Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Bro una yumba kinoma noma !
Hujaonesha wapi, kivipi, kwa nini, na unanisahihishaje.

Kwa sababu hakuna nilipoyumba unapoweza kunionesha.

Wewe unayemuamini Mungu ambaye unasema ana haki kabisa, lakini kaua viumbe kibao wasio na hatia katika gharika, ndiye unayumba vibaya sana.

Unaamini Mungu wa haki kabisa kaua viumbe wasio na hatia kwa makosa ambayo hawajayafanya.

Una contradiction kubwa sana katika imani yako.

Umeyumba vibaya sana.

Sio mimi niliyeyumba, wewe ndiye uliyeyumba.
 
Huyu Kiranga ni mweupe sana kichwani huwa hawezi kujenga na kupangua hoja, anachojua yeye kuruka ruka tu kutoka mada moja kwenda nyingine ambazo napo ukimfuata hukohuko unamkuta pia ni mweupe akiona umemzidi zaidi anarudi kwa Id nyingine .
Kama mimi ni mweupe kichwani, hilo pia litakuwa ushahidi kwamba Mungu wa haki yote, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Aangekuwepo, asingeninyima akili mimi niwe mweupe sana kichwani, halafu nyie wenzangu muwe na akili za kuniona mimi mweupe sana kichwani.

Mungu wa kufanya hivyo atakuwa na upendeleo wa kuwafanya watu fulani wawe na akili, na wengine wawe weupe sana kichwani.

Tofauti ya watu katika uwezo wao kiakili ni ushahidi kwamba huyo Mungu hayupo.
 
Nimepitia huu uzi nimegundua kuwa watu wachache tu hapa ndio wana "reason".

Ila wengi ni watu wasio na reason na chochote watakachoambiwa " In the name of God" hata kiwe kisichokuwa na mashiko basi wao watashikilia hivyo hivyo bila kuhoji kwanini iwe hivyo?

Ubaya mkubwa zaidi ni kuwa hao wengi ambao hawataki kuhoji mioyoni mwao wanahoji na wanakubaliana kabisa na hizi facts za mleta mada na Kiranga

Tatizo ule unafki wa nje ndio unafanya waandike vijimaneno hapa ili kuficha ule ukweli wanaoukubali moyoni. Lakini huyu Mungu sianazijua mpaka fikra zetu? Kwahiyo ukikubali kimoyomoyo tayari ushamkataa.

NB: Mimi ni mkristo kwa kurithi, sikuchagua dini mwenyewe nimerithi ya wazazi na kwa mafundisho ya dini yangu niliambiwa Mungu yupo na sifa kedekede.

Lakini kama msomi ambae naweza kukaa na kujenga hoja na wasomi wengine, sina budi kuunga foleni kati ya wale tunaotaka majibu ya maswali yaliyoulizwa maana mpaka sasa hakuna aliejibu zaidi ya kutishiana tishiana tu.
Kuna swali moja dogo tu nimeuliza kwa wanaosema Mungu yupo, sijajibiwa.

Nawauliza, nawaambia, mnaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Thibitsheni.

Mpaka sasa sijapata uthibitisho.

Wanahubiri. Wanapinga. Wanavuruga mjadala. Wanajifaragua.Wanakataa kujibu swali.

Lakini hawajaweza kuthibitisha Mungu yupo.

Mungu anatakiwa asiwe na contradiction. Huyu Mungu wa Biblia na Quran kwa mfano, mtu akiweza kuniondolea contradictions zote zilizopo katika habari zake, sio tu nitakubali, bali pia nitafurahi sana. Contradictions hizo ni hizi.

Kwa uchache.

1. Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, upendo wote na utakatifu wote, kaumba ulimwengu ambao maovu yanaweza kutokea, wakati alikuwa ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezi kutokea? Naomba jibu lisiwe kusema maovu yapo kwa sababu ya shetani. Swali linauliza kabla shetani hajaumbwa Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao shetani hawezi kuwepo. Jibu la swali lisiseme maovu ni matokeo ya dhambi za watu. Mungu angeweza kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani. Jibu lisiseme free will, hatuna hiyo inayoitwa free will katika mengi sana na hata kui define tu watu hawawezi.

2. Inakuwaje Mungu awe ndiyo mtoa rehema ya kumjua, anachagua mwenyewe nani amjue na nani asimjue, halafu mtu akishindwa kumjua Mungu, kwa sababu Mungu hajamchagua huyo mtu kumpa neema yake Mungu ya kumjua, huyo mtu aonekane ana makosa, ahukumiwe kuchomwa moto? Baba anawezaje kumhukumu mtoto ambaye hajui kusoma, kama mtoto hajui kusoma kwa sababu baba ndiye aliyemnyima nafasi ya kwenda shule?

3. Inakuwaje mahakama za watu tu zinakataza mtoto kuhukumiwa kwa makosa ya mzazi, lakini vitabu vya Mungu vinasema Mungu anahukumu watoto na wajukuu vizazi hata vizazi? Kwa kosa la mzazi wa zamani sana? Huyu Mungu mbona haki yake haijafikia hata haki yetu watu tu?

4. Mnasema Mungu anajua yote. Anayajua maisha ya mtu yote mwanzo mpaka mwisho kabla hata mtu hajaishi. Na anachojua huyo Mungu kitatokea, ni lazima kitokee. Anavyojua si kama utabiri wa hali ya hewa kwamba kuna 80% ya mvua. Yeye anajua kitu kamili hakina utata. Sasa kama anajua hivyo, ina maana mtu muuaji, alimjua huyu atakuwa muuaji kabla hata hajazaliwa. Na muuaji huyo hawezi kuepuka kuua hata afanye nini. Kwa sababu kuepuka kuua wakati Mungu kashajua huyu ataua ni kum prove Mungu wrong. Sasa kama huyu mtu anaenda kuwa muuaji, na hana jinsi ya kuepuka hilo, tutasemaje ana uhuru wa kuamua na anaua kwa uamuzu wake na atahukumiwa motoni kwa uuaji?

5. Mbona hivyo vitabu vinavyosemwa ni vya Mungu vina contradictions lukuki?

6. Mbona huyo Mungu mnayemsema yupo hathibitishiki? Anajificha asijulikane vizuri kwa nini? Kwa nini hakufanya ulimwengu uweze kumjua vizuri bila uwezo wowote wa kuwepo ubishi juu ya uwepo wake?

7. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anaweza kuumba jiwe zito sana kiasi yeye mwenyewe ashindwe kulibeba? Akiweza kuumba jiwe hilo, atakuwa hawezi yote, maana kuna jiwe atakuwa kashindwa kulibeba. Akishindwa kuumba jiwe hilo, atakuwa hawezi yote maana kuna jiwe atakuwa kashindwa kuliumba.

8. Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ameruhusu kifo kitenganishe wapendanao, baba na mama, wazazi na mtoto, marafiki etc, wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kuwepo?

Kwa nini watetezi wa Quran waajitapa sana kusema vitu fulani vichache vimethibitishwa kisayansi, kuinadi Quran kama kitabu cha ukweli, wakati vingi sana vina contradictions ama vinapingana na sayansi ama havijathibitishwa kisayansi, hawasemi vinapingana nansayansi au havijathibitishwa kisayansi?

10.Kama kuna Mungu kweli, kwa nini karuhusu confusion ya dini nyingi tofauti kuwa na vitabu vingi tofauti vyote vinasema vya Mungu wa kweli?

Kwa leo tuishie na maswali haya 10.

Wwanaosema Mungu yupo wanaweza kujibu?
 
