Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Technically speaking,but it's the president who did that,I've no doubt about it.

but guess what? hata yeye hatosema "mimi nimefanya hivi" kwa sababu hapendi kubeba lawama moja kwa moja. So tamko lolote (kwa sababu Kikatiba uamuzi wowote lazima utangazwe) utasema ni Halmashauri Kuu ya Taifa. This is not only technically right but also constitutionally justifiable.
 
Mie naona CCM kama vile wanacheza mdako, unarusha jiwe juu, wakati jiwe likiwa hewani unatoa baadhi ya mawe mengine huku yakiwa yamehesabiwa.......kisha unarudisha pale mawe yalipokuwa.

Kwa maana hiyo sioni kama CCM inaweza kufanya lolote zito kujivua gamba. Mwenyekiti wa chama ni mmoja wa wale wanaotakiwa kuondolewa katika kujivua gamba, lakini ni yeye ndiye anayeendesha hilo zoezi la kujivua gamba. Tusubiri kama na yeye atajiondoa katika kujivua gamba.
 
Katiba ya Chama cha Mapinduzi inasema wazi kuwa majukumu ya kuleta nidhamu yako kwa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC)katika ngazi mbalimbali za uongozi kitaifa. Katiba hiyo inasema hivi (Ibara ya 107 inayoshughulikia na Kazi za Halmashauri Kuu ya Taifa):


Kwa hiyo kwa vifungu hivyo viwili tu tunaweza kuona kuwa NEC inaweza kufanya mambo mbalimbali ikiwemo "kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake uifanywa na NEC".

Ibara ya 109 inaweka mojawapo ya mjukumu ya Kamati Kuu ya Taifa ni:



Halafu inabidi tuangalie kuwa Sekretariati ya CCM wajumbe wake wote wanaingia kutoka na nyadhifa zao. Hii ina maana hakuna ambaye anaingia kwa kuteuliwa na Mwenyekiti. Mwenyekiti wa CCM Taifa hana madaraka ya kumuondoa au kumsimamisha kiongozi yeyote wa CCM. Hata kama Mwenyekiti huyo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ina maana gani?

Ina maana ya kwamba lolote lililofanyika Dodoma litakuwa ni tendo la Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya Taifa. Tukumbuke kuwa Mwenyekiti ana kura ya turufu pale tu endapo kura za wajumbe zinalingana katika vikao visivyo husiana na vya uchaguzi - kwani huko ana kura moja.

Ina maana:

a. JK hakuvunja Sekretariati ya Halmashauri Kuu kwani hana madaraka hayo
b. JK hakuvunja Kamati Kuu kwani hana madaraka hayo
c. JK hakumuondoa mtu yeyote uongozi

Hii ina maana kuwa lolote lililotokea Dodoma limetokana na NEC au CC; na hii ina maana ya kwamba wale watu waliokuwa wanaonekana ni vigogo kweli na wana influence ndani ya Chama inawezekana hawana influence ambayo walidhania wanayo. The only x-factor katika hili lote ni kuwa Mwenyekiti wa CCM ndiye Rais vile vile na Katiba ya CCM haitoi maelekezo ya M/Kiti atumie madaraka yake vipi endapo ndiye Rais? Hivyo kama hana nguvu fulani kama mwenyekiti anaweza kutumia madaraka ya Urais kutimiza mambo mbalimbali.

Na hicho ndicho ambavyo kitakuwa kimetokea.



Mkuu,

Nafikiri umequote vipengele wrong. Kwanza kabisa tuanze na ibara ya 104 ambayo inasema kuwa kutakuwa na vikao vifuatavyo vya CCM vya Taifa:-
(1) Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa.
(2) Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.
(3) Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.
(4) Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (Zanzibar).
(5) Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
(6) Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.
(7) Kamati ya Wabunge wote wa CCM.
(8) Kamati ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wote wa CCM (Zanzibar).

Kikao kilichoanza jana ni Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa. Nakubali Ibara ya 107(22) inaipa mamlaka Halimashauri kuu ya Taifa kumwachisha au kumfukuza Uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho ulifanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa. Swali linakuja, je Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa ina mamlaka gani ya kuteua viongozi wa chama? Ibara ya 107(12) inasema kuwa Halimashauri Kuu ya Taifa inayo mamlaka ya kuteua Makatibu wa CCM wa Mikoa. Hakuna sehemu nyingine kwenye hiyo ibara inayoonyesha kama Halimashauri ya Taifa inaweza kuteuwa watu wengine zaidi ya makatibu wa Mikoa. Kwa mantiki hiyo Halimashauri Kuu ya Taifa haiwezi kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yoyote kwenye Ibara ya 107(12) isipokuwa Makatibu wa Mikoa ambao ndio imewateua.

