Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

Ikiwa watu wanazaliwa wakiwa wajinga, kosa ni la nani? Muumbaji, siyo? Kwa hivyo yeye ndiye atakuwa na ujinga kwa kushindwa kutumia uwezo wake kuumba watu werevu. Simple logic.
Kila mtu anazaliwa akiwa hajui kitu/mjinga.

Mazingira tunayoishi ,vyakula tunavyokula na elimu tunayoipata ndizo zinatufanya tujue vitu mbalimbali/tuondoe ujinga.
 
Nimeeleza kuwa uwepo wangu hapa umenifanya nijue kuwa kabla ya mimi kuwepo kuna vilivyokuwepo kabla ya uwepo wangu,hivyo uwepo wangu umefanya nijue kuwa kuna vilivyokuwepo kabla yangu na si kwamba uwepo wangu ndiyo umesababisha kuwepo hivyo vitu. Kwahiyo hauwezi kusema Mungu hayupo kiukweli basi hata haya maisha pia hayapo kiukweli na hivyo haina haja ya kuyathamini.
Msijipe tabu sana huyo Otolung'anyi ndio Kiranga mwenyewe ameona anaanza kushindwa akaamua kuja kwa ID nyingine ili akwepe aibu.
 
Hakuna anayekataa haya usemayo. Ila, namna watu wanavyotumia dhana ya Mungu ndio kuna shida kubwa. Ni utumwa mtakatifu.
Sasa na wewe hauoni kuwa unajipumbaza kwa kusema hakuna Mungu kisa tu kuna watu wanatumia vibaya imani ya uwepo wa Mungu?
 
Umesema kwanza awali uthibitisho lazima uweze kupimika,lakini hujasema ni ipi mizani ya kuipima hiyo ithibati.
Nimeendelea kuitaja mizani hiyo kama logical consistency, kutokuwa na contradiction, kuweza kutabiri vitu.

Sema hujaweza kusoma tu.
 
nimethinkiiiiii nimegundua kuwakweli Mungu yupo na ili ujue Mungu yupo jiulize wewe umekujaje duniani amekuleta nani? ukishajua haya ndo uendelee kufikiria mengineyo
That is a priori logical non sequitur
 
Nimeendelea kuitaja mizani hiyo kama logical consistency, kutokuwa na contradiction, kuweza kutabiri vitu.

Sema hujaweza kusoma tu.
Inaonekana hujui nini maana ya mizani,mizani ya kielimu ni kule ambako tunarejea kuupata ukweli au muafaka.

Hali ya kutokuwa na utata au tatizi haiwezi kuwa mizani sababu hali hiyo inajadiliwa.

Soma mizani niliyokutajia mimi,kisha ufikirie katika hali halisi....!
 
Kaka mkubwa naelekea katika ile safari niliyokuwa naisubiri kwa hamu sana. Safari ya kuonyesha haki iko wapi na kina nani wenye haki.

Naanzia hapa :

Wewe unawezaje kuthibitisha kutokuwepo kwa Mola kutokana na vigezo vyako hivyo ? Hapa chini nakueletea uthibitisho wa haki na vigezo vya ithibati.

Vigezo au vijenzi vya ithibati.

1. Katika kuthibitisha jambo kwanza lazima ujue nini unachotakiwa kukithibitisha. Je jambo husika linaweza kuthibitishwa au kinyume chake ?

2. Lazima ujue ni wapi ithibati ilipo,yaani kwa lile ukusudialo kulithibitisha lazima ujue wapi utapata ithibati.

3. Lazima uwe na elimu ya kile unachotakiwa kukithibitisha.

4. Ni yapi maegemeo yako katika ithibati zako,je unatumia hoja za kihisia,hoja za kiakili au unatumia nukuu za ki ufunuo ?

Mizani au vipimo vya Ithibati

Nakuja..............!
Hujaweza kuthibitisha Mungu yupo kw njia iliyo na logical consistency.

Habari zako za Mungu kuwepo zina contradiction.

Hapa mnatuambia Mungu yupo, ana ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote, ana haki kuu.

Pale mnatuambia kaleta gharika ya mafuriko imeua kuanzia vitoto vichanga visivyojua alif wala be, mpaka vinyama visivyo na akili ya kujua mazuri na mabaya.

Huyo Mungu yupo kweli au tunapigana kamba tu?
 
Nimeendelea kuitaja mizani hiyo kama logical consistency, kutokuwa na contradiction, kuweza kutabiri vitu.

