Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Discussion in 'JF Doctor' started by Castle, Apr 6, 2009.

 1. Castle

  Castle Member

  #1
  Apr 6, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 87
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Wakuu habari za leo, nina ndugu yangu anasumbuliwa sana na vidonda vya tumbo tangu mwaka 1993 alipopima na kugundulika kuwa ana matatizo hayo.

  Ombi langu kwenu kama kuna mtu anafahamu dawa ya vidonda vya tumbo hata kama ya kienyejei naomba msaada wenu wa wapi inapatikana na kiasi gani. Alishatumia dawa za aina mbalimbali mpaka ile dozi kubwa ya HELIGO KIT, lakini bado.

  Naomba msaada wenu!
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mwambie apunguze mawazo na awe ana kunywa mazima.
  Ajitahidi kukimbia vyakula vyenye tindikali?? (Acid) kama Limau, ndimu, binzari, maharage, pombe kali au pombe kwa ujumla nk ...

  Kwa nyie nduguze mjitahidi kuwa naye kwa karibu na kumkeep busy ili asiwe na muda wa kukaa na kufikiri saana.
   
 3. a

  aanntumaini New Member

  #3
  Apr 6, 2009
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vidonda vya tumbo havisababishwi na kile unachokula bali kile kinachokula wewe hivyo tafadhali msaidieni kufaham ni nini kinamla?anawaza nini,na kwakua ni mda mrefu sasa atumie maziwa wengine wanasisitiza ya mbuzi na kupunguza vitu vya acid kwakua tayari kuna michubuko,asante
   
 4. p

  p53 JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Katika matibabu yake alishapewa antibiotics yoyote au ni antihistamines tu?mara nyingi normal flora helicobacter pylori ndiyo chanzo kikubwa cha vidonda vya tumbo.

  Sasa, kimatibabu pamoja na hizo H2antihistamines lazima uwadhibiti hawa jamaa pia kwa antibiotics.

  Sikonge kakushauri vizuri,vidonda vya tumbo kama hypertension matibabu yake yanaambatana na lifestyle change. Kama anavuta sigara aache. Aepuke vyakula vyenye mafuta mengi,spices na vyenye acid. Asitumie any non steroidal antiinflammatory drug kama aspirin, ibuprofen nk.

  Dawa pekee hazitoshi bila kubadili style yake ya maisha kwani vidonda vitakuwa haviponi au vitajirudia. Jaribu kuzingatia matibabu na ushauri wa daktari wako kabla hujaenda kwa waganga wa kienyeji
   
 5. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  HELIGO KIT in antibiotics ndani yake!

  Ushauri!

  Aende kwa vipimo zaidi, inawezekana sio vidonda vya tumbo ambavyo tunavihisi/fahamu (hivyo vya H. pylori, NSAIDs, ama vya mawazo); yaweza kuwa ugonjwa mwingine kama Crohn's disease, matatizo ya kifuko cha nyongo, na syndrome yenye my favourite name- Zollinger-Ellison syndrome!
   
 6. p

  p53 JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hahaha mazee umenikumbusha mbali sana na Zollinger-Ellison syndrome..lakini hata h2 antihistamines like cimetidine zingeiondoa kama ingekuwepo.
  anyway ushauri wako mzuri lakini mimi bado nasisitiza kuhusu kupata matibabu bora na kufuata ushauri wa daktari wake kama ugonjwa wake utabaki kuwa vidonda vya tumbo.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Dawa ya vidonda vya tumbo Mfahamishe huyo jamaa anayeumwa na Vidonda vya Tumbo atumie Dawa ya Hii ya Kienyeji Akiamka Asubuhi kabla ya kula kitu akojowe mkojo wake mwenyewe kwa kipimo cha Glasi moja awe anakunywa mkojo wake kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa Siku Saba kisha Aende kupima hivyo Vidonda vya Tumbo Vitapona na kukauka kabisa Mwambie ajaribu kutumia hiyo Dawa itamsaidia Sana.

  Tahadhari:
  Kabla ya kunywa huo Mkojo wake aende kupima Hospitali huo mkojo wake je unayo maradhi ya Zinaa au hauna? Ahakikishe Mkojo hauna Maradhi yoyote yale ndio anaweza kuutumia kwa kunywa .
   
 8. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  We mzizi mkavu, kweli wewe kiboko. Yaani jamaa akakinge nanii yake kwa siku saba na kuinywa? Du!
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Ndio Akinge (Urine) wake awe anakunywa kila Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa wiki moja aende kupima hivyo Vidonda vyake vya Tumbo vitakuwa Vimekwisha kauka na Matatizo yake yatakuwa yamekwisha nasema kweli simtanii hiyo dawa imewasaidia wengi.Kabla ya kunyw a:Mkojo wake akaupime hospitali je mkojo wake hauna maradhi yoyote yale? ndipo anaweza kutumia kwa kunywa.
   
 10. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Tena akiuvundika huo mkojo ndio bora zaidi, hata mie nimeona watu wamepona kwa dawa hiyo.
   
 11. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hizi dawa zingine jamani zahitaji moyo,ninachojiuliza huyu aliyegundua dawa hii alikuwa anatafuta nini mpaka akafanikisha ugunduzi huu,any way kama pretty na mzizimkavu wako serious though I can't see it in their words,mgonjwa akashauriwe atumie dawa husika.DAWA HII NI ZAIDI YA DAWA YA KIENYEJI.
   
 12. K

  Kungurumweupe JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 317
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mzee wewe ni msabato masalia nini?!
   
