Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,264
- 9,715
Ndugu zangu Watanzania,
Rais atakayepokea madaraka kutoka kwa Rais samia baada ya kukamilisha miaka yake kumi madarakani kwa mujibu wa katiba yetu atakuwa na kazi nyepesi sana ya kuliongoza Taifa letu, kwa kuwa atakuta kazi kubwa ya kujenga misingi ya uchumi wa Taifa letu imeshafanywa na kuwekwa na Rais wetu mama Samia.
Atakuta miuondombinu Bora na imara ya Barabara imejengwa kila kona ya Taifa letu ambayo itachochea usafiri na usafirishaji wa mazao mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali nchini kwenda sokoni na sehemu mbalimbali.
Ajaye atakuta Rais samia Amemsafishia njia katika mahusiano ya kimataifa ambapo Taifa letu litaendelea kupokea mafuriko ya wawekezaji, watalii na wafanyabiashara wakubwa kutoka kila pembe ya Dunia. Atakuta mapato yetu ya kila mwezi na mwaka yanaendelea kuongezeka kutokana na kuwa na wigo mpana wa kodi kutokana na kuwa na wawekezaji wa kila aina na biashara mbalimbali nchini pamoja na miradi mbalimbali ya kimkakati itakayoendelea kuleta faida katika Taifa letu.
Ajaye atakuta hali nzuri ya usalama nchini, ujirani mwema, umoja wa kitaifa, mshikamano na uzalendo wa dhati mioyoni mwa watanzania, atakuta Taifa ambalo watu wake wapo imara kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja.
Atakuta huduma bora za kijamii zilizo bora na kuboreshwa kwa kiwango cha juu,atakuta watumishi wa umma wenye morali ya kazi na wenye kujituma makazini na kuleta matokeo chanya kutokana na maslahi mazuri wanayolipwa.
Ajaye atafanya kazi ya kuendeleza tu pale alipoishia Rais samia na kufanya maboresho kiasi ya kisera na kisheria kulingana Na wakati husika wa kuendana na mabadiliko na kasi ya ulimwengu kiuchumi na kiteknolojia. Ajaye atakuta mifumo mizuri ya kisheria katika kuongoza nchi, atakuta Taasisi imara zenye kufanya kazi kwa weledi, uadilifu pasipo kusukumwa au kusimamiwa au kumtegemea mtu mmoja pekee.
Ajaye atakuta Taifa lililo shamiri na kuchanua kwa Demokrasia na uhuru wa kuwawezesha watu kutoa mawazo yao katika ujenzi wa Taifa letu. Atakuta Taifa lenye amani na utulivu na lenye utayari wa kufanya kazi kwa uzalendo na moyo wa uzalendo.
Kwa hakika ajaye baada ya miaka kumi ya Rais samia madarakani atakuwa na kazi ndogo sana na Nyepesi sana katika kuliongoza Taifa letu kwakuwa kazi kubwa Imefanywa na inaendelea kufanywa na Rais samia wakati huu ambao anafanya kazi usiku na mchana pasipo kupumzika na ndio maana tunaona akifanya kazi hata akiwa ndani ya ndege ili kuhakikisha kuwa Taifa linasonga mbele kwa kasi kubwa sana.
Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.