Mambo 10 kuhusu Dick Cheney, Makamu wa Rais aliyekuwa na nguvu zaidi katika historia ya Marekani

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,783
66,962
Mfahamu Dick Cheney aliyepata kuwa Makamu wa Rais wa 46 nchini Marekani katika utawala wa Rais George W. Bush

1. Jina lake kamili ni Richard Bruce Cheney, mzaliwa wa Lincoln huko Nebraska nchini Marekani, alizaliwa 30 January 1941. Ni mwanasiasa mashuhuri wa chama cha Republican lakini pia ni mfanyabiashara nguli nchini Marekani. Baba yake alikuwa ni mfanyakazi wa sekta ya kilimo nchini humo huku mama yake akiwa ni mama wa nyumbani.

2. Akiwa na miaka 18 alipata bahati ya kusomeshwa katika chuo kikuu cha Yale lakini akafeli (kudisco) kutokana na kupata alama za chini ambazo zilikuwa haziridhishi. hakukata tamaa alirudi masomoni miaka miwili baadae katika chuo kikuu cha Wyoming na kupata degree pamoja na masters yake ya political science mwaka 1966. Hapo ndipo damu ya siasa ilipoanza kumuingia katika mwili wake. Alimuoa rafiki yake wa siku nyingi Lynne Cheney mwaka 1964 wakiwa chuoni. Wawili hao wakaja kupata watoto wawili wa kike ambao ni Mary pamoja na Elizabeth. Mtoto wake wa kwanza Mary Cheney ni shoga na amekuwa akiunga na kusapoti harakati za mashoga!

3. Tofauti na ilivyokuwa kwa viongozi wengi walioshika nyadhifa kubwa na za juu nchini Marekani, Dick Cheney hakuwahi kupita jeshini enzi za ujana wake, hivyo hakuwa anajua mambo mengi ya kijeshi lakini baadae alikuja kuwa mtu hatari sana kwa masuala ya kijeshi. Dick Cheney pia alikwepa kwenda kwenye vita ya Vietnam akisingizia ubize wa masomo.

4. Akiwa na miaka 34 tu alichaguliwa kuwa Mnadhimu mkuu wa Ikulu ya Marekani (White House) katika utawala wa Rais Gerald Ford mwaka 1970. Ni katika nafasi hiyo ndipo Cheney alipokutana na Donald Rumsfeld ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Fursa za Kiuchumi katika Ikulu ya Marekani baadae akaja kuwa Waziri wa Ulinzi. Donald Rumsfeld alikuwa anambeba sana Cheney kwenye utendaji wa kazi. "Ndege wafananao huruka pamoja" ni kweli kabisa kwani Cheney na Rumsfeld walitengeneza urafiki ambao ulikuja kudumu na kuwa na faida kubwa kwa siku za usoni kwa kuwa walifanana sana vitu vingi hasa ubabe.

5. Mwaka 1978 Cheney alishinda uchaguzi na kuwa katika Bunge la Seneti la Marekani ambapo alihudumu hadi mwaka 1989 katika kipindi chake atakumbukwa kwa kupiga kura ya hapana dhidi ya kuanzishwa kwa siku ya kitaifa ya kumbukumbu ya Martin Luther king Jr. Pia mwaka 1986 Dick Cheney alipiga kura ya hapana dhidi ya kuachiwa kwa Nelson Mandela wa South Africa aliyekuwa anashikiliwa na Makaburu huko gerezani. Cheney alihojiwa na CNN akasema chama cha ukombozi cha Afrika Kusini (ANC) walikichukulia kama kikundi cha magaidi hivyo wakasema tupige kura ya hapana dhidi ya Mandela ili wasipate nguvu.

6. Dick Cheney alichaguliwa kuwa Waziri wa Ulinzi mwaka 1989 na serikali ya Rais George H.W. Bush (Bush Mkubwa). Cheney alichaguliwa katika nafasi hiyo mara baada ya Bunge la Seneti kumkataa Seneta John Tower kwa kupiga kura ya hapana, ndipo Rais George Bush alipomchagua Cheney na alipitishwa kwa kura za kishindo. Alihudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi chote cha muhula mmoja tu wa madaraka wa Rais George Bush Mkubwa.

7. Akiwa kama Waziri wa Ulinzi akasimamia operation mbalimbali za kijeshi nje ya Marekani. Mojawapo ni kumuondoa madarakani dikteta Manuel Noriega wa Panama mwaka 1989. Pia alisimamia vita ya Marekani dhidi ya Saddam Hussein ijulikanayo kama Vita ya Ghuba ambapo wamarekani waliita " Operation Desert Storm " ambapo Marekani alishindwa na kelele zilikuwa nyingi toka kwa wananchi wa Marekani. Suala hilo lilipelekea Rais George Bush Sr. kupigwa chini kwenye uchaguzi wa mwaka 1993 ambapo Rais Bill Clinton aliingia madarakani na ukawa mwisho wa Waziri wa Ulinzi mbabe ambaye hakupitia jeshini. Lakini kuna mambo hayatokei kwa bahati mbaya bali hupangwa kwanini? utajionea mbele...

