Rais Samia amewasafishia na kuwatengenezea njia Wanawake kuaminiwa katika nafasi ya Urais wa Taifa letu

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,311
9,740
Ndugu zangu watanzania,

Kwa miaka mingi na yote Taifa letu liliongozwa na marais wa kiume katika ngazi ya Urais,umakamu wa Rais na uwaziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Ilikuwa ni kama utamaduni na ilizoeleka na kuwa kama kawaida kuwa nafasi hizo tatu tajwa zimemilikishwa kwa wanaume. Wananchi wakawa ni kama wana mfumo uliowajenga na kujengeka katika akili zao kuwa Nafasi ya urais ni maalumu kwa ajili ya wanaume na kwamba wakati wa wanawake kupewa na kuaminiwa katika nafasi ya Urais ulikuwa bado haujawadia na kufika.

Lakini ndani ya muda mfupi wa uongozi wa Rais samia ni kama watanzania wamenyweshwa kinywaji kilichowalevya kwa namna wanavyompenda, kumkubali, kumuunga mkono na kuwa na imani kubwa sana na Rais samia.Imefikia hatua Watanzania wanatamani Rais samia aongoze Taifa letu Bila kikomo na wala kusiwe na uchaguzi wa Urais uchaguzi ujao, ili aendelee kusalia ikulu wakati tunaendelea na utaratibu wa kikampeni wa kuwapata wawakilishi wa kata na majimbo.

Rais samia amejenga imani kubwa sana kwa watanzania,sasa njia nyeupee kabisa miaka ijayo kuanzia 2030 kwa mwanamke yeyote atakayetaka kuchukua Fomu ya Urais. Kwa kuwa Rais samia ameshafanya kazi ya kitume ya kuwasafisha njia wanawake kushika uongozi wa ngazi ya juu,.Ameonyesha utulivu wa hali ya juu ulioteka mioyo ya mamilioni ya watanzania. Amefanya kazi zilizogusa maisha ya watanzania na kuleta nuru kwa wanyonge,Tabasamu kwa wanyonge na Faraja na matumaini kwa waliokata Tamaa.

Kwa kuwa ni wakati wa Rais samia ambapo Demokrasia imechanua nchini kuliko wakati mwingine wowote katika Historia ya Taifa letu,Ndio maana mnaona namna watu wanavyozungumza mpaka wanapitiliza mipaka,Ni wakati huu ambao watu wapo huru kufanya siasa za ndani na majukwaani kwa uhuru bila bughudha wala wasiwasi,ni wakati huu wa Rais Samia ambapo hata mtu akisahau kufunga mlango kwa komea hawezi kuamka kwenda kufunga kwa kuwa anajuwa ya kuwa hakuna wakuja kuusukuma mlango wake na kuiba vilivyo ndani.

Ni wakati huu wa Rais samia ambapo tumepiga hatua katika kila nyanja,kila sekta na kila eneo kutokana na sera nzuri za kiuchumi na kiuwekezaji,ameimarisha Demokrasia na diplomasia iliyowavutia wawekezaji ambao siku zote wanapenda kuwekeza mitaji yao mahali penye amani ,usalama na utulivu wa kisiasa,. Amewekeza mabilioni ya fedha katika kila sekta inayogusa maisha ya mamilioni ya watanzania ,kama alivyofanya katika secta ya kilimo kwa kutoa mabilioni kwa mabilioni ya fedha,ambapo sasa kilimo ni biashara inayolipa na secta inayokimbiliwa na Watanzania wengi wasomi na wasio wasomi,sasa kilimo ni fahari na jambo la kujivunia kwa mtanzania.

Embu jiulizeni ndugu zangu watanzania Nani atashangaa siku moja mh Ummy mwalimu akiteuliwa nafasi ya juu ya uongozi wa Taifa letu kati ya zile nafasi tatu? Nani atashituka kwa hilo? Nani asiyefahamu uwezo mkubwa wa kiuongozi na kiutendaji alionao mh ummy mwalimu msomi huyu wa sheria na fahari ya wana Tanga? Ameshika na kupitia wizara ngapi? Wapi ambako hajaacha alama za maendeleo na mafanikio? Wapi ambako hajaleta tija ? Wapi ambako hajaleta matokeo chanya mama huyu mchapa kazi na mwenye moyo wa huruma? Wapi ambako watumishi na watanzania hawakumkumbuka alipohamishwa wizara? Nani amewahi kulalamikia uteuzi wa mh Ummy mwalimu katika wizara yoyote ile? Nani atashangaa siku akipewa nafasi ya juu zaidi?

