwa sugu.

Kitu cha kwanza kabisa ukipatikana na ugonjwa sugu wowote iwe Sukari ,Presha ,HIV-UKIMWI , Lupus ,Seli Mundu - sickle cell disease , Rheumatoid ...etc lazima uielewe shida ulionayo na uikubali , kisha uelewe yafuatayo :-

1. Pepo au jini halionekani kwenye vipimo ,umepima kipimo kiplimesoma ni Postive au kuna shida basi jua kuna shida na uikubali achana na mawazo na maneno kama ..
------ Watumishi wa dini na Waganga kukwambia majirani ,ndugu , kazini au rafiki hawakupendi wamekutupia ugonjwa .

-------unatafutwa na mizimu au nguvu za mauti ..nk

HIV imesoma positive ni positive hakuna pepo hapo la kutolewa au kuombewa , hakuna wa kukupa Sukari au Presha etc

2. Bado hakuna tiba mbadala zilionekana kutibu hayo magonjwa Sugu kama Sukari ,UKIMWI, Presha na mengine hivyo usiache dawa na kupaka Mafuta ,kunywa maji ya uzima au dawa ambazo hujapewa na wataalamu hospitali, Zaidi labda uende navyo vyote sababu hizo dawa mbadala nyingi zake ni virutubisho.

3. Fuata ushauri wa wataalamu wa afya maana kadri unavyokaa na shida bila matibabu unajiweka kwenye hatari ya kupata shida zaidi. Natambua kuna vitu bado science haina maelezo ya kina au mtoa huduma uliyekutana nae hana maelezo ya kutosha ila kufuata ushauri wa wataalamu wa Afya kabla ugonjwa haujazidi zaidi ni Muhimu.

MUHIMU: Ukipata Sukari au Presha uwezekano mkubwa ni utatumia dawa maisha yako yote na utaishi Muda mrefu sababu viungo vya mwili Sukari au hiyo presha ikiwa kawaida havipati shida.

:Usipofuata Matibabu na kutumia dawa ndani muda mfupi viungo vingine kama figo na moyo vitafeli utakufa mapema lakini pia Presha na sukari vitakuweka kwenye hatari ya kupata stroke - utapooza au kufa ghafla.

Ni hayo tu katika ishu ya magonjwa Sugu sina nia ya kupunguza waumini au wateja wa watu huo ni ukweli.​
 
Serikali ilipaswa kuwapiga marufuku waganga wa kienyeji, waombezi nk wanaowapotosha watu na kuwaweka maisha yao hatarini. Fika ocean road kusikia testimonies za wagonjwa walivyocheleweshwa kwa waombezi.

Kwenye haya PK ni mfano wa kuigwa. Ha-lei upuuzi puuzi.

Kwetu sasa stajaabu ya akina jiwe na corona, mwampsa na mafuta ya uzima, askofu Rashidi mfufua wafu, Dakta Mwaka na wenzao waliopewa baraka za kujifanyia watakayo (wakijipatia vipato) na watawala.

Kwamba nyungu ilipigishwa Muhimbili hadi Mloganzila na bado kina Yaffo ni mawaziri na serikali inakenua? Nini tofauti tetu na manyani?
 
Serikali imeruhusu wataalamu wa tiba mbadala na Dini hivyo watu wapewe elimu kisha wachuje wenyewe
 
Serikali haikupaswa kuwaendekeza hawa watu. PK ni mfano bora sana katika hili.

Nakazia fika ocean road, bugando, kcmc, nk kusikia shuhuda:

"Wagonjwa wakiwamo wa saratani wamecheleweshwa mno huku wakiporwa pesa zao na matapeli hao kwa kivuli cha leseni za serikali."

Kumbe wajibu au manufaa ya serikali ni nini?

Muda utafika hatutaacha kuwawajibisha watu. Habari hii iwafikie kina Yaffo, Mwaka na wenzao.
 
Hatari sana hii
 
Habari JF, nimeandika kuandika haya ili kuzuia madhara yatokanayo na ufuatiliaji duni wa magonjwa sugu.

Kitu cha kwanza kabisa ukipatikana na ugonjwa sugu wowote iwe Sukari ,Presha ,HIV-UKIMWI , Lupus ,Seli Mundu - sickle cell disease , Rheumatoid ...etc lazima uielewe shida ulionayo na uikubali , kisha uelewe yafuatayo :-

1. Pepo au jini halionekani kwenye vipimo ,umepima kipimo kiplimesoma ni Postive au kuna shida basi jua kuna shida na uikubali achana na mawazo na maneno kama ..
------ Watumishi wa dini na Waganga kukwambia majirani ,ndugu , kazini au rafiki hawakupendi wamekutupia ugonjwa .

-------unatafutwa na mizimu au nguvu za mauti ..nk

HIV imesoma positive ni positive hakuna pepo hapo la kutolewa au kuombewa , hakuna wa kukupa Sukari au Presha etc

2. Bado hakuna tiba mbadala zilionekana kutibu hayo magonjwa Sugu kama Sukari ,UKIMWI, Presha na mengine hivyo usiache dawa na kupaka Mafuta ,kunywa maji ya uzima au dawa ambazo hujapewa na wataalamu hospitali, Zaidi labda uende navyo vyote sababu hizo dawa mbadala nyingi zake ni virutubisho.

3. Fuata ushauri wa wataalamu wa afya maana kadri unavyokaa na shida bila matibabu unajiweka kwenye hatari ya kupata shida zaidi. Natambua kuna vitu bado science haina maelezo ya kina au mtoa huduma uliyekutana nae hana maelezo ya kutosha ila kufuata ushauri wa wataalamu wa Afya kabla ugonjwa haujazidi zaidi ni Muhimu.

MUHIMU: Ukipata Sukari au Presha uwezekano mkubwa ni utatumia dawa maisha yako yote na utaishi Muda mrefu sababu viungo vya mwili Sukari au hiyo presha ikiwa kawaida havipati shida.

:Usipofuata Matibabu na kutumia dawa ndani muda mfupi viungo vingine kama figo na moyo vitafeli utakufa mapema lakini pia Presha na sukari vitakuweka kwenye hatari ya kupata stroke - utapooza au kufa ghafla.

Ni hayo tu katika ishu ya magonjwa Sugu sina nia ya kupunguza waumini au wateja wa watu huo ni ukweli.​
da!! nimemkumkumbuka sama la mapangal"dunia 2napita"
 
Back
Top Bottom