Ninafikiri the relevant provsion ni Ibara ya 107(8) ambayo inasema kuwa kazi za Halimashauri kuu ya taifa ni pamoja na Kudumisha uangalizi juu ya vitendo vya Wanachama na Viongozi wa CCM na endapo itadhihirika kwamba tabia na mwenendo wa Mwanachama fulani vinamwondolea sifa za Uanachama au Uongozi itakuwa na uwezo wa kumwachisha au kumfukuza Uanachama au Uongozi alio nao.

Umeghusia Ibara ya 107(21) ya kumsimamisha Mwenyekiti wa CCM au Makamu Mwenyekiti wa CCM iwapo mwenendo na utendaji wao wa kazi vinamwondolea sifa za uongozi. Sijaelewa hiki kipengele kinaingiaje hapa kwani wanaoshukiwa kuachishwa au kusimamishwa uongozi sio Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti.

Nakubaliana na wewe Mwenyekiti wa CCM hana madaraka yoyote ya kumsimamisha kiongozi yoyote uongozi. Pia kwa kuongezea hapo hana mamlaka yoyote ya kuvunja hivyo vyombo vinane nilivyovitaja hapo juu, ikiwemo Sekretarieti ya Halimashauri kuu ya Taifa. Yaani katiba ya CCM inambana sana Mwenyekiti wao katika kutoa maamuzi lakini akiwa rais katiba yetu inampa madaraka luluki. I don't get it! Pia inaonyesha kuwa kama kwenye hivyo vikao kukiwa na rebels wa kutosha mwenyeti anaweza kuondolewa kiulani. Mwenyekiti kama Mwenyekiti ni toothless.

Umeghusia kuwa kwa vile hana mamlaka kama mwenyekiti then anaweza kutumia madaraka ya Urais kutimiza mambo mbalimbali. How? If that is possible then anaweza pia kutumia madaraka yake ya urais kumsimamisha uongozi kiongozi wa chama cha upinzani au kuvunja sekretarieti ya ya chama kingine?

Ibara ya 37(1) ya katiba inasema kuwa mbali na kuzingatia masharti yali yomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote. Bado sioni ni jinsi anaweza kutumia hiki kifungu.

Unless uamuzi umefanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, Kikwete kama mwenyekiti wa CCM hawezi kufanya maamuzi yoyote ya kichama yeye mwenyewe. labda atumie udictator. Is he actually the leader of this revolutionary party? Compare him with Gaddafi - the leader of the revolution.
 
Umeghusia kuwa kwa vile hana kama mwenyekiti then anaweza kutumia madaraka ya Urais kutimiza mambo mbalimbali. How? If that is possible then anaweza pia kutumia madaraka yake ya urais anaweza kumsimamisha uongozi kiongozi wa chama cha upinzani au kuvunja sekretarieti ya ya chama kingine?

pointi yangu hapa ni kuwa kwa vile JK hana madaraka ya kufanya maamuzi magumu ndani ya CCM ametumia madaraka yake ya Urais kutimiza nia za kisiasa. Kujibu swali lako ni kuwa katika mazingira ya kawaida hawezi lakini tunayo sheria inayompa madaraka ya kuuondoa uongozi wa taasisi au chombo chochote kama kwa kufanya hivyo itasaidia katika usalama wa taifa.
 
Sasa nini unafikiri ni suluhisho? Maana hatuwezi kukaa tukisema "hata wapinzani wakipewa nchi bado mambo yatakuwa yaleyale", sentensi kama hizi zinaonyesha kukata tamaa na mwisho wa kufikiri kuwa hatuwezi kutatua matatizo yetu wenyewe, kitu ambacho si kweli.

Ufumbuzi ni MKUTANO wa KATIBA tu...
Jk akichezea fursa hii itakula kwake!
Ni heri wenye HEKIMA 10 wakukosoe kuliko wapumbavu 100 wakushangilie wee BOMBA!
 
pointi yangu hapa ni kuwa kwa vile JK hana madaraka ya kufanya maamuzi magumu ndani ya CCM ametumia madaraka yake ya Urais kutimiza nia za kisiasa. Kujibu swali lako ni kuwa katika mazingira ya kawaida hawezi lakini tunayo sheria inayompa madaraka ya kuuondoa uongozi wa taasisi au chombo chochote kama kwa kufanya hivyo itasaidia katika usalama wa taifa.