Hapana. Namna watu wanavyotumia vibaya dhana ya Mungu ni sehemu ya uthibitisho kuwa hakuna kitu kama hicho. Ndio kama hivyo inavyofahamika wazi kuwa kifo ni sehemu ya lazima ya mwanadamu lakini kinatumika kama sehemu ya uthibitisho was uwepo wake Mungu, sawasawa na hali ya kuishi. So utasikia watu wanasema kuishi ni kwa neema ya Mungu tu? Na wakati huo huo pia kufa ni kwa mapenzi yake? Unaweza kuona mkanganyiko huu ukivyo.
Msingi wa dhana ya uwepo wa Mungu ni kifo?
 
Nimepitia huu uzi nimegundua kuwa watu wachache tu hapa ndio wana "reason".

Ila wengi ni watu wasio na reason na chochote watakachoambiwa " In the name of God" hata kiwe kisichokuwa na mashiko basi wao watashikilia hivyo hivyo bila kuhoji kwanini iwe hivyo?

Ubaya mkubwa zaidi ni kuwa hao wengi ambao hawataki kuhoji mioyoni mwao wanahoji na wanakubaliana kabisa na hizi facts za mleta mada na Kiranga

Tatizo ule unafki wa nje ndio unafanya waandike vijimaneno hapa ili kuficha ule ukweli wanaoukubali moyoni. Lakini huyu Mungu sianazijua mpaka fikra zetu? Kwahiyo ukikubali kimoyomoyo tayari ushamkataa.

NB: Mimi ni mkristo kwa kurithi, sikuchagua dini mwenyewe nimerithi ya wazazi na kwa mafundisho ya dini yangu niliambiwa Mungu yupo na sifa kedekede.

Lakini kama msomi ambae naweza kukaa na kujenga hoja na wasomi wengine, sina budi kuunga foleni kati ya wale tunaotaka majibu ya maswali yaliyoulizwa maana mpaka sasa hakuna aliejibu zaidi ya kutishiana tishiana tu.
Kufuata tamaduni na mambo yaliyokuzunguka kwenye jamii uliyozaliwa na kukulia ni jambo la kawaida halina mjadala,kama ungezaliwa misituni huko sidhani hata kama leo hii ungekuwa na huo usomi.

Hivyo kukulia kwenye imani ya uwepo wa Mungu na ukristo sio hoja ila kama hadi sasa upo kwenye hizo imani kwa sababu tu umezaliwa na kukulia katika hizo imani basi hilo ni tatizo lako,usitafute wa kumtupia lawama kwa sababu hakuna anayekulazimisha kuendelea na hizo imani.
 
CHARMILTON nimependa sana bandiko lako ila nimecheka sana asee umewaza!!na sijaona majibu ya kwanini tuna appendix na mwanamme chuchu za nini?😀😀😀
 
Mungu ndiye atakuwa anakosea. Kwa uwezo wrote alionao, wala asingeruhusu Kiranga kuandika yote haya! Unaweza kuona namna huyu Mungu alivyo mdhaifu na wala hakuna kitu kama hicho.
Kwa namna ya pekee mungu amemuumba binadam tofauti na viumbe vingine na amemuweka kwenye daraja la juu kuliko viumbe vyote na ndiye mtawala ya vyote hapa duniani. Zaidi ya hapo amempa binadam uwezo wa kupambanua baya na jema na kwa kila baya hulipwa kwa dhambi na kila jema hulipwa kwa thawabu.
Hili ndiyo hubiri kubwa kwa dini zote na hata mila zetu. Lakini kwa jeuri na kiburi tunayaponda mengi ambayo tuliyofundishwa kuyaenzi na kuyaenzi yale ambayo hayamfurahisi mola wetu.
Jeuri yetu yote inaisha pale mungu anapositisha pumzi zetu na hayo ya mbele hakuna wa kuyahadithia ila yeye kupitia vitabu vyake vitukufu
 
Kufuata tamaduni na mambo yaliyokuzunguka kwenye jamii uliyozaliwa na kukulia ni jambo la kawaida halina mjadala,kama ungezaliwa misituni huko sidhani hata kama leo hii ungekuwa na huo usomi.

