Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Unatakiwa unieleweshe mungu yupo na jina lake ni .....

Ili na mimi nianze kumfatilia huyo mungu niangalie nafundisho yake

Lakini ukisema mungu yupo halafu huniambii mungu wenyewe ni yupi? ni sawa na kuchukua tani moja za sukari utumbukize katka bahari usitegemee bahari kuwa tamu

Niambie huyo mungu ni yupi?
Kwanini unakimbilia kutaka kujua mafundisho ya Mungu na kuacha point ya msingi ya dhana ya kuwepo kwake?

Unaruka hoja ya msingi ya dhana ya kuwepo Mungu halafu unataka nikutajie jina la aina ya huyo Mungu wakati hatujajadili kabisa kwa vp kuna hiyo dhana?
 
Naomba kuuliza Kwanza for the sake of interest tu do you believe in God ? Na kama Sio why do you trouble yourself with all those questions after all „GOD DOES NOT EXIST“ Kwanini usiendelee tu na maisha yako, na amani yako na ujuzi wako kuliko kusumbuka na Hawa Watu wanaojifanya kuna MUNGU. Or do you want to be converted to their religion that believes there is GOD who is all Good , all KNOWING, TRANSZENDENT, ALMIGHTY, THE UNCAUSED CAUSER, the Absolute Being etc etc. tuwaache tu sisi tuendelee na yetu. Ila Kama unataka kuwa-convinced ili tu uamin then me siwezi kukusaidia kwa kuwa hata Mie Siamini.

Mi mwanasayansi bwana. Napenda 1+1 iwe mbili na nipp njiani hapa kujua the origin of human being mana Hawa Watu wamenichosha hawajanambia asili ya asili ya asili ya asili ya asili ya asili ya mimi mwanadamu, na kwanini mimi nina utashi na akili lakini naambiwa mbwa na kiboko wanyama naowapenda hawana hivi vitu. Ohhh. Tuachane na hawa watu mana kuna wakati najiuliza Kama nimwamini mke wangu au nianze kujiuliza why ana ndude tofauti na mimi kwanini hatukuwa na ndude moja. Ohh sorry niko nje ya mada.
Soma post namba 2160 mtu mwingine kaniuliza kwa nini ninajadili haya mambo kama Mungu hayupo, nimejibu kirefu.

Ukijua kwamba ugonjwa fulani hauna dawa, ukaona watu wanajiweka katika imani potofu kwamba ugonjwa huo una dawa kiasi cha kutojikinga na ugonjwa huo, kuupata na kufa, kwa sababu ugonjwa hauna dawa, unakuwa umefanya kosa la kutoelimisha watu kwamba ugonjwa hauna dawa na wajikinge.

Tuseme UKIMWI hauna dawa na unaua, watu wanafanya ngono zembe kwa kuamini una dawa, dawa yake muarobaini, wewe kama unajua hauna dawa halafu usiwaambie watu kwamba ugonjwa hauna dawa, muarobaini si dawa, utakuwa unafanya makosa.

Kitu kisichopo, kinaweza kukuua kwa ujinga wa kuamini kwamba kipo.

Ukiwa kwenye ukingo wa ghorofa, mwisho, ukaamini huko kusiko na ghorofa bado kuna kiambata cha ghorofa, ukakanyaga, utaanguka na kufa.

Kiambata hakipo, na kwa sababu hakipo, ujinga wako kuamini kipo unakuua.

Dawa haipo, ujinga wako wa kuamini kipo unaweza kukuua.
 
Ulichoandika hakina mantiki. Inaonekana una matatizo ya kuweka mawazo vizuri kwenye maandishi.

Umeandika kwa double negatives "kutotambua" na "hayupo" ambazo ukizichanganya zinaleta maana kwamba natambua Mungu yupo.

Kitu ambacho si kweli.

Wewe mwenyewe kuandika unachofikiria tu ni shida.

Tutajadiliana vipi?
ufahamu wako ndio umekwamia hapo. ni vigumu sana kuelewa.na kukubali sababu umeshajivisha akilini mwako kuwa hakuna MUNGU lakni wala hujui na huwezi/hutaweza kamwe kujitambua kuwa wewe Kiranga umefikajefikaje hapoulipo na ni nani aliyekuleta hapa duniani labda umejileta mwenyewe.
kama hutambui muumba wa mbingu na dunia basi unaweza kusema hata baba yako huna uhakika kama ni wa kwako kweli.
hayo unayoyapigia chapuo humu ndio yanayoendesha maisha ulimwenguni mazima. kabla hujazaliwa inamaana hukuwepo je umekujaje duniani.
NI KWA UWEZO WA MUNGU KAMLETA MAMAKO AKAKUTANA NA BABAKO WAKAUNGANA UKAWA MWILI MMOJA NA UKAZALIWA Karanga.
 