Mkuu naomba hicho kifungu nikisome
 
Mkuu, ...
Kikao kilichoanza jana ni Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa. Nakubali Ibara ya 107(22) inaipa mamlaka Halimashauri kuu ya Taifa kumwachisha au kumfukuza Uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho ulifanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa. Swali linakuja, je Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa ina mamlaka gani ya kuteua viongozi wa chama? Ibara ya 107(12) inasema kuwa Halimashauri Kuu ya Taifa inayo mamlaka ya kuteua Makatibu wa CCM wa Mikoa. Hakuna sehemu nyingine kwenye hiyo ibara inayoonyesha kama Halimashauri ya Taifa inaweza kuteuwa watu wengine zaidi ya makatibu wa Mikoa. Kwa mantiki hiyo Halimashauri Kuu ya Taifa haiwezi kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yoyote kwenye Ibara ya 107(12) isipokuwa Makatibu wa Mikoa ambao ndio imewateua.

Nimekupata vizuri sana lakini nadhani umejenga msingi usio sahihi na kwa hivyo umefikia hitimisho lisilosahihi:

Ibara hiyo ya 107(22) inaipa NEC madaraka ya kuweza kumsimamisha na kumwachisha uongozi mtu ambaye ilifanya UTEUZI WA MWISHO siyo tu uteuzi wake. Ukiangalia kipengele cha 13 cha ibara hiyo hasa vipengele vidogo vya d - i utaona kuwa kuna nafasi ZAIDI YA YA Makatibu wa Mikoa ambazo uteuzi wake wa mwisho unafanywa na NEC. Hii ni pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu.
 
Mkuu,

wa CCM (Zanzibar).
Kikao kilichoanza jana ni Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa. Nakubali Ibara ya 107(22) inaipa mamlaka Halimashauri kuu ya Taifa kumwachisha au kumfukuza Uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho ulifanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa. Swali linakuja, je Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa ina mamlaka gani ya kuteua viongozi wa chama? Ibara ya 107(12) inasema kuwa Halimashauri Kuu ya Taifa inayo mamlaka ya kuteua Makatibu wa CCM wa Mikoa. Hakuna sehemu nyingine kwenye hiyo ibara inayoonyesha kama Halimashauri ya Taifa inaweza kuteuwa watu wengine zaidi ya makatibu wa Mikoa. Kwa mantiki hiyo Halimashauri Kuu ya Taifa haiwezi kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yoyote kwenye Ibara ya 107(12) isipokuwa Makatibu wa Mikoa ambao ndio imewateua.

Tafadhali naomba kufahamishwa, kikao kilichoanza ni cha Halmashauri kuu(NEC) au kamati kuu (CC). Na kuvunjwa kwa sekretariati ni kutokana na kikao kipi. Naona taarifa zimenichanganya kidogo kwani hapo awali ilisemekana NEC imeahirishwa hadi leo.
 
Nimekupata vizuri sana lakini nadhani umejenga msingi usio sahihi na kwa hivyo umefikia hitimisho lisilosahihi:

Ibara hiyo ya 107(22) inaipa NEC madaraka ya kuweza kumsimamisha na kumwachisha uongozi mtu ambaye ilifanya UTEUZI WA MWISHO siyo tu uteuzi wake. Ukiangalia kipengele cha 13 cha ibara hiyo hasa vipengele vidogo vya d - i utaona kuwa kuna nafasi ZAIDI YA YA Makatibu wa Mikoa ambazo uteuzi wake wa mwisho unafanywa na NEC. Hii ni pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu.


Mkuu nimekupata lakini kipengele cha 13 cha Ibara ya 107 kina-aaply tuu pale "Unapofika wakati wa Uchaguzi". Sasa sijui kwa nini wakitumie kipengele hicho wakati huu ambapo hakuna uchaguzi.
 