Vipi kuhusu mh Dr Tulia Acksoni mwansasu Dada msomi na nguli wa sheria ,mwalimu wa sheria,mhadhiri wa sheria ,Naibu mwanasheria mkuu wa serikali mstaafu,spika wa Bunge ,na Rais mtarajiwa wa umoja wa mabunge Duniani? Katika uanadamu wake amefanya mangapi ya kugusa maisha ya watanzania? Kwa sababu uongozi ni kugusa maisha ya watu na kuleta matokeo chanya na kuwapa matumaini watu unaowaongoza Dkt Tulia ameyafanya hayo na anaendelea kuyafanya na kutekeleza kwa weledi wa hali ya juu sana.

Kwa hakika kupitia Rais samia tunakwenda kuona wanawake wengi sana wakikua kiuongozi na kuaminiwa sana.Nani atashangaa siku moja suzani kaganda akiwa IGP? Rais samia licha ya kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania lakini wanawake wanakila sababu ya kutembea kifua mbele na kwa Madaha kuwa wameonyesha uwezo mkubwa na utulivu mkubwa sana wapewapo uongozi. Wameonyesha kuwa wanaweza kuyakabili mambo makubwa na kuyatatua pasipo mihemuko au kukurupuka au jazba,wameonyesha kuwa uongozi unahitaji ngozi ngumu,uvumilivu ,subira,utulivu, stamina na kifua cha uongozi .kwa hakika Rais samia Ameliheshimisha sana Taifa letu Barani Afrika na Dunia nzima kwa ujumla, kwa kuonyesha namna Tanzania tulivyopiga hatua za kisiasa ,tulivyo na vipaji vizuri na hadhina ya viongozi wenye uwezo mkubwa wa kiuongozi.

Sasa hata hamasa ya kusoma kwa watoto wakike imeongezeka sana maana wanaona wanayo fursa na nafasi sawa na wanaume katika kufanikiwa na kufanya vizuri katika kila sekta ,imewajengea kujiamini na kufanya kazi kwa kujiamini pasipo hofu wala wasiwasi,wanaona wanaweza kufanya kazi na kufanikiwa vizuri bila kuwa chini ya uangalizi wa yeyote yule na wakatoa matokeo chanya.

Tanzania inahitaji kutengeneza akina mama Samia wengi zaidi ili Taifa letu liwe na uwezo wa kusonga mbele zaidi,kwa kuwa na viongozi wenye maono makubwa kama alivyo Rais samia,kuwa na Dira,muelekeo, vipaombele,uzalendo,uchapa kazi,weledi na Bidii katika kazi pamoja na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa letu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Nina mashaka huwa unamkejeli Rais.
Kila mtanzania mwenye akili Timamu na anayejitambua ameona uwezo wa kiuongozi aliouonyesha Rais samia na ambao umeleta matokeo chanya kwa kila mtanzania , mwenye kujituma na kufanya kazi kwa bidii,juhudi na maarifa.
 
Anza kwa kuandika hivi "Rais Samia amekata kabisa kiu ya wanawake wote nchini kuaminiwa katika nafasi ya urais......"

Hutakiwi kuyasahau haya maneno "kukata kiu....."
Kwa sasa watanzania wana imani kubwa sana na wanawake na wanatamani akitoka na kumaliza muda wake 2030 aingie mwanamke mwingine kama mh Ummy mwalimu kuliongoza Taifa letu.kwa kuwa wanawake wameonyesha uwezo mkubwa sana katika uongozi na kufanya maamuzi magumu kwa hekima na busara.
 
Nina mashaka na afya ya akili yako, anyway sijasoma bandiko lako

Sent using Jamii Forums mobile app
Nina mashaka na utimamu wa akili na kichwa chako kama unaweza usisome ujumbe halafu ukawa na ujasiri wa kujibu usichosoma ,kwa hakika ni kichaa pekee anaeweza kukataa kuwa wewe una matatizo ya kiakili yanayohitaji matibabu ya haraka sana.
 
Back
Top Bottom