Chakaza
Platinum Member
- Mar 10, 2007
- 41,017
- 74,670

Kama unamiliki shule ya sekondari na inafika mahali unakuwa na wanafunzi watatu tuu wa kidato cha nne ambao hata hivyo katika mtihani wa taifa wote wanafeli. Wakati huo huo una madeni makubwa ya Kibenki yanayohusiana na shule hiyo hiyo ni wazi huwezi kupambana na msongo mkubwa wa mawazo. Na walio karibu nawe wanapaswa kukupa msaada wa kisaikolojia na ushauri wa kimkakati ili kukutoa katika hali hiyo.
Wapo waliokuwa karibu naye kijamii na kikazi (hasa kichama zaidi) lakini pamoja na kuliona hili hawakumpa ushauri nasaha au alipewa na akaudharau. Na matokeo ndio haya ya kuzidiwa na shinikizo lililoleta yaliyotokea. Poleni wafiwa na wengine tujifunze tuwapo na matatizo kama haya tuwashirikishe wataalamu wengine watusaidie.