Kamati kuu ya CCM kwawaka moto
WAJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM), wameendelea kuvutana na kusababisha kuahirishwa kwa Mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho kilichokuwa kianze jana. Kikao cha CC ambacho kilianza juzi jioni kilitarajiwa kumalizika usiku wa siku hiyo na jana kilikuwa kifanyike kikao cha NEC, ajenda kuu ikiwa ni kujadili tathmini ya Mchaguzi Mkuu uliopita. Hata hivyo, Kamati Kuu iliyoanza kikao saa 10 jioni juzi, iliahirisha kikao chake saa 1:00 usiku na kurejea tena saa 3:00 hadi saa 5:00 usiku, bila kumaliza kupanga ajenda za NEC.

Wajumbe wa NEC walianza kukusanyika asubuhi jana katika Makao Makuu ya CCM, baadaye walitakiwa kurudi tena saa 7:00 mchana, lakini waliporejea walitakiwa kurudi tena saa 10:00 jioni, pia walitakiwa kurejea leo tena saa 3:00 asubuhi. Kuahirishwa kwa kikao cha NEC, kulidaiwa kuwa kumetokana na CC kutomaliza kuandaa ajenda cha kikao hicho.


Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, zilidai kuwa hatua ya kuahirishwa kwa kikao hicho ilitokana na kuwepo kwa mvutano mkali kati ya wajumbe wa CC. Habari zinasema kundi moja likitaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Kamati Kuu, Rostam Aziz na Mbunge wa Bariadi Magharibi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, Andrew Chenge wajiuzulu kwa kuandika barua za kujiuzulu CC.


Inadaiwa kundi hilo linataka wajumbe hao wa Kamati Kuu kujiuzulu ili kuinusuru CCM kutokana na tuhuma mbalimbali kinazobebeshwa na kuharibu taswira yake. Kundi hilo linadai pia kuwa kama wajumbe hao watatoswa watakuwa wamewanyima Chadema ajenda mbele ya wananchi, lakini kundi jingine linalowaunga mkono likipinga mapendekezo hayo. Hata hivyo, inadaiwa kuwa Makamba, Chenge na Rostam bado walikuwa wakigoma kutekeleza mapendekezo hayo, hali iliyofanya mjadala wa pande hizo kuwa ngumu baada ya kuvutana.


Baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa CCM, wanaunga mkono kundi hilo lilikuwa likikutana kwenye hoteli moja, wakihaha kuhakikisha ajenda hiyo inazimwa. Katika mkutano huo, inadaiwa ajenda nyingine iliyokuwa na mvutano zaidi ni ya Muswada wa Sheria ya Kubadilisha Katiba wa 2011 ambapo katika kikao hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema pia alihudhuria.


Awali, kulikuwa na taarifa za kuvunjwa kwa Sekretarieti ya CCM, hatua ambayo ingesababisha Makamba kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwenye CCM.


Taarifa zilizopatikana jana mchana zilidai kuwa Sekretarieti hiyo ilikuwa tayari kujiuzulu, lakini inadaiwa kwamba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alikuwa akikataa hatua hiyo na kutaka kwenda nayo Sekretarieti hiyo hadi uchaguzi wa chama unaotarajiwa kufanyika mwakani. Sekretarieti hiyo inaundwa na Makamba akiwa mwenyekiti, manaibu makatibu wakuu wa CCM Bara na Visiwani, George Mkuchika na Saleh Ramadhan Feruzi; Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati.


Wengine ni Katibu wa Uchumi na Fedha, Amos Makala, Katibu wa Mipango, Kidawa Saleh na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe. Wanaotajwa kurithi nafasi ya Makamba iwapo atajiuzulu ni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Habari, Ajira, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi.


Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Kanali Abdulrahman Kinana, ambaye anadaiwa anaweza kukinusuru chama hicho na mgawanyiko uliopo, anadaiwa kukataa nafasi hiyo baada ya kuombwa na mwenyekiti. Mwingine anayetajwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira, lakini anahukumiwa na historia yake ya kuhama chama hicho kwenda NCCR-Mageuzi mwaka 1995.


Kikao hicho kinadaiwa pia kujadili matamshi ya kejeli na matusi yaliyotolewa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) dhidi ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kuwa yanakigharimu chama. "Kama kuna kitu kimetugharimu kichama ni kauli za UVCCM, huwezi ukabeza mchango wa Frederick Sumaye. Huyu amelitumikia taifa na chama kwa muda wa mrefu," kilisema chanzo chetu.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, alisema ngoma bado ni nzito na kuwataka wajumbe wa Nec kuwapo kwa ajili ya kikao leo saa 5:00 asubuhi. Hata hivyo, Chiligati alikataa kutaja ajenda zilizokuwa zikijadiliwa kupelekwa NEC na kuahidi kuzitaja kwa waandishi wa habari leo saa 3:00 asubuhi.