 13. K

  Kungurumweupe JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 317
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Dawa ya vidonda vya tumbo ni mchanganyiko wa asali mbichi na juice ya alovera katika ratio ya 1:1. Tumia vijiko vya chakula viwili asubuhi, viwili mchana na viwili usiku kwa muda wa mwezi mmoja itakusaidia! Pia mwambie apunguze mawazo na ajitahidi kula ili tumbo lake liwe na digestable food material kwa muda mrefu!

  How it works:

  Kwanza, layer nene ya mchanganyiko huu hufunika kabisa vidonda vya tumbo na kuzuia uwezekano wa intestinal acids (e.g week hydrochloric acid, HCL) kuendelea kuishambulia ile ngozi laini iliyoathilika (vidonda).

  Pili, wakati alovera juice (chemical) inatibu vidonda vya tumbo, asali inafanya kazi ya ku-hold still hiyo alovera chemical ili iendelee kukaa palepale kwenye kidonda(Asali inatumika kama binding material). So the mixture will persistently coat the infected area, hence it completely removes any further possibility of the intestinal acids and any other corrosive chemicals to reach that area.
   
  Last edited: Apr 20, 2009
 14. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Jana jamaa kaniambia eti mafuta ya mamba ni dawa nzuri sana.
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hizi ndio tiba mbadala wandugu na siyo utani!
  Mkojo wako lakini, siyo wa mtu mwingine na unatibu magonjwa mengi sana.
   
 16. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Castle,

  Kwanza mpe pole sana. Mimi siyo Daktari ila ninajua dawa ya kienyeji ambayo niliwahi kuelekezwa kwa ajili ya my wife wangu, na alipoitumia akapona kabisa na ninatamani siku moja nimpate Daktari aliyebobea katika ugonjwa huu anielezee kwa undani.

  Dawa yenyewe ni hivi, chukua kokwa la parachichi, likatekate vipande vidogovidogo kisha anika juani mpaka likauke. Baadae saga ili kupata unga laini. Chukua yai la kuku wa kienyeji, pasua utoe kile kiini chenye rangi ya njano, changanya na ule unga ambao umeandaa awali, koroga ili kupata mchanganyiko mzuri.

  Kisha mpe mgonjwa wako anywe kijiko kimoja mara tatu, baada ya siku tatu atakuwa amepona.

  Baada ya hapo akitaka kujua kama amepona au la, anaweza kufanya test ya kawaida kabisa kwa kula maharage, au chakula chenye pili*2 au akaenda kupima hospitali kabisa.

  Ukifanikiwa ni PM.
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Ndugu Che Kalizozele hiyo Dawa niliyosema Ya kutibu Mgonjwa Wa Vidonda Vya Tumbo nimeipata katika vitabu vya zamani sana vya Uganga wa Kienyeji vya Mwaka 1200 na Huo Utaalamu wa Kutumia Mkojo Kwenye Hospitali hawajuwi hata Ma Proffeser hawaoni ndani usione kuwa natani hiyo ni kweli na wengi waliojaribu wamepona.

  Hakuna Dawa Ya kutibu Vidonda vya Tumbo yaani kwa lugha ya kigeni ni (Ulser) hakuna Hospitali ipo ya kutuliza tu sio kutibu Kunguru Mweupe kuna Maradhi ambayo hayawezi kutibika Hospitalini lakini kwa Wataalamu wa Kienyeji wanaweza kutibu kama Ugonjwa wa Pumu ugonjwa wa kisukari, Ugonjwa wa Kifafa, Ugonjwa wa Wendawazimu Kupooza na Ugonjwa wa Saratani (Cancer) na Ugonjwa Hepatitis B Virus.

  Mpaka sasa hakuna Dawa za kutibu hayo maradhi ila zipo za kutuliza sio kuyamaliza Maradhi kinachotakiwa kwa Mgonjwa ni kujaribu kutumia Dawa ili kuona kama itaweza kumsaidia sio kupinga jamani Wenzangu tunajaribu kuelimishana sina kushindana asanteni sana.
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  mafuta ya Mamba sio Dawa ya kutibu Maradhi ya Vidonda vya Tumbo Jaribu kutumia Urine wako mwenyewe kila siku ukinge Asubuhi Glasi moja unywe kabla ya kula kitu kwa muda wa siku 7 kisha uende kupima utakuta vidonda vyote vya Tumbo vimekauka na hiyo wamejaribu watu wengi imewasaidia ukiweza fanya hukuweza Achana nao itawasaidia wengine wenye huo ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo asante sana.
   
 19. L

  Lusajo Kyejo Member

  #19
  Apr 23, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 33
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inawezekana ikawa kweli,maana mimi nakumbuka ilikuwa 1994,nilikuwa nasumbuliwa na jino halafu nilikuwa ugenini nikuwa hapo Livingstone Zambia,sikuwa nafedha ya kutosha kung"oa jino nikashauliwa na mtu,lakini mimi hakuwa kunywa,niliambiwa asubuhi mapema kabla ya kula chochote nichukue glasi moja la mkojo wangu wa kwanza baada ya kuamka nisukutue kwenye meno na niteme kwa siku 3,nikafanya hivyo,leo ni mwaka 2009 sijawahi kuumwa jino mpaka leo,inawezekana Mzizi mkavu ni mkweli kabisa,kwani si ni mkojo wako kwani kunashida gani.
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Lusajo Kyejo Waeleze wewe ndio labda watamini wanafikiri mimi ninawadanganya kuwa Mkojo wako mwenyewe unatibu Maradhi ya Vidonda vya Tumbo? wanafikiri ninasema maneno ya uongo jaribu kuwaeleza wewe labda wataelewa vizuri asante sana ndugu Lusajo Kyejo
   
Loading...