Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Jamani eeh.. Greath THinkers... Naona mada imekuwa stori za kijiweni.. Kwanini tusijaribu ku-analyse sababu za JK kufanya hivi. Ndio tunafahamu kuwa alisema anatoa 'gamba' lakini je madhumuni hasilia ni nini...? Je nguvu ambayo upinzani umeipata na haswa CDM ndio umemtishia kupatwa na yale ya KANU? au ni mambo yaliyotokea bondeni kwa MADIBA hapo... ANC overthrow of Mbeki by ZUMA... Je Kikwete anarespond to Lowassa's attempts to take control of CCM's decision making bodies so that he could secure his presidential nomination 2015? Ama ni nini? Kwa hakika kesho majina mapya yatakapo pendekezwa ndipo nia na madhumuni yatajulikana.... Swali la kwanza ni je EL atarudi? tunajua kabisa RA ndio basi (at least in hatokuwepo jikoni directily), je wale wanaojiita wapiganaji kina Kilango, Mwakyembe n.k wataingia? je JK atawapoteza viongozi wengine waliochafuka kama Chenge (most likely in my opinion), na Je atataka kuwadhibiti wale ambao wako kambi ya Lowassa (makinda, et al.) na je wale wengine wanao imezea mate 2015 kama Samwel Sitta watatupiliwa choo cha shimo au ? Ingekuwa vizuri jukwaa la GREAT thinkers likawa mstari wa mbele kuchambua mambo haya kwakua yanatabiri hali ya nchi yetu katika siku za usoni itakuaje... tupunguze ushabiki na uchama katika haya... Nimejaribu kuangalia mawazo mbali mbali tuliyochangia humu nimeona yapo mawazo yamsingi lakini pia ushabiki mwingi (mara ccm wafe tuu..atakama wafe sawa vizuri labda, lakini tunaomba uchambuzi tafadhali...jukwaa hili lirudie hali yake ya miaka ya nyuma.) UCHAmbuzi MAKINI tafadhali jamani.

KK

Kuna wengine humu kazi yao kuchungulia kuna users wangapi online na wanapost kwa mbwembwe, na wengine sio great thinkers but great suckers! Hiki kijiwe cha chadema kikiendelea hivi haya ya Dodoma yatatokea CDM hivi karibuni. FUTURE haionekani kwa macho yenye miwani bali macho ya KI-FIKRA.
 
Msipoteze usingizi wenu kusubiri ati habari kutoka Idodomia, mafisadi wataendelea kula tu kwa sababu fisadi papa aliyeiba kura bado yupo ni sawa na kufikiri Ngamia atapita kwenye tundu la sindano. Hawawezi kubadilika hawa kwa sababu wamekwisha kula damu ya walipa kodi.

Dawa yao ni kuwang'oa tu wapende wasipende. Hizi zote ni zuga zuga zao tu. Na ushahidi wa zuga yenyewe waulizeni ile kamati waliyomkabidhi Mzee Rukhsa kuishughulikia imefika wapi?

Mkishituka mtasikia Dowans wamekwishalipwa na mambo yanendelea kama kawaida.
 
Wana CCM naomba mnisaidie, maana naona kuna watu wanaweza kuwa wanashangilia mafisadi kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya Chama na kumbe uvuliwaji huo umefanyika kimakosa.

Kulingana na Katiba ya CCM ni nani au kikao gani chenye maamuzi ya kumvua kiongozi wa CCM uongozi kwenye ngazi ya Kamati Kuu au NEC?

Chenge alikuwa Mjumbe wa CC kwa kigezo kwamba alipata kura nyingi kwenye uchaguzi wa wajumbe wa NEC kupitia vile viti 20 vya Bara. Je, replacement yake itafanyika vipi?

RA aliingia kwenye CC kwa njia ipi? AU ndio wale wateule wachache wa Mwenyekiti?

Kama Kamati Kuu imevunjwa, je ilivunjwa baada ya kuwavua uongozi hao watuhumiwa?

Mantiki ya kuvunja CC iko wapi? Maana wajumbe wengi wanaingia huko kwa Nyadhifa zao mfano, wenyeviti wote wa Jumuiya za Chama, Spika, Makamu Mwenyekiti Bara na Visiwani, Katibu Mkuu, nadhani na manaibu wake wa Bara na Visiwani. Waliobaki wengine akina Mkapa, Mwinyi na wengineo kibao wanaingia kwa kuwa walishawahi kuwa viongozi wa kitaifa wa CCM.