Chanzo: Mwananchi
 
Kamati Kuu CCM yawaka moto
Sunday, 10 April 2011 06:39am

Waandishi wetu, Dodoma
Mwananchi

WAJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM), wameendelea kuvutana na kusababisha kuahirishwa kwa Mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho kilichokuwa kianze jana.

Kikao cha CC ambacho kilianza juzi jioni kilitarajiwa kumalizika usiku wa siku hiyo na jana kilikuwa kifanyike kikao cha NEC, ajenda kuu ikiwa ni kujadili tathmini ya Mchaguzi Mkuu uliopita.

Hata hivyo, Kamati Kuu iliyoanza kikao saa 10 jioni juzi, iliahirisha kikao chake saa 1:00 usiku na kurejea tena saa 3:00 hadi saa 5:00 usiku, bila kumaliza kupanga ajenda za NEC.

Wajumbe wa NEC walianza kukusanyika asubuhi jana katika Makao Makuu ya CCM, baadaye walitakiwa kurudi tena saa 7:00 mchana, lakini waliporejea walitakiwa kurudi tena saa 10:00 jioni, pia walitakiwa kurejea leo tena saa 3:00 asubuhi.

Kuahirishwa kwa kikao cha NEC, kulidaiwa kuwa kumetokana na CC kutomaliza kuandaa ajenda cha kikao hicho.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, zilidai kuwa hatua ya kuahirishwa kwa kikao hicho ilitokana na kuwepo kwa mvutano mkali kati ya wajumbe wa CC.

Habari zinasema kundi moja likitaka Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Kamati Kuu, Rostam Aziz na Mbunge wa Bariadi Magharibi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, Andrew Chenge wajiuzulu kwa kuandika barua za kujiuzulu CC.

Inadaiwa kundi hilo linataka wajumbe hao wa Kamati Kuu kujiuzulu ili kuinusuru CCM kutokana na tuhuma mbalimbali kinazobebeshwa na kuharibu taswira yake.

Kundi hilo linadai pia kuwa kama wajumbe hao watatoswa watakuwa wamewanyima Chadema ajenda mbele ya wananchi, lakini kundi jingine linalowaunga mkono likipinga mapendekezo hayo.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa Makamba, Chenge na Rostam bado walikuwa wakigoma kutekeleza mapendekezo hayo, hali iliyofanya mjadala wa pande hizo kuwa ngumu baada ya kuvutana.

Baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa CCM, wanaunga mkono kundi hilo lilikuwa likikutana kwenye hoteli moja, wakihaha kuhakikisha ajenda hiyo inazimwa.

Katika mkutano huo, inadaiwa ajenda nyingine iliyokuwa na mvutano zaidi ni ya Muswada wa Sheria ya Kubadilisha Katiba wa 2011 ambapo katika kikao hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema pia alihudhuria.

Awali, kulikuwa na taarifa za kuvunjwa kwa Sekretarieti ya CCM, hatua ambayo ingesababisha Makamba kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwenye CCM.

Taarifa zilizopatikana jana mchana zilidai kuwa Sekretarieti hiyo ilikuwa tayari kujiuzulu, lakini inadaiwa kwamba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alikuwa akikataa hatua hiyo na kutaka kwenda nayo Sekretarieti hiyo hadi uchaguzi wa chama unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Sekretarieti hiyo inaundwa na Makamba akiwa mwenyekiti, manaibu makatibu wakuu wa CCM Bara na Visiwani, George Mkuchika na Saleh Ramadhan Feruzi; Katibu wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati.

Wengine ni Katibu wa Uchumi na Fedha, Amos Makala, Katibu wa Mipango, Kidawa Saleh na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe.

Wanaotajwa kurithi nafasi ya Makamba iwapo atajiuzulu ni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na Waziri wa Habari, Ajira, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Kanali Abdulrahman Kinana, ambaye anadaiwa anaweza kukinusuru chama hicho na mgawanyiko uliopo, anadaiwa kukataa nafasi hiyo baada ya kuombwa na mwenyekiti.

Mwingine anayetajwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira, lakini anahukumiwa na historia yake ya kuhama chama hicho kwenda NCCR-Mageuzi mwaka 1995.

