Malasusa awa askofu mkuu KKKT, lakini walutheri wengi hawana furaha na amani, nini shida?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,153
Nimefuatilia mwitikio wa waumini wa kanisa la Lutheran hapa Tanzania (KKKT) baada ya Askofu Alex Malasusa kuchaguliwa kuwa askofu mkuu wa kanisa hilo hapa Tanzania. Hali imekuwa tofauti kidogo, kwa waumini kadhaa ambao nimefanikiwa kuwasikiliza ni kama vile hawajafurahia hilo au wamechukizwa kimtindo. Hili nimeligundua zaidi kwa waumini wa dayosisi ya Mashariki na Pwani (dayosisi ambayo inaongozwa na Askofu Malasusa takribani miaka 20 sasa). Machache niliyoweza kuyagundua yakisemwa (kwanini wamekwazika na kuchaguliwa kwa Malasusa) na wale ambao hawakufurahishwa na kuchaguliwa kwa Askofu Malasusa ni haya;

1. Askofu Malasusa kukaa muda mrefu kupitiliza katika dayosisi ya Mashariki na Pwani huku akibadilisha katiba imruhusu kukaa hata milele. (Askofu Malasusa amekuwa askofu wa dayosisi ya Mashariki na Pwani kwa wastani wa miaka 20 sasa)

2. Kurudia kukalia nafasi hiyo hiyo ya uaskofu mkuu wa kanisa. (Miaka kadhaa nyuma alishakuwa askofu mkuu tena).

3. Skendo mbaya ya Uzinzi ya miaka kadhaa ya nyuma (Askofu Malasusa alihusishwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mchungaji mmoja wa kike ambaye alikuwa mke wa mtu, na mwenye mke alikuwa akipambania arejeshewe mke wake)

4. Misimamo kadhaa yenye utata kiimani ambayo hukinzana na baadhi ya wachungaji, mafundisho ya kilutheri au mafundisho mapya katika dayosisi ya Mashariki na Pwani (Malasusa aliwahi kuhusishwa na kuleta fundisho jipya la kuruhusu unywaji pombe kwa walutheri hapa Tanzanua, kupingana na mafundisho na mapokeo ya kilokole ndani ya kanisa la Lutheran)

5. Tabia za Askofu Malasusa kujipendekeza/kujihusisha na watawala hususani kipindi cha Magufuli kiasi cha kukinzana hadharani na misimamo rasmi ya kanisa la Lutherani hapa Tanzania. (Askofu Malasusa inasemekana alikuwa 'chawa' rasmi wa Magufuli na alikuwa mwiba mkali dhidi ya utawala wa Kikwete)

6. Ubabe na ukiritimba wa kimadaraka alionao Askofu Malasusa katika dayosisi ya Mashariki na Pwani. (Sakata la kutaka kumzimisha kinguvu mchungaji Kimaro wa Kijitonyama ni mfano mmojawapo)

Mtu msiyemtaka ndio huyo kaja sasa?
 
5. Tabia za Askofu Malasusa kujipendekeza/kujihusisha na watawala hususani kipindi cha Magufuli kiasi cha kukinzana hadharani na misimamo rasmi ya kanisa la Lutherani hapa Tanzania. (Askofu Malasusa inasemekana alikuwa 'chawa' rasmi wa Magufuli na alikuwa mwiba mkali dhidi ya utawala wa Kikwete)
Hili hapa ndio kubwa! Malasusa ni CCM na Kwa kweli ameshaingiza kanisa kwenye shida mara kadhaa! Mnakumbuka mkutano mkubwa wa Injili ambao tulichangishana Kwa muda mrefu Ili kufanikisha mkutano huo? Na mwisho wa siku wakamruhusu Paul Makonda ahubiri?
 
Dah viongozi wangu wa kiimani sijui wamekuja kuaje ila malasusa hamna mtu pale anyway pongezi ziende kwa watu wa system wamefanikiwa kuinstall pandikizi lao
Yes huyu amewekwa na mipuuzi ya CCM! Anyway uzuri Lutheran Kila Dayosisi Ina Katiba yake!
 
Tutake radhi Mpwa, ni hawa pimbi tu wachache wa CCM please 🙏 hata sisi wenyewe hatupendi!
Nilipenda KKKT mimi ila malasusa alichomfanyia Mwaikali na kumtukana prof Mwakihaba mruteli mnyoofu yule nikahamia rasmi kanisa la kirutheli Africa mashariki. Bagonza anasubiri nini ?
 
Yes huyu amewekwa na mipuuzi ya CCM! Anyway uzuri Lutheran Kila Dayosisi Ina Katiba yake!
Licha ya dayosis kua na katiba, Lutheran hua Kuna transparency ndo maana mara nyingi ni rahis mgogoro kurise.
 
Yes huyu amewekwa na mipuuzi ya CCM! Anyway uzuri Lutheran Kila Dayosisi Ina Katiba yake!
Mkuu, wameshafanya mabadiliko. Dayosisi zote zitatumia Katiba moja. Na kuanzia sasa, hiyo nafasi aliyopata Malasusa, ina nguvu Tanzania nzima. Yaani, anakuwa ana nguvu kuwazidi Maaskofu wote! Ana uwezo hata wa kumuwajibisha Askofu wa jimbo lolote!
Bagonza AJIANDAE!
 
Waluteri Wana furaha

Kwahiyo askofu Dr Alex Malasusa PhD hapo DMP amechaguliwa Wakati na Freeman Mbowe anachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema

KKKT mmetisha sana

Mkitoa Rais wa JMT Sijui atakaa Muda gani kama siyo Sawa na Dipi weldi
Sio lazima ukomenti kila uzi.
 
Mkuu, wameshafanya mabadiliko. Dayosisi zote zitatumia Katiba moja. Na kuanzia sasa, hiyo nafasi aliyopata Malasusa, ina nguvu Tanzania nzima. Yaani, anakuwa ana nguvu kuwazidi Maaskofu wote! Ana uwezo hata wa kumuwajibisha Askofu wa jimbo lolote!
Bagonza AJIANDAE!
Mbona wanataka kurudi kule kule kwenye Mfumo wa kipapa?
 
Back
Top Bottom