Je, kuvunja CC sasa hivi ina maana kwamba Kikwete ataleta sura mpya ndani ya CC? Atazipataje na ilihali uchaguzi wa CCM ni mwakani?

Hapo sioni kama JK ametatua mgogoro wa CCM, tatizo siyo Lowassa, RA na Chenge, tatizo ni kundi zima lililo nyuma ya hao mafisadi na hao ndio wamekuwa vinara wa kuongoza utetezi dhidi ya mafisadi na hao ndio waliojaa kwenye NEC. Ngoja tusubiri kesho.

Kama NEC ikibariki hayo maamuzi, basi tusubiri vita kuu ndani ya CCM, hakuna atakayepona. Vita vya panzi ni furaha ya kunguru, wapinzani kazeni buti Ikulu inazidi kuwa wazi na hili limetokea kipindi kizuri sana, inawezekana kabisa wabunge wa CCM wanaweza kuungana na wabunge wa upinzani kuupinga mswaada wa Katiba Mpya, maana hawajui kesho watakuwa wapi.

Kikwete aliingia madarakani kwa siasa za makundi akisaidiwa na ufisadi wa EPA ambao ulimpa fedha za kampeni. Ni makundi hayo hayo na ufisadi huo huo ndio ambao utasababisha CCM imfie mikononi mwake.

mwenyekiti wa chama kubadilisha sekretarieti ya chama ni mabadiliko ya kawaida. kwa wenye kumbukumbu nzuri,baada ya kikwete kupata uenyekiti wa ccm,aliunda sekretarieti yake ikiongozwa na katibu makamba. kwamba eti amevunja cc hiyo haiwezekani. hana mamlaka hayo. wajumbe wa cc ukiondoa wanaoingia kwa nyadhifa zao wanachaguliwa na nec!
 
Jamani eeh.. Greath THinkers... Naona mada imekuwa stori za kijiweni.. Kwanini tusijaribu ku-analyse sababu za JK kufanya hivi. Ndio tunafahamu kuwa alisema anatoa 'gamba' lakini je madhumuni hasilia ni nini...? Je nguvu ambayo upinzani umeipata na haswa CDM ndio umemtishia kupatwa na yale ya KANU? au ni mambo yaliyotokea bondeni kwa MADIBA hapo... ANC overthrow of Mbeki by ZUMA... Je Kikwete anarespond to Lowassa's attempts to take control of CCM's decision making bodies so that he could secure his presidential nomination 2015? Ama ni nini? Kwa hakika kesho majina mapya yatakapo pendekezwa ndipo nia na madhumuni yatajulikana.... Swali la kwanza ni je EL atarudi? tunajua kabisa RA ndio basi (at least in hatokuwepo jikoni directily), je wale wanaojiita wapiganaji kina Kilango, Mwakyembe n.k wataingia? je JK atawapoteza viongozi wengine waliochafuka kama Chenge (most likely in my opinion), na Je atataka kuwadhibiti wale ambao wako kambi ya Lowassa (makinda, et al.) na je wale wengine wanao imezea mate 2015 kama Samwel Sitta watatupiliwa choo cha shimo au ? Ingekuwa vizuri jukwaa la GREAT thinkers likawa mstari wa mbele kuchambua mambo haya kwakua yanatabiri hali ya nchi yetu katika siku za usoni itakuaje... tupunguze ushabiki na uchama katika haya... Nimejaribu kuangalia mawazo mbali mbali tuliyochangia humu nimeona yapo mawazo yamsingi lakini pia ushabiki mwingi (mara ccm wafe tuu..atakama wafe sawa vizuri labda, lakini tunaomba uchambuzi tafadhali...jukwaa hili lirudie hali yake ya miaka ya nyuma.) UCHAmbuzi MAKINI tafadhali jamani.

KK

The way I perceive this is, JK amelazimika kufanya hivyo maana vitu kwake vimekuwa vigumu na kweli ameamua kufanya kile anachopaswa kufanya. Tatizo ni kuwa wakati akiwa na dhamira njema kabisa hajui kuwa ameingia kwenye mtego ambao hautamwacha yeye salama hapa ndipo napo mwonea huruma kwamba sincerely amekuwa victim wa circumstances.

