Kwa hiyo una kataa uwepo wa Mungu kisa watu wanakufa?
Hujui kwamba nafsi zina sifa kuu/phases tatu ,ambao ni kuzaliwa ,kuishi na kufa, na lazima zipitie phases zote tatu.
Kufahamu hivyo unahitaji Mungu mkuu? Au kufahamu kuwa viumbe vinahitaji kuthaminiwa tunahitaji Mungu? Ndio maana ninasema Mungu ni ukomo wa kufikiri. Kwa nini kama tunafahamu kuwa kifo ni miongoni mwa hatua za msingi katika maisha, tunaingiza katika hili propaganda za Mungu kampenda zaidi? Mara mchungaji fulani anafufua na hicho kinakuwa miongoni mwa vigezo vya kujipatia wafuasi nyomi?
Yani kwa kuwa hakuna namna watu wanafahamu ni lini watakufa, basi mazingira kama haya ndio ati yanathibitisha kuwa kuna Mungu. Ilihali kwa sasa unakiri kuwa kifo ni sehemu ya hatua za kiumbe hai. Ni lazima afe. Ila kwa kuwa hstujui siku wala SAA, hapa ndipo Mungu anapoingia.
He, tukisema huyu Mungu ndiye anayesababisha hizi ajali kama za kuzama kwa kivuko, au ajali za ndege, magari, mabasi, aliweka magonjwa n.k utabisha? Je, huyu ndiye Mungu wa upendo au ndiye Mungu mkatili kuliko kitu chochote kile?
Tuache sasa kusimamia ukweli kuwa kivuko kuzama ni uzembe wa watu kwa kushindwa kusimamia taratibu na ukweli kuwa kilistahili kubeba watu mia tu? Ndio tuseme mipango ya Mungu haikiukwi? Alishapanga hivyo na ilipaswa kuwa hivyo? Elewa ninaposema Mungu ni ukomo wa kufikiri, unielewe basi. Ni kichaka cha kupata majibu mepesi kwenye maswali magumu.
Eti pale uwezo wa binadamu unapoishia, ndio Mungu anaanzia hapo. Kwamba, kadiri uwezo wetu unapoongezeka, kwa maana ya kupata ufumbuzi wa changamoto, basi tunasogeza mbele uwezo wa Mungu. Huoni uwezo wa Mungu ndio huo uwezo wa binadamu tu?
Kwanza ukichunguza kwa making utakuja kuona kuwa uwepo wa Mungu unategemea sana uwepo wa vitu na hususani vile ambavyo, katika wakati fulani binadamu amekosa majibu wa kwa nini vipo namna hiyo. Kimojawapo ni muda we kufa.
Vitu vingine ni mwanzo wa kila kiumbe, mwonekano wa kipekee wa vitu kama milima, water bodies. Kwa mfano pale bahari mbili zinapokutana. Yani ni muujiza, na hapo tunasema kweli mwache Mungu aitwe Mungu!