Hivyo kukulia kwenye imani ya uwepo wa Mungu na ukristo sio hoja ila kama hadi sasa upo kwenye hizo imani kwa sababu tu umezaliwa na kukulia katika hizo imani basi hilo ni tatizo lako,usitafute wa kumtupia lawama kwa sababu hakuna anayekulazimisha kuendelea na hizo imani.
Kama umesoma vizuri katika aya yangu ya mwisho nimeomba na mimi kupatiwa majibu ya maswali yaliyoulizwa kuanzia mwanzo wa uzi kwa 'facts' na sio porojo na mboyoyo zisizoeleweka.

Mbona maswali yenyewe yako wazi sana na yanaeleweka? Mnashindwa nini kuyajibu ili kutetea hoja zenu?
 
Kuna swali moja dogo tu nimeuliza kwa wanaosema Mungu yupo, sijajibiwa.

Nawauliza, nawaambia, mnaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Thibitsheni.

Mpaka sasa sijapata uthibitisho.

Wanahubiri. Wanapinga. Wanavuruga mjadala. Wanajifaragua.Wanakataa kujibu swali.

Lakini hawajaweza kuthibitisha Mungu yupo.

Mungu anatakiwa asiwe na contradiction. Huyu Mungu wa Biblia na Quran kwa mfano, mtu akiweza kuniondolea contradictions zote zilizopo katika habari zake, sio tu nitakubali, bali pia nitafurahi sana. Contradictions hizo ni hizi.

Kwa uchache.

1. Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, upendo wote na utakatifu wote, kaumba ulimwengu ambao maovu yanaweza kutokea, wakati alikuwa ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezi kutokea? Naomba jibu lisiwe kusema maovu yapo kwa sababu ya shetani. Swali linauliza kabla shetani hajaumbwa Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao shetani hawezi kuwepo. Jibu la swali lisiseme maovu ni matokeo ya dhambi za watu. Mungu angeweza kuumba ulimwengu ambao dhambi haiwezekani. Jibu lisiseme free will, hatuna hiyo inayoitwa free will katika mengi sana na hata kui define tu watu hawawezi.

2. Inakuwaje Mungu awe ndiyo mtoa rehema ya kumjua, anachagua mwenyewe nani amjue na nani asimjue, halafu mtu akishindwa kumjua Mungu, kwa sababu Mungu hajamchagua huyo mtu kumpa neema yake Mungu ya kumjua, huyo mtu aonekane ana makosa, ahukumiwe kuchomwa moto? Baba anawezaje kumhukumu mtoto ambaye hajui kusoma, kama mtoto hajui kusoma kwa sababu baba ndiye aliyemnyima nafasi ya kwenda shule?

3. Inakuwaje mahakama za watu tu zinakataza mtoto kuhukumiwa kwa makosa ya mzazi, lakini vitabu vya Mungu vinasema Mungu anahukumu watoto na wajukuu vizazi hata vizazi? Kwa kosa la mzazi wa zamani sana? Huyu Mungu mbona haki yake haijafikia hata haki yetu watu tu?

4. Mnasema Mungu anajua yote. Anayajua maisha ya mtu yote mwanzo mpaka mwisho kabla hata mtu hajaishi. Na anachojua huyo Mungu kitatokea, ni lazima kitokee. Anavyojua si kama utabiri wa hali ya hewa kwamba kuna 80% ya mvua. Yeye anajua kitu kamili hakina utata. Sasa kama anajua hivyo, ina maana mtu muuaji, alimjua huyu atakuwa muuaji kabla hata hajazaliwa. Na muuaji huyo hawezi kuepuka kuua hata afanye nini. Kwa sababu kuepuka kuua wakati Mungu kashajua huyu ataua ni kum prove Mungu wrong. Sasa kama huyu mtu anaenda kuwa muuaji, na hana jinsi ya kuepuka hilo, tutasemaje ana uhuru wa kuamua na anaua kwa uamuzu wake na atahukumiwa motoni kwa uuaji?