Wakati akiwaondoa hao ambao wamechafuka tayari wengine wameshajitengenezea escape route mapema yeye alipochelewa kufanya maamuzi sasa hao pamoja na wale ambao bado angalau wanaweza kusimama mbele ya jamii watamshugulikia yeye bila yeye kuelewa na hatimaye atajikuta mweupe asijue chakufanya.

Kuna mawili yatatokea kama system itabomoka which I doubt basi tutaanza siasa mpya ambapo kila mtu atachukua tahadhari haya yaliyotokea yasitokee tena. Lahasha kama system ndiyo hii hii basi mmoja kati ya vigogo ambao walipakwa matope huko nyuma ataibuka kidedea maana amekuwa mwangalifu sana naamefanya vitu vyake kiakili mno kiasi kwamba walishindwa kumwelewa mapema naye ameweka plan A na B zote ambazo moja ikifanikiwa ndo atajitokeza lakini ikishindikana atamwacha huyo wa B aendelee.

Yangu ni usomaji wa ramani tu na historia za watu na naamini kwa asilimia si chini ya 50% niko sahihi. Ila kinachonifurahisha katika yote haya matokeo yake ni Tz njema kuzaliwa na hili hakuna wakulirudisha nyuma maana mwasisi na mwenye ufunguo hakuna anayeweza kumnyang'anya akifungua hakuna wakufunga na akifunga hakuna wakufungua.
 
Msipoteze usingizi wenu kusubiri ati habari kutoka Idodomia, mafisadi wataendelea kula tu kwa sababu fisadi papa aliyeiba kura bado yupo ni sawa na kufikiri Ngamia atapita kwenye tundu la sindano. Hawawezi kubadilika hawa kwa sababu wamekwisha kula damu ya walipa kodi. Dawa yao ni kuwang'oa tu wapende wasipende. Hizi zote ni zuga zuga zao tu. Na ushahidi wa zuga yenyewe waulizeni ile kamati waliyomkabidhi Mzee Rukhsa kuishughulikia imefika wapi?

Mkishituka mtasikia Dowans wamekwishalipwa na mambo yanendelea kama kawaida.
Wacha, inamaana hujui kuwa kamati ya mzee Mwinyi imeshatoa majibu? Unaweza kujiliza kwanini Mwakyembe na Sitta wamepelekwa serikalini? Kwanini CCM wamebadilisha Spika? Na kwanini leo hii kina RA, Makamba na EL wanang'oka. Ulitegemea jibu la moja kwa moja?

Mengine hufanywa kimyakimya na hasa kikipatikana kisingizio aka matokeo ya uchaguzi
 
Wana CCM naomba mnisaidie, maana naona kuna watu wanaweza kuwa wanashangilia mafisadi kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya Chama na kumbe uvuliwaji huo umefanyika kimakosa.

Kulingana na Katiba ya CCM ni nani au kikao gani chenye maamuzi ya kumvua kiongozi wa CCM uongozi kwenye ngazi ya Kamati Kuu au NEC?

Kaka ajavuliwa mtu uongozio hawa WAMEJIUZULU WENYEWE.
au kwa kiundani wamelazimishwa KUJIUZULU
 
Kuna wengine humu kazi yao kuchungulia kuna users wangapi online na wanapost kwa mbwembwe, na wengine sio great thinkers but great suckers! Hiki kijiwe cha chadema kikiendelea hivi haya ya Dodoma yatatokea CDM hivi karibuni. FUTURE haionekani kwa macho yenye miwani bali macho ya KI-FIKRA.

Acha upuuzi.Hukulazimishwa kujiunga hapa,umejileta mjwenyewe.Sasa kashfa na dharau za nini?Kuna watu na busara zao ambao chama chao cha siasa ni nchi inayoitwa Tanzania.Wazembe wa kufikiri kama wewe hmakawii kuwaita watu wa aina hiyo kuwa ni wana-Chadema.Sio kila anayepinga ufisadi ni mwana-Chadema,just like ambavyo sio kila mwana-CCM ni fisadi.

