WanaJF,
Ni kweli hali ya watanzania ni mbaya sana kwa sababu ya ugumu wa maisha. Tunaamini hali hiyo imesababishwa na uongozi mbovu wa Serikali ya CCM ambayo kwa miaka zaidi ya mitano dereva wake mkuu ni Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwa muda mrefu sasa tumemlaumu JK kwa kushindwa kuchukua maamuzi magumu ili kuinusuru nchi.
Lakini kwa alichofanya juzi Dodoma ndani ya chama chake, anastahili PONGEZI.
Kama mwanadamu yoyote ni vigumu kumtosa rafiki yako wa karibu kwa sababu yoyote ile. Kama mwanadamu amewatetea maswahiba wake wa karibu kwa sababu anazojua yeye. Lakini juzi tumeona amechukua uamuzi wa kuwatosa maswahiba wake wa karibu RA, EL, Yusufu M, na washirika wa siku nyingi akina mzee wa vijisenti n.k., ili kuinusuru chama chake, bila shaka kwa lengo la kuinusuru nchi yetu kwa ujumla.
Hatuna hakika kama malengo yake yatatimia kuleta matumaini kwa watanzania tuliokata tamaa. Hatuna hakika kama hao waliochukua nafasi za uongozi ndani ya chama chake watakuwa msaada kwake na kwa chama chake. Hatuna hakika kama ana dhamira njema ya kuleta matumaini. Hatuna hakika na mengi kwa sasa..... lakini amefanya ujasiri mkubwa kuwatosa maswahiba wake.
Ni vema tukalaumu pa kuhitaji lawama, na kusifu au kupongeza japo kidogo panapohitaji kufanya hivyo. Kinyume chake tutakuwa wanafiki tukilalama tu.
Hatusemi amemaliza kazi, ndiyo anatakiwa kuanza.... bado anakazi kubwa... bado kama dreva wa chama chake ana nafasi ya kuponya walau baadhi ya majeraha ya watanzania bila kusahau hali ya Arusha... ili ufanyike uchaguzi wa meya kihalali na mengine mengi. Kama ana dhamira njema ya kufanya hivyo anaweza kufanya ndani ya muda mfupi.
Ni maoni yangu tu wanaJF