Mama Samia Suluhu: Rais anawasalimia, anasema tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,813
Leo Mama Samia ameanza ziara mkoani Tanga na akiwa kwenye kiwanda kimojawapo alichozindua kinachoshughulika na matunda wilayani Korogwe, alipata nafasi ya kusalimu wananchi baada ya kuombwa na mkuu wa mkoa wa Tanga ambapo alianza na salam kutoka kwa Rais Magufuli

"Kabla ya kuwapongeza niwasalimie salam za Rais anawasalimia, anasema tuendelee tuchape kazi, kipindi hiki tushikane tujenge mshikamano, tujenge upendo, tuchape kazi tulete tija kwa Taifa letu"

Baada ya salam hizo Mama Samia amewapongeza kwa kuwa na kiwanda kwani ni mkombozi.

Pia soma > Mama Samia: Katika wakati muhimu Watanzania kushikamana ni wakati huu, Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje yakatuparaganya vichwa
 
Behaviourist chapa kazi Broo
Acha kuombea watu kifo

Wewe na genge lako mnajisikiaje kupata taarifa hii??
Hii serekali iliyofitinika imekubuhu kwa uongo. Kama Rais ni mzima ajitokeze watu wamuone kwani ugumu hapo uko wapi? Wanachofanya ni kudanganya wapumbavu wachache ambao hawajui kuhoji na ambao hawawezi kutenganisha kati ya ukweli na uongo.
 
Kama nakuona hivi ulivyodhoofu baada ya kuona hii taarifa
 
Hii serekali iliyofitinika imekubuhu kwa uongo. Kama Rais ni mzima ajitokeze watu wamuone kwani ugumu hapo uko wapi? Wanachofanya ni kudanganya wapumbavu wachache ambao hawajui kuhoji na ambao hawawezi kutenganisha kati ya ukweli na uongo.
Acha kujipaka ujinga akilini. Unasatahili kuwa na akili kuliko unachoandika sasa.
 
Back
Top Bottom