Mama Samia Suluhu: Rais anawasalimia, anasema tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu

Sirikali inaleta taharuki kwa kutotoa taarifa mahali aliko rais wetu kipenzi, pengine katekwa na wasiojulikana.

Taarifa gani zaidi na taarifa wameshatoa, Leo mama Tanga, Mama katoa salam za Rais na kasema watu washikamane, sasa taarifa gani hizo mnazotaka zaidi, kama mpo na taarifa zaidi basi zitolewe. Nawaamini sana Serikali kwa hili kuliko Lissu.
 
Leo Mama Samia ameanza ziara mkoani Tanga na akiwa kwenye kiwanda kimojawapo alichozindua kinachoshughulika na matunda alipata nafasi ya kusalimu wananchi baada ya kuombwa na mkuu wa mkoa wa Tanga ambapo alianza na salam kutoka kwa Rais Magufuli

"Kabla ya kuwapongeza niwasalimie salam za Rais anawasalimia, anasema tuendelee tuchape kazi, kipindi hiki tushikane tujenge mshikamano, tujenge upendo, tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu"

Baada ya salam hizo Mama Samia amewapongeza kwa kuwa na kiwanda kwani ni mkombozi.

Pia soma > Mama Samia: Katika wakati muhimu Watanzania kushikamana ni wakati huu, Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje yakatuparaganya vichwa
Nikumbusheni ni kazi ipi vilee!
 
Endelea kufanya kazi zako,kuwa ana amani. Magufuli yupo hai sema kuonekana itachukua miezi. Hivyo chapa kazi.Magufuli si O2 .Kwamba tusipomuona basi tutakosa hewa.
Fanya hivyo wewe,sisi tunataka tumuone Rais wetu...au kuna ubaya???

Rais si O2 ila ni kiongozi wetu wa nchi.....
 
Watajua wenyewe, abaki huko huko asije hadi mwaka 2025 kwenye uchaguzi mwingine, yani abaki huko huko, tusimuone kabisa, yani watu usitafute ugali wa familia yako uanze kuwaza mijitu mingine kwamba wapo wapi,
 
Leo Mama Samia ameanza ziara mkoani Tanga na akiwa kwenye kiwanda kimojawapo alichozindua kinachoshughulika na matunda alipata nafasi ya kusalimu wananchi baada ya kuombwa na mkuu wa mkoa wa Tanga ambapo alianza na salam kutoka kwa Rais Magufuli

"Kabla ya kuwapongeza niwasalimie salam za Rais anawasalimia, anasema tuendelee tuchape kazi, kipindi hiki tushikane tujenge mshikamano, tujenge upendo, tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu"

Baada ya salam hizo Mama Samia amewapongeza kwa kuwa na kiwanda kwani ni mkombozi.

Pia soma > Mama Samia: Katika wakati muhimu Watanzania kushikamana ni wakati huu, Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje yakatuparaganya vichwa
Safi na sisi wananchi tunamwombea HERI na amani aendelee kuchapa kazi kutuletea maendeleo
 
Mkuu Hawa binadamu wananishangaza ivi ninani ambaye atakaa milele (hatakufa) Kiukweli inaumiza Sana mtu mwenye akili zake kufanya mambo ambayo hafanani nayo. Ni miaka mitatu iliopita Kuna watu waliamua kuzusha kifo juu ya mwana familia wangu kutokana tu na chuki ( figisu) lakini chaajabu waliozusha ndio wameondoka mwanafamilia wangu you buheri waafya. Nashindwa kumuelewa huyu binadamu kwamba hajui anae panga kifo?
Mh... Ndiyo wanakushangaza leo? Ndiyo unajua hakuna wa kukaa milele leo? Tundu Lissu alipopigwa risasi hukuwa unajua? Wakati Ben Saanane anauawa hukujua kuwa waliomuua hawatakaa milele? Jinga kabisa!
 
Ukimsikiliza kwa umakini huyo bi mkubwa moja kwa moja unapata majibu bila hata kujiuliza mara mbili.
" You can fool some of the people all of the time, and all of the people some of the time, but you can not fool all of the people all of the time".
 
Back
Top Bottom