8. Mwaka 2001 Rais George W. Bush (Bush Mdogo) alimchagua Dick Cheney kuwa Makamu wa Rais wa Marekani. Wengi walishuku uteuzi huo. Dick Cheney anatajwa kama makamu wa Rais mwenye nguvu zaidi, kwani alikuwa na mamlaka makubwa sana katika utawala wa Rais George Bush alipanga na kuamua vitu vingi kwa maono yake tena nyakati nyingine bila hata ya kumshirikisha Rais George Bush. Kwanza kabisa alimpendekeza rafiki yake wa siku Donald Rumsfeld kwa Rais Bush awe Waziri wa Ulinzi, japo Rumsfeld na Bush walikuwa maadui lakini Rais Bush akakubali. Dick Cheney akawa anapatiwa taarifa nyingi za kiintelejensia za CIA yeye badala ya Rais. pia akampendekeza bibie Condoleeza Rice awe Mshauri wa masuala ya Ulinzi katika uatawala wa Rais Bush na baadae alikuja kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

9. Mara baada ya Mashambulio ya September 11, Marekani ikatangaza vita dhidi ya Ugaidi. Vita hii iliendeshwa kibabe na kusimamiwa na Makamu wa Rais wa Dick Cheney na rafiki yake Donald Rumsfeld ambapo waliitangazia Dunia, Iraq ya Saddam Hussein inawafadhili Al Qaeda na inamiliki silaha za Nyuklia. Nilisema kuna mambo hayatokei kwa bahati mbaya, Dick Cheney aliwekwa pale kwa ajili ya kulipa kisasi dhidi ya Saddam na safari hii Saddama alidakwa na akanyongwa ikawa furaha ya Bush Mkubwa baada ya yeye kumshindwa akiwa Rais. Kwahyo Dick Cheney alikuwa Makamu wa Rais kwasababu maalum sio kwa bahati mbaya.

10. Maisha bila unafki hayaendi, Rais George Bush Sr akajitokeza hadharani na kuponda utatu mtakatifu wa Dick Cheney, Donald Rumsfeld na mwanamama Condoleezza Rice (hajawahi kuolewa wala kupata mtoto) kuwa hao ndio waliompoteza na kufanya utawala wa mwanae Rais George Bush Jr uonekane utawala wa kimabavu na wa hovyo. Wengi walihisi huu ni mchezo wa kuwahadaa watu huku wakiamini George Bush Sr alibariki matendo yote kimyakimya. Kama ilivyoada, january mwaka 2009 Rais George Bush Jr alihitimisha miaka yake 8 ya utawala na ukawa mwisho wa Dick Cheney ofisini kama Makamu wa Rais. Kama alivyotarajiwa siku anaingia ofisini aliifanya kazi yake na kuacha legacy kubwa sana na sidhani kama kwa siku za karibuni atakuja kutokea makamu wa rais kama Dick Cheney. Kila lenye mwanzo halikosi mwisho na nyakati ngumu hazipiti ila watu wagumu hupita.

MV5BOGExMjY0ZGItNDk5NS00OThlLWI3NDItYzdjZDU2MGM2ZDE0XkEyXkFqcGdeQXVyNjUxMjc1OTM@._V1_.jpg
 
View attachment 2046012
Ahsante
 
Mwamba alikuwa anajulikana kwa kutumia nguvu aliyokuwa nayo kufanya maamuzi ambayo yeye alikuwa anaona yanafaa, ata kama yatakuwa ni maamuzi mabaya na yenye athari hasi, mwamba alikuwa hajutii mbele za watu wala kuomba msamaha

Kipindi cha Obama alikuwa anambeza kwamba jamaa ni soft sana, kuanzia yeye hadi serikali yake, ispokuwa alimsifia Obama sehemu moja tu, kwenye operation ya kumpoteza Osama bin laden, hapo tu Obama alimfurahisha Dick
 
Hatariii

Hali iliyopelekea mpaka Bush Mkubwa kuwa na mashaka na hao jamaa kuwa wanaweza wakazamisha utawala wa mwanae
Nakumbuka walipokuwa wanahalalisha kuivamia Iraq DR akawa anasema "There are no good targets in Afghanistan, let's bomb Iraq".....
Kupiga mabomu Tora-Bora (Afghanistan) wakijifanya wanamtafuta Osama bin Laden ilikuwa zuga tuu, lengo haswa lilikuwa na Iraq.
 
Back
Top Bottom