Kikao hicho kinadaiwa pia kujadili matamshi ya kejeli na matusi yaliyotolewa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) dhidi ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, kuwa yanakigharimu chama.

"Kama kuna kitu kimetugharimu kichama ni kauli za UVCCM, huwezi ukabeza mchango wa Frederick Sumaye. Huyu amelitumikia taifa na chama kwa muda wa mrefu," kilisema chanzo chetu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, alisema ngoma bado ni nzito na kuwataka wajumbe wa Nec kuwapo kwa ajili ya kikao leo saa 5:00 asubuhi.

Hata hivyo, Chiligati alikataa kutaja ajenda zilizokuwa zikijadiliwa kupelekwa NEC na kuahidi kuzitaja kwa waandishi wa habari leo saa 3:00 asubuhi.
 
Kama kubunya keki ya taifa washaibunya sana,makamba hata kama ataondoka au anaondoka ameshajiwekea mazingira ya watu watakaoendelea kumlinda
 
Tafadhali naomba kufahamishwa, kikao kilichoanza ni cha Halmashauri kuu(NEC) au kamati kuu (CC). Na kuvunjwa kwa sekretariati ni kutokana na kikao kipi. Naona taarifa zimenichanganya kidogo kwani hapo awali ilisemekana NEC imeahirishwa hadi leo.


Kweli inachanganya.

Hata mimi nilikuwa nafikiri NEC imekaa jana lakini gazeti la Mwananchi linasema kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM), wameendelea kuvutana na kusababisha kuahirishwa kwa Mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho kilichokuwa kianze jana. Kikao cha CC ambacho kilianza juzi jioni kilitarajiwa kumalizika usiku wa siku hiyo na jana kilikuwa kifanyike kikao cha NEC, ajenda kuu ikiwa ni kujadili tathmini ya Mchaguzi Mkuu uliopita. Hata hivyo, Kamati Kuu iliyoanza kikao saa 10 jioni juzi, iliahirisha kikao chake saa 1:00 usiku na kurejea tena saa 3:00 hadi saa 5:00 usiku, bila kumaliza kupanga ajenda za NEC.

Kwa hiyo hata NEC haijakaa then.
 
Kichwa cha thread kibadilishwe. Mnampa credit bure wakati kikatiba (ya CCM ) inaonekana Kikwete hana uwezo wa kumtimua Katibu Mkuu na kuvunja sekretarieti ya Kamati Kuu.

Bila hata kupitia Katiba ya CCM, unaweza kujiuliza, mtu ambae hajawateua atawaenguaje?
Na kwa sasa haiingii akilini Kikwete kuanza kuwafukuzisha kazi ma Katibu Wakuu wakati huu ambapo kuna tatizo la makundi kwenye chama. Huwezi kumfukuza mtu sasa hivi mule. Na Kikwete huwa hana hulka ya kumtosa rafiki.

Na kweli, vyombo vya habari vinaripoti, Makamba aliomba kujiuzulu. Kikwete kafanya maamuzi mazito, yepi?
 
Muulizeni huyo Slaa ni miswada mingapi yeye akiwa kama mbunge aliitolea shilingi na mingapi aliipigia kura ya ndio?.....It's so easy to know these people if you look at their voting records,something that most fanatics here don't have access to!...angalia watu walioupigia kura muswaada wa madini wa 1998 na walioukataa.

Mazee hilo la voting records za wabunge nishaliongelea, muhimu kweli.

Mwenzetu unapata wapi voting records za wabunge?
 
TBC1 Bulletin imemnukuu Chilligati akiongea na waandishi wa habari akisema:

  1. CC imejiuzulu
  2. Sekretariat kuu ya CCM imejiuzulu
Amedai nia ni kumsaidia mwenyekiti kukijenga chama upya kama ilivyokubalika ajali.

Alipoulizwa kama wanajiuzulu kwa sababu ya pressure ya UV-CCM kuwa CC imeshindwa kumsaidia Rais na mwenyekiti JK, Chilligati alibeza UV-CCM kuwa wanajisemea tu lakini wao hawajalazimishwa na UV-CCM.
 
Wakuu zangu kilitokea nini mwaka 2005, JK alipotangaza secretariet mpya toka ile aloiacha Mkapa? - I mean ni hatua zipi zilifuatwa!
 
Back
Top Bottom