Wwapi unapata msingi wa swali hilo? Kipi kinachokufanya uamini kwamba naweza kuwa nataka kumuona Mungu?
Sasa si umesema unataka kuthibitishiwa kama Mungu yupo au lah.

Au unataka uthibitisho upi ?Kama unataka kumuona Mungu sema tukuoneshe yupo wapi.
 
ufahamu wako ndio umekwamia hapo. ni vigumu sana kuelewa.na kukubali sababu umeshajivisha akilini mwako kuwa hakuna MUNGU lakni wala hujui na huwezi/hutaweza kamwe kujitambua kuwa wewe Kiranga umefikajefikaje hapoulipo na ni nani aliyekuleta hapa duniani labda umejileta mwenyewe.
kama hutambui muumba wa mbingu na dunia basi unaweza kusema hata baba yako huna uhakika kama ni wa kwako kweli.
hayo unayoyapigia chapuo humu ndio yanayoendesha maisha ulimwenguni mazima. kabla hujazaliwa inamaana hukuwepo je umekujaje duniani.
NI KWA UWEZO WA MUNGU KAMLETA MAMAKO AKAKUTANA NA BABAKO WAKAUNGANA UKAWA MWILI MMOJA NA UKAZALIWA Karanga.
Umeelewa nilichoandika katika post uliyoinukuu hapo?
 
Sasa si umesema unataka kuthibitishiwa kama Mungu yupo au lah.

Au unataka uthibitisho upi ?Kama unataka kumuona Mungu sema tukuoneshe yupo wapi.
Kwani uthibitisho lazima kuona kinachothibitishwa?

Ushawahi kuiona namba moja? Siyo sehemu ilipoandikwa namba moja, namba moja yenyewe, ushawahi kuiona?
 
Mungu anweza kufanya lolote mahala popote na saa yoyote. Hachelewi wala hawahi, hivyo acha kumkashfu Mungu yeye ni yule jana, leo na hata milele habadiliki. Anaweza kufanya zaidi ya hayo unayo fikiri
 
Kama upi unaoutaka wewe?

Unaniuliza nataka uthibitisho gani.

Nakuambia wenye logical consistency na usio na contradiction, halafu unaniuliza kama upi.

Unauliza swali nililolijibu. Unalinukuu. Halafu unauliza swali hilo hilo.

Nina shaka sana kama tunaweza kufikia sehemu tukaelewana.

Mwisho utaniambia nithibitishe mwenyewe kwamba Mungu yupo, kwa niaba yako.
 
Hujajibu swali naona unajikanyaga kanyaga

Je mungu ni mwarabu?

Kwanini maneno ya mungu mpaka yaandikwe kwa kiarabu?

Muhamad hakujua lugha yoyote zaidi ya kiarabu ndio maana alitoa mafunzo ya kiarabu au wewe ulitaka atoe mafunfisho kwa lugha ipi?

Nijibu maswali hayo ukishindwa huna mamlaka ya kunilazimisha kuandika kiarabu wakati kutetea kama mungu mwarabu huwezi

"INNAMAL AMALU BI NII YAATI WA INNAMAA LIKULLI MRIII IM MANAWAA"

Kikubwa nia na dhamira ya mtu kiarabu ni lugha kama lugha nyingine kama mungu yupo usinipangie kutumia mafundisho yake mpaka kwa kiarabu alimtumia muhammad kwakuwa alikuwa mwarabu mm si mwarabu
Bro una matatizo sikufichi,wewe ni hujui halafu unajidai unajua,wewe ni wa kuachwa kwani unaingia katika kundi la WAPUMBAVU.

Umenukuu hadithi ambayo ukiisoma kwa maandishi yako unakosea,sehemu ya 'ayni unaweka hamzatul qatwi'i,sasa mtu kama wewe sina muda wa kupoteza na wewe,maana nikiendelea kujibizana na wewe kwanza sifaidiki chochote yaani sipati kitu cha kujifunza kutoka kwako,pili utazidi kupata madhambi tu.
 
Unaniuliza nataka uthibitisho gani.