5. Mbona hivyo vitabu vinavyosemwa ni vya Mungu vina contradictions lukuki?

6. Mbona huyo Mungu mnayemsema yupo hathibitishiki? Anajificha asijulikane vizuri kwa nini? Kwa nini hakufanya ulimwengu uweze kumjua vizuri bila uwezo wowote wa kuwepo ubishi juu ya uwepo wake?

7. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anaweza kuumba jiwe zito sana kiasi yeye mwenyewe ashindwe kulibeba? Akiweza kuumba jiwe hilo, atakuwa hawezi yote, maana kuna jiwe atakuwa kashindwa kulibeba. Akishindwa kuumba jiwe hilo, atakuwa hawezi yote maana kuna jiwe atakuwa kashindwa kuliumba.

8. Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, ameruhusu kifo kitenganishe wapendanao, baba na mama, wazazi na mtoto, marafiki etc, wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani kuwepo?

Kwa nini watetezi wa Quran waajitapa sana kusema vitu fulani vichache vimethibitishwa kisayansi, kuinadi Quran kama kitabu cha ukweli, wakati vingi sana vina contradictions ama vinapingana na sayansi ama havijathibitishwa kisayansi, hawasemi vinapingana nansayansi au havijathibitishwa kisayansi?

10.Kama kuna Mungu kweli, kwa nini karuhusu confusion ya dini nyingi tofauti kuwa na vitabu vingi tofauti vyote vinasema vya Mungu wa kweli?

Kwa leo tuishie na maswali haya 10.

Wwanaosema Mungu yupo wanaweza kujibu?

Naomba kuuliza Kwanza for the sake of interest tu do you believe in God ? Na kama Sio why do you trouble yourself with all those questions after all „GOD DOES NOT EXIST“ Kwanini usiendelee tu na maisha yako, na amani yako na ujuzi wako kuliko kusumbuka na Hawa Watu wanaojifanya kuna MUNGU. Or do you want to be converted to their religion that believes there is GOD who is all Good , all KNOWING, TRANSZENDENT, ALMIGHTY, THE UNCAUSED CAUSER, the Absolute Being etc etc. tuwaache tu sisi tuendelee na yetu. Ila Kama unataka kuwa-convinced ili tu uamin then me siwezi kukusaidia kwa kuwa hata Mie Siamini.

Mi mwanasayansi bwana. Napenda 1+1 iwe mbili na nipp njiani hapa kujua the origin of human being mana Hawa Watu wamenichosha hawajanambia asili ya asili ya asili ya asili ya asili ya asili ya mimi mwanadamu, na kwanini mimi nina utashi na akili lakini naambiwa mbwa na kiboko wanyama naowapenda hawana hivi vitu. Ohhh. Tuachane na hawa watu mana kuna wakati najiuliza Kama nimwamini mke wangu au nianze kujiuliza why ana ndude tofauti na mimi kwanini hatukuwa na ndude moja. Ohh sorry niko nje ya mada.
 
Kama umesoma vizuri katika aya yangu ya mwisho nimeomba na mimi kupatiwa majibu ya maswali yaliyoulizwa kuanzia mwanzo wa uzi kwa 'facts' na sio porojo na mboyoyo zisizoeleweka.

Mbona maswali yenyewe yako wazi sana na yanaeleweka? Mnashindwa nini kuyajibu ili kutetea hoja zenu?
Ithibati ya uwepo wa chanzo kikuu chenye maarifa na hekima hautegemei vitabu vya kidini

Kama umezaliwa timamu hushindwi kufahamu hilo kupitia lugha inayojieleza ya kitabia ulimwengu

Shida ni kwamba muanzisha mada kajenga maswali yake yakiwa tayari yana mlengo wa kikundi fulani cha kiitikadi

Hilo ndilo tatizo......

