Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,314
- 33,808
Kweli inachanganya. hata mimi nilikuwa nafikiri NEC imekaa jana lakini gazeti la Mwananchi linasema kuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM), wameendelea kuvutana na kusababisha kuahirishwa kwa Mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho kilichokuwa kianze jana. Kikao cha CC ambacho kilianza juzi jioni kilitarajiwa kumalizika usiku wa siku hiyo na jana kilikuwa kifanyike kikao cha NEC, ajenda kuu ikiwa ni kujadili tathmini ya Mchaguzi Mkuu uliopita. Hata hivyo, Kamati Kuu iliyoanza kikao saa 10 jioni juzi, iliahirisha kikao chake saa 1:00 usiku na kurejea tena saa 3:00 hadi saa 5:00 usiku, bila kumaliza kupanga ajenda za NEC. Kwa hiyo hata NEC haijakaa then.
Ahsante EMT.
Kwa mantiki ni kuwa sekretariati imevunjwa wakati CC ikiandaa agenda za kikao cha NEC kwa taratibu za CCM.
CC wanaingia wajumbe wa kuchaguliwa na wale wanaoingia kwa heshima zao kama marais wastaafu.
NEC wanaingia wajumbe wa kuchaguliwa na wale wa heshima kama mawaziri wakuu wastaafu.
Kikao cha NEC cha Butima kiligubikwa mjadala mkali sana wa ufisadi. Kabla ya kikao, wenyeviti wa CCM wa mikoa chini ya mwenyeji wa mkutano Makongoro Nyerere waliazimia wale wanaokichafua chama wafukuzwe. Hoja yao iliungwa mkono na wazee wastaafu wakiwamo mawaziri wakuu na wanafunzi wa kweli wa Mwalimu Nyerere. Hoja ilizimwa kibabe na mwenyekiti ili kuokoa wanamtandao waliomsaidia kufika hapo.
Uchaguzi uliopita pamoja na viongozi kuficha ukweli kwa maneno ya kejeli umewatisha sana CCM. Kuingiliwa ngome za Dar, Mbeya na Mwanza haikuwa dalili nzuri. Hii imelazimisha baadhi yao wakubali ukweli kuwa ufisadi na kashfa kama za Richmond na Dowans vimechangia sana, na kibaya zaidi wahusika ni viongozi ndani ya chama na kuharibu taswira nzima ya chama.
Wajumbe wengi wa NEC wamedhamiria kukinusuru chama wakiungwa mkono kichini chini na wastaafu maarufu. Nguvu ya kundi la mafisadi ndani ya NEC imepungua.
Uwezekano wa NEC kujadili hoja za kushindwa kwa chama unaweza kuleta mpasuko na uwezekano wa watuhumiwa kupoteza nyadhifa zao kichama au kufukuzwa. Ili kupunguza jazba,mwenyekiti amevunja sekretariati inayolaumiwa kwa utendaji mbovu kama njia ya kuua agenda hiyo kwa vile suala limeshughulikiwa (pre-emptive strategy). Hii itawaokoa watuhumiwa kutojadiliwa mbele ya NEC kwa kina kuzuia jaribio kama la Butiama kuweza kujirudia kwa nguvu zaidi.
Kuwafukuza uanachama kundi lenye nguvu kifedha ni jambo lisilowezekana ikizingatiwa kuwa limeshajipanga vema ndani ya CC, NEC na bunge. Jambo linalofanyika hapa ni 'funika kombe mwanaharamu apite'. Ni mbinu ya hali ya juu sana kuwanusuru watuhumiwa kwa kupunguza nguvu za hoja iliyoko mbele kwa majibu kuwa chama kipo mbioni kujiunda upya na kipewe nafasi.
Mabadiliko hayatalenga kujivua gamba bali kufunika kombe. Hii itakuwa sawa na kunywa 'asprin' homa ipungue bila kutibu tatizo.
Kwa maoni yangu kama hatua kali hazitachukuliwa dhidi ya watuhumiwa ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nyadhifa au kufukuzwa, hakutakuwa na mabadiliko yoyote na itakuwa ni njia rahisi ya kukipeleka chama kule UNIP na KANU zilipopunzika.