Nakuambia wenye logical consistency na usio na contradiction, halafu unaniuliza kama upi.

Unauliza swali nililolijibu. Unalinukuu. Halafu unauliza swali hilo hilo.

Nina shaka sana kama tunaweza kufikia sehemu tukaelewana.

Mwisho utaniambia nithibitishe mwenyewe kwamba Mungu yupo, kwa niaba yako.
Logical Consistency kama ipi?
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ugomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwanini kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwanini anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATED THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
1. Kwanza ujue Mungu sio dictetor, ametuumba sio kama roboti, ila wenye utashi, uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi ya kumtii au kuto mtii, kuheshimu taratibu zake au la. Hata malaika wamepewa uamuzi wa kumtii au kuto mtii. Mungu hakumuumba Shetani, alimuumba Lucifer. LUCIFER aliamua kutotii taratibu za Mungu, na kutaka nae apewe heshima sawa na Mungu, na alidai kwa nini Mungu pekee ndo abudiwe..? hivyo Mungu ni Dictator. hapo ndipo matatizo yalipo anzia. unaweza ukajiuliza kwa nini Mungu asingemuangamiza punde tu Lucifer alipo asi..? Mungu angemuangamiza shetani, malaika na viumbe wengine wangelizani madai ya shetani yangelikua sahihi, na wasingeelewa madhara ya dhambi. Sasa malaika na viumbe wengine wanajua nini madhara ya dhambi, na mabaya mengi yametokea duniani kwa matokeo ya dhambi. ila walielewa zaidi madhara ya dhambi pale Mwana wa Mungu alipo mwaga damu kwa sababu ya dhambi, hapo ndipo walipo jua uzito na madhara ya dhambi.
2. Dhambi zimefanya utengano kati ya Mungu na mwanadamu, ila kabla ya hapo Adamu walikua wakionana Mungu kila mara
3. mafuriko wakati wa nuhu ni funzo tosha kutuonesha jinsi Mungu anavyo chukia dhambi. na ndivyo atakavyo angamiza dhambi pamoja na wale wanao ing'ang'ania.

NB. Matokeo yote mabaya yaliopo duniani ni matokeo ya maamuzi ya sio sahihi ya mwanadamu, yaani kutomtii Mungu, toka kipindi cha Adamu mzazi wetu wa kwanza. Lakini ipo siku yatakomeshwa yote na kufanywa yote kua mapya...
 
Kuambiwa unaweza kuambiwa uongo, kuona unaweza kuoneshwa hata movie ya Hollywood.

Nataka uthibitisho wenye logical consistency usio na contradiction.
Sasa bro mbona unajifanya hujui aisee. Hivi unataka kuniambia hujui madhaifu ya logic mpaka utake kuthibitishiwa kwa logic ?


Huwa nasema hivi nyinyi mmenyimwa misingi ndio maana hata utambuzi wa mambo hamna.
 
إذا كان الله يعاقبك فهو ربك و إذا كان يعفو لك فهو الرحمان

"Laa ikraah fii diyiin"[/QUOTE]



😁😁 wewe humuamini Mungu sasa hiyo "laa ikraha fii diin" wewe inakuhusu vipi?? au unayo dini yako na Mungo wako wa bandia minghair ya Allah??.
 
Mtoa maada uko vizuri sana hayo maswali yanatakiwa yaulizwe kweli sio mtuletee blabla.hata mimi ujinga staki kupelekwa pelekwa nimechoka.mungu ni nguvu sawa anaishi wapi?wataema popote hivyo mungu hana mwili wa nyama mungu ni hewa mungu upepo au mungu nini?huyo jamaaa maada aliyo toa inamashiko kwa wenye akili na ufahamu wa kutosha tu.
 
"Laa ikraah fii diyiin"



😁😁 wewe humuamini Mungu sasa hiyo "laa ikraha fii diin" wewe inakuhusu vipi?? au unayo dini yako na Mungo wako wa bandia minghair ya Allah??.[/QUOTE]

Inaonekana hujui maana dini nipe maana yake?

Halafu ndio utajua mimi nina dini au?
 
😁😁 wewe humuamini Mungu sasa hiyo "laa ikraha fii diin" wewe inakuhusu vipi?? au unayo dini yako na Mungo wako wa bandia minghair ya Allah??.

Inaonekana hujui maana dini nipe maana yake?

Halafu ndio utajua mimi nina dini au?[/QUOTE]



Dini= Religion =دين
 
Back
Top Bottom