Unasema future haionekani ilhali bado unakuja hapa JF!?
 
Katiba ya Chama cha Mapinduzi inasema wazi kuwa majukumu ya kuleta nidhamu yako kwa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC)katika ngazi mbalimbali za uongozi kitaifa. Katiba hiyo inasema hivi (Ibara ya 107 inayoshughulikia na Kazi za Halmashauri Kuu ya Taifa):
21. Kumsimamisha Mwenyekiti wa CCM au Makamu Mwenyekiti wa CCM iwapo mwenendo na utendaji wake wa kazi vinamwondolea sifa za uongozi. Hata hivyo Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itafikisha mapendekezo yake mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kwa uamuzi wa mwisho.

22. Kumwachisha au kumfukuza Uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake
wa mwisho ulifanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.

Kwa hiyo kwa vifungu hivyo viwili tu tunaweza kuona kuwa NEC inaweza kufanya mambo mbalimbali ikiwemo "kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake uifanywa na NEC".

Ibara ya 109 inaweka mojawapo ya mjukumu ya Kamati Kuu ya Taifa ni:

Kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote isipokuwa Mwenyekiti wa CCM na
Makamu wa Mwenyekiti wa CCM endapo itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za uongozi.

Halafu inabidi tuangalie kuwa Sekretariati ya CCM wajumbe wake wote wanaingia kutoka na nyadhifa zao. Hii ina maana hakuna ambaye anaingia kwa kuteuliwa na Mwenyekiti. Mwenyekiti wa CCM Taifa hana madaraka ya kumuondoa au kumsimamisha kiongozi yeyote wa CCM. Hata kama Mwenyekiti huyo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ina maana gani?

Ina maana ya kwamba lolote lililofanyika Dodoma litakuwa ni tendo la Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya Taifa. Tukumbuke kuwa Mwenyekiti ana kura ya turufu pale tu endapo kura za wajumbe zinalingana katika vikao visivyo husiana na vya uchaguzi - kwani huko ana kura moja.

Ina maana:

a. JK hakuvunja Sekretariati ya Halmashauri Kuu kwani hana madaraka hayo
b. JK hakuvunja Kamati Kuu kwani hana madaraka hayo
c. JK hakumuondoa mtu yeyote uongozi

Hii ina maana kuwa lolote lililotokea Dodoma limetokana na NEC au CC; na hii ina maana ya kwamba wale watu waliokuwa wanaonekana ni vigogo kweli na wana influence ndani ya Chama inawezekana hawana influence ambayo walidhania wanayo. The only x-factor katika hili lote ni kuwa Mwenyekiti wa CCM ndiye Rais vile vile na Katiba ya CCM haitoi maelekezo ya M/Kiti atumie madaraka yake vipi endapo ndiye Rais? Hivyo kama hana nguvu fulani kama mwenyekiti anaweza kutumia madaraka ya Urais kutimiza mambo mbalimbali.

Na hicho ndicho ambavyo kitakuwa kimetokea.
 
tatizo la ccm siyo lowasa,ra na mafisadi wengine waliojaa huko. tatizo ni mfumo ambao umekigeuza hicho chama kuwa chama dola! bila kupambana na huo mfumo ccm haiwezi safishika. na wala haitafishika ikiwa madarakani. tutakapowaondoa hawa watu madarakani ndipo watapata muda wa kujisafisha.maana wengi wa viongozi wao ambao wako huko ili kupata pesa na madaraka watawakimbia pindi chama kitakapoondolewa madarakani.kwamba eti mwenyekiti wao anaweza fanya mageuzi ya maana hizo ni ndoto za mchana.

Siku ya kufa nyani miti yote huteleza.
Kama wadau wengi walivyochangia hapa tatizo si hao watatu RA, EL na Chenge, bali mfumo uliowaingiza hadi kujiona wako ndani ya peace of heaven. Wakati umelishwa na kukua halafu huyo yaya unamtema wakati ameshajua siri na madhaifu yako, siku atakapoyaibua utaomba inchi ifunuke ikufiche.

Kwa tafsiri rahisi Mwenyekiti hajatumia busara kwa muda mrefu na sasa ni zima moto tu na kwa aliyofanya ni dhahiri ameongeza crack ndani ya chama kuwa makundi mawili ingawa hayaonikani kimfumo bali kinadharia.