Sasa pia yakubidi kupembua ni nani akupae majibu

Kama ni mtu wa kidini au muumini wa chanzo cha uwepo wa kitu bila itikadi ya kidini..
 
Kuhusu kuuliza au kusema hajui lugha nyingine hili ni swali la kijinga au swali la uongo sababu yeye ndio aliyeleta lugha na watu waka nena.

Ninaposema kwamba usiandike kwa maneno yasiyo ya kiarabu nina maanisha,sababu ukifanya hivyo unapoteza maana ya aya.

Aya ya Qur'an inatakiwa iandikwe kama inavyosomwa,ila kwa ulichokiandika wewe ni kinyume na aya ilivyo.

Qur'an imeandikwa kwa kiarabu ili kubainisha na imeteremka kwa kiarabu kwa sababu mtume alikuwa muarabu. Huu ni utaratibu ambao ni wa haki.

Ukija na maswali mengine,uliza maswali ya kweli.

Hujajibu swali naona unajikanyaga kanyaga

Je mungu ni mwarabu?

Kwanini maneno ya mungu mpaka yaandikwe kwa kiarabu?

Muhamad hakujua lugha yoyote zaidi ya kiarabu ndio maana alitoa mafunzo ya kiarabu au wewe ulitaka atoe mafunfisho kwa lugha ipi?

Nijibu maswali hayo ukishindwa huna mamlaka ya kunilazimisha kuandika kiarabu wakati kutetea kama mungu mwarabu huwezi

"INNAMAL AMALU BI NII YAATI WA INNAMAA LIKULLI MRIII IM MANAWAA"

Kikubwa nia na dhamira ya mtu kiarabu ni lugha kama lugha nyingine kama mungu yupo usinipangie kutumia mafundisho yake mpaka kwa kiarabu alimtumia muhammad kwakuwa alikuwa mwarabu mm si mwarabu
 
Kama umesoma vizuri katika aya yangu ya mwisho nimeomba na mimi kupatiwa majibu ya maswali yaliyoulizwa kuanzia mwanzo wa uzi kwa 'facts' na sio porojo na mboyoyo zisizoeleweka.

Mbona maswali yenyewe yako wazi sana na yanaeleweka? Mnashindwa nini kuyajibu ili kutetea hoja zenu?
Kwanza unapaswa kufahamu kwamba hatuwezi kuwa na majibu kwa kila swali ambalo mtu anajisikia kuuliza kwa sababu Mungu si kama gari iliyoundwa na binaadamu kwamba huyo muundaji wa gari anajua kila kitu kuhusu hiyo gari kwa sababu yeye ndiye aliyeiunda.

Sasa mtu kama wewe ambaye umekulia kwenye imani ya kuamini Mungu lakini hadi sasa wewe mwenyewe hujaona sababu yeyote yenye kukufikirisha kuwepo Mungu,je unadhani hayo maswali ndio yataweza kukufanya ujue msingi wa hii imani ya uwepo wa Mungu?

Mfano muulizaje wa hayo maswali anapinga uwepo wa Mungu ila anauliza mambo ya kuhusu shetani na ahadi za Mungu,kitu ambacho hata akijibiwa na akaridhika hayo majibu hayatafanya yeye aamini Mungu,kwa sababu hakubali dhana ya kuwepo kwake yani haoni lolote lenye kumfanya afikiri hivyo.
 
Na hapo ndiyo penye tatizo,mie nazungumzia kwanza ile fikra ya kukubali kuwepo Mungu maana bila ya kuelewana hapa huko mbele kwenye Mungu gani hatuelewana.

Mfano wewe hapo hauamini Mungu yeyote na ni kwa sababu ya kutokubali ile fikra ya kuwepo Mungu,hauoni lolote lenye kukufikirisha kukubali kuwepo Mungu.

