Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 9,689
- 14,435
Arusha. Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na wasimamizi wa mirathi ya marehemu mfanyabiashara Zacharia Hans Poppe, pamoja na kampuni ya ZH Poppe Limited.
Wasimamizi hao walikuwa wakiomba zuio la muda dhidi ya Benki ya Biashara Tanzania (TCB) kuzuia kuchukuliwa na kuuzwa kwa mali zilizowekwa rehani kwa ajili ya kurejesha mkopo wa zaidi ya Sh7.4 bilioni.
Maombi hayo ya Madai Na.11792/2026 yaliwasilishwa na Angel Zacharia na Abel Zacharia, ambao ni watoto wa marehemu na wasimamizi wa mirathi yake, pamoja na kampuni ya ZH Poppe Limited.
Wajibu maombi walikuwa TCB, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili Mkuu wa Serikali.
Uamuzi huo ulitolewa Juni 15, 2026 na Jaji Arnold Kirekiano, aliyesikiliza maombi hayo. Nakala ya hukumu imewekwa katika mfumo wa mtandao wa Mahakama.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote na kupitia nyaraka zilizowasilishwa, Mahakama ilihitimisha kuwa waombaji hawakutimiza vigezo vya kisheria vinavyohitajika ili kupewa amri ya muda ya kuzuia benki kuendelea na hatua za kurejesha mkopo wake.
Kutokana na hilo, ombi hilo lilitupiliwa mbali kwa gharama, huku TCB ikiachiwa kuendelea na utekelezaji wa dhamana zake kwa mujibu wa sheria.
Baada ya deni hilo kufikia zaidi ya Sh7.4 bilioni, TCB ilitoa notisi ya mwisho ya kudai malipo na kuanza taratibu za kurejesha fedha zake kupitia mali zilizowekwa rehani.
Hatua hiyo iliwafanya waombaji kufungua maombi ya zuio la muda wakitaka Mahakama iamuru hali ibaki kama ilivyo na kuzuia kukamatwa au kuuzwa kwa malori ya mizigo, malori ya mafuta, trela na mali nyingine hadi muda wa notisi ya kisheria ya siku 90 utakapomalizika.
Waombaji walieleza kuwa kupitia barua ya Machi 25, 2026, walitoa notisi ya nia ya kuishtaki Serikali, wakitarajia kufungua kesi ya msingi dhidi ya TCB baada ya kipindi hicho cha siku 90 kumalizika. Hivyo waliomba Mahakama izuie kwa muda utekelezaji wa dhamana hadi taratibu hizo zikamilike.