Huu utaratibu wa rais na mwenyekiti kutaka wenye madaraka wafanye kama robot si rahisi maana hata robotical incording system inahitaji programmer specialist. Wasifu wa Rais Kikwete ni kukaa ikulu kila kitu kitajiendesha chenyewe kwa kuwa tumeweka watu, yeye mguu majuu kukagua mahoteli bora duniani.
Kazi kwelikweli.
 
Nahisi hapo amepokea ushauri toka kwa wakulu wenzake na namna ya kutumia madaraka yake bila kufikiria kuwa madaraka ni kitu kimoja na nguvu ya ushawishi ni kitu kingine; makundi yaliyopo yenye nguvu ni hilo la wakulu na la watendaji wao wakuu katika serikali zao huku la watendaji wakuu likiwa na ushawishi na la wakulu likiwa na authority hapo ndipo unabii wa Nyerere waweza kutimia. Ila Kundi moja hapo ni janja kweli maana linaungana na magwiji wa kuwachapa viboko mafisadi ambao wamefungamanishwa na wananchi. Na hili lingine linajihami kwa nguvu zote maana wao ndiyo wahanga wakuu wa ufisadi na wanajua kama hilo la wenzao litafanikiwa basi pepo yao imefika mwisho hapo ngoma inogile.
 
Katiba ya Chama cha Mapinduzi inasema wazi kuwa majukumu ya kuleta nidhamu yako kwa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC)katika ngazi mbalimbali za uongozi kitaifa. Katiba hiyo inasema hivi (Ibara ya 107 inayoshughulikia na Kazi za Halmashauri Kuu ya Taifa):

Kwa hiyo kwa vifungu hivyo viwili tu tunaweza kuona kuwa NEC inaweza kufanya mambo mbalimbali ikiwemo "kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake uifanywa na NEC".

Ibara ya 109 inaweka mojawapo ya mjukumu ya Kamati Kuu ya Taifa ni:

Halafu inabidi tuangalie kuwa Sekretariati ya CCM wajumbe wake wote wanaingia kutoka na nyadhifa zao. Hii ina maana hakuna ambaye anaingia kwa kuteuliwa na Mwenyekiti. Mwenyekiti wa CCM Taifa hana madaraka ya kumuondoa au kumsimamisha kiongozi yeyote wa CCM. Hata kama Mwenyekiti huyo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii ina maana gani?

Ina maana ya kwamba lolote lililofanyika Dodoma litakuwa ni tendo la Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya Taifa. Tukumbuke kuwa Mwenyekiti ana kura ya turufu pale tu endapo kura za wajumbe zinalingana katika vikao visivyo husiana na vya uchaguzi - kwani huko ana kura moja.

Ina maana:

a. JK hakuvunja Sekretariati ya Halmashauri Kuu kwani hana madaraka hayo
b. JK hakuvunja Kamati Kuu kwani hana madaraka hayo
c. JK hakumuondoa mtu yeyote uongozi

Hii ina maana kuwa lolote lililotokea Dodoma limetokana na NEC au CC; na hii ina maana ya kwamba wale watu waliokuwa wanaonekana ni vigogo kweli na wana influence ndani ya Chama inawezekana hawana influence ambayo walidhania wanayo. The only x-factor katika hili lote ni kuwa Mwenyekiti wa CCM ndiye Rais vile vile na Katiba ya CCM haitoi maelekezo ya M/Kiti atumie madaraka yake vipi endapo ndiye Rais? Hivyo kama hana nguvu fulani kama mwenyekiti anaweza kutumia madaraka ya Urais kutimiza mambo mbalimbali.

Na hicho ndicho ambavyo kitakuwa kimetokea.
Technically speaking,but it's the president who did that,I've no doubt about it.
 
Kuna wengine humu kazi yao kuchungulia kuna users wangapi online na wanapost kwa mbwembwe, na wengine sio great thinkers but great suckers! Hiki kijiwe cha chadema kikiendelea hivi haya ya Dodoma yatatokea CDM hivi karibuni. FUTURE haionekani kwa macho yenye miwani bali macho ya KI-FIKRA.
Hasira za mkizi.
 
Back
Top Bottom