Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
1703317603126.png

Utumbo, uwe wa mbuzi au wa ng’ombe kwa asili ni mgumu, hivyo kuhitaji muda wa kutosha wa kupika ili uive.

Baadhi ya watu katika mapishi ya utumbo, hutumia viungo kama vile tangawizi, limao, papai bichi, siki na ajinamoto ili kuufanya uive mapema.

Wapo pia wanaotumia sufuria isiyoruhusu mvuke kutoka wakati wa kupika (pressure cooker) ambayo huwezesha utumbo kuiva ndani ya muda mfupi.

Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni baadhi ya mamalishe hutumia dawatiba aina ya panadol wakidai inalainisha na kuwahisha utumbo kuiva.

Mamalishe anayefanya biashara Buguruni, aliyejitambulisha kwa jina la Mama Aziza anasema hutumia panadol kupika utumbo.

Anasema alianza kutumia dawa hiyo kutokana na ushauri aliopewa na rafiki aliyekuwa akifanya kazi kwenye mgahawa uliopo Kariakoo, jijini hapa.

“Sikuwa nafahamu matumizi haya ya panadol, rafiki yangu alipokuja kwenye biashara zangu aliniona naweka tangawizi na viungo vingine, ndipo aliponiambia ili mboga yangu iive haraka niweke dawa hiyo. Nilipojaribu niliona matokeo na ninatumia kidonge kimoja hadi viwili,” anasema.

Mama Aziza anasema hafahamu iwapo kuna madhara ya kuchemsha utumbo kwa kuweka panadol, lakini alitumia njia hiyo kwa kuamini ni kilainishi kama vilivyo vingine vinavyowekwa kwenye nyama.

Mamalishe eneo la Kimanga, jijini Dar es Salaam, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, anasema anatumia dawatiba hiyo ili kuokoa muda wa kuchemsha supu.

Anasema asubuhi ni muda wenye wateja wengi, hivyo hutumia kidonge kimoja kuivisha kwa haraka utumbo na pia kupunguza matumizi ya mkaa katika upishi.

Ernest Kimbau, mtaalamu wa ufamasia, anasema madhara yanaweza kuwapo kwa sababu dawatiba ina kiwango ambacho watu wanatakiwa kutumia.

Anasema panadol ina kiwango chake na kinapozidi ni kuwa mtu amejizidishia dawa na inabadilika kuwa sumu inayoweza kuleta tatizo kwenye ini. Anasema anayekunywa supu iliyowekwa panadol maana yake ni kuwa anakula dawa bila utaratibu, kitendo ambacho si kizuri.

Mwananchi
 
Kansa kansa kansa ndio maana imeshamiri sanaa hapa nchini sasaa....mara ya Koo mara matiti ...mara kizazi etc
 
• Tumeamua kujiua wenyewe, kwa kukosa maarifa 😟
 
Imeanza kutumika kitambo tu sema ndio hivyo watu hatufatilii, kuna rafiki angu mmoja aliniambia mama ake alikuwa anatumia panadol kuivisha maharage wakiwa wadogo, sasa hivi ni kijana mkubwa tu... sasa fikiria miaka kama 10-15 nyuma huko ilikuwa inatumika sasa hivi mchanganyiko utakuwa balaa
No wonder watu wanaumwa sana.
Hii ni hatari sana kwa afya zetu, hasa kwa tunaokula mitaani mara nyingi.
 
Back
Top Bottom