Unatakiwa unieleweshe mungu yupo na jina lake ni .....

Ili na mimi nianze kumfatilia huyo mungu niangalie nafundisho yake

Lakini ukisema mungu yupo halafu huniambii mungu wenyewe ni yupi? ni sawa na kuchukua tani moja za sukari utumbukize katka bahari usitegemee bahari kuwa tamu

Niambie huyo mungu ni yupi?
 
Sasa kama unajua hayupo kwa nini kila kukicha unahangaika na kitu ambacho unajua hakipo?
Kwa sababu kuonesha uongo uko wapi na ukweli uko wapi ni elimu.

Kwa sababu kuamini kisichopo kipo ni ujinga.

Kwa sababu ukiamini dawa ya ugonjwa fulani unaoua ipo, wakati haipo, ukaacha kuishi kwa kujikinga kwa imani utapata dawa, utakufa kwa ujinga huo. Hata kisichopo kinaweza kukuua kwa ujinga wako.

Kwa sababu watu wanaishi kwa hofu kubwa ya Mungu ambaye hayupo.

Kwa sababu watu wanapigwa hela ndefu sana makanisani, misikitini etc kwa imani ya Mungu ambaye hayupo.

Kwa sababu watu wanashikiwa akili na wanasiasa kwa imani ya "fulani ni chaguo la Mungu" wakati Mungu hayupo.

Kwa sababu watu wanaacha kuchunguza sababu halisi za mambo kama chanzo cha ulimwengu, maisha etc kwa kukubali imani za uongo kwamba chanzo ni Mungu.

Kwa sababu naweza kuonesha Mungu huyo hayupo.

Kwa sababu huwezi kuonesha kwamba Mungu huyo yupo.
 
sasa embu elezea ufahamu wako wa kutotambua kuwa mungu hayupo
Ulichoandika hakina mantiki. Inaonekana una matatizo ya kuweka mawazo vizuri kwenye maandishi.

Umeandika kwa double negatives "kutotambua" na "hayupo" ambazo ukizichanganya zinaleta maana kwamba natambua Mungu yupo.

Kitu ambacho si kweli.

Wewe mwenyewe kuandika unachofikiria tu ni shida.

Tutajadiliana vipi?
 
Kwa sababu kuonesha uongo uko wapi na ukweli uko wapi ni elimu.

Kwa sababu kuamini kisichopo kipo ni ujinga.

Kwa sababu ukiamini dawa ya ugonjwa fulani unaoua ipo, wakati haipo, ukaacha kuishi kwa kujikinga kwa imaninutaoata dawa, utakufa kwa ujinga huo. Hata kisichopo kinaweza kukuua kwa ujinga wako.

Kwa sababu watu wanaishi kwa hofu kubwa ya Mungu ambaye hayupo.

Kwa sababu watu wanapigwa hela ndefu sana makanisani, misikitini etc kwa imani ya Mungu ambaye hayupo.

Kwa sababu watu wanashikiwa akili na wanasiasa kwa imani ya "fulani ni chaguo la Mungu" wakati Mungu hayupo.

Kwa sababu watu wanaacha kuchunguza sababu halisi za mambo kama chanzo cha ulimwengu, maisha etc kwa kukubali imani za uongo kwamba chanzo ni Mungu.

Kwa sababu naweza kuinesha Mungu huo hayupo.

Kwa sababu huwezi kuinesha kwamba Mungu huyo yupo.
Unataka kumuona Mungu ?
 
Hayupo huyo allah kamleta muhammad maana inaonekana allah kapata nguvu baada ya kuzaliwa muhammad 570C.E

إذا كان الله يعاقبك فهو ربك و إذا كان يعفو لك فهو الرحمان[/QUOTE]

"Laa ikraah fii diyiin"
 
Back
Top Bottom