Sema hujaweza kusoma tu.
Umezungumzia kitabiri,suala la kitabiri nje ya ufunuo linabaki ni jambo la kubahatisha. Kwanini tubahatishe katika suala ambalo halihitajo kubahatisha ?
 
Hapa naendelea pale nilipoishia.

Vipimo vya ushahidi / uthibitisho /Ithibati.

1. Nafsi

Hiki ni kipimo madhubuti na chenye nguvu sana katika katika kuhakiki ukweli wa mambo jinsi ulivyo. Naposema nafsi ni kile kinachotafutiwa uthibitisho kinasemaje au kinajielezeaje. Hapa nakupa mfano. Kwa mfano wewe kiranga unajijua zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Kwahiyo nikitaka kumjua Kiranga kwa uhalisia wake,lazima nikuulize wewe mwenyewe kisha wafate wale wanao kujua.

Mathalani sisi tunao muamini Mola muumba tunapata ushahidi wa uwepo wake kwanza kutokana na yeye alovyojipambanua kwetu sisi kupitia wateule wake ambao ni mitume na manabii.

Sasa swali linakuja kwako wewe,unathibitishaje kutokuwepo kwake kinyume kwake kwa kutumia hisia na akili tu ? Akili ambayo ni dhaifu na hisia ambazo si kamilifu ?

2. Maumbile

Naendelea......
Nafsi ni nini? Unaweza kuthibitisha ipo?

Maumbile yanathibitishaje Mungu yupo? Kama Mungu yupo, mbona kuna watu wasio na hatia awanazaliwa vilema, vichaa, vipofu etc?
 
Hujaweza kuthibitisha Mungu yupo kw njia iliyo na logical consistency.

Habari zako za Mungu kuwepo zina contradiction.

Hapa mnatuambia Mungu yupo, ana ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote, ana haki kuu.

Pale mnatuambia kaleta gharika ya mafuriko imeua kuanzia vitoto vichanga visivyojua alif wala be, mpaka vinyama visivyo na akili ya kujua mazuri na mabaya.

Huyo Mungu yupo kweli au tunapigana kamba tu?
Kushindwa kupata jibu moja katika hoja mbili za kufanana ni uchache wa elimu.
 
Nafsi ni nini? Unaweza kuthibitisha ipo?

Maumbile yanathibitishaje Mungu yupo? Kama Mungu yupo, mbona kuna watu wasio na hatia awanazaliwa vilema, vichaa, vipofu etc?
Huyu kuzaliwa kilema na huyu kuzaliwa vile,ana onyesha ukamilifu na ubora wake katika uumbaji.

Kila nafsi itaonja umauti. Kwa kauli hii kama wewe huwa unafikiri kiundani utajua nini maana ya nafsi.

Maumbile yanathibitisha uwepo wa Mola sababu hayakwepo kabla ya kuwepo kwake. Kwa maana yuko ambaye ni chanzo cha hayo. Na chanzo chenyewe hakina baada yake.

Kuna post nilitolea mfano wa seti A na Universal set U unaweza kurejea ili ufaidike zaidi.
 
Tuanzie hapa, umesema "Mungu wa haki asingeumba hivyo" mpaka hapa umeonesha kwamba kuna Mungu wa haki yupo ila huyu tunayemuabudu sisi si wa haki, tuambie sasa huyu wa haki unayemjua wewe ana sifa zipi ?
Wwewe jifunze kusoma kwanza, tafuta mwalimu wa logic akufundishe truth table ni nini, p ni nini, negation ya p ni nini, tautology ni nini, contradiction ni nini, fallacy ni nini.

Halafu ni jinsi gani unaweza kuivunja sentensi ukaipitisha katika truth table.

Halafu, ukimaliza somo hilo, njoo tujadiliane tena hapa.

Kwa sasa naona naweza kubishana na ngumbaru asiyejua kusoma.

Pata darasa la bure hapa kuhusu Truth Table, Boolean Aalgebra, Venn Diagram etc

Inaonekana hujui nini maana ya mizani,mizani ya kielimu ni kule ambako tunarejea kuupata ukweli au muafaka.

Hali ya kutokuwa na utata au tatizi haiwezi kuwa mizani sababu hali hiyo inajadiliwa.

Soma mizani niliyokutajia mimi,kisha ufikirie katika hali halisi....!
Huwezi kuwa na mizani kama unakubali contradiction.

Utapimaje wapi kumezidi wapi wakati kulikozidi kunaweza kuzidiwa na kulikozidiwa?

Kama unakubali contradiction, kilo 50 zinaweza kuwa nzito zaidi ya kilo 100.

Sasa hapo utapimaje uzito kujua wapi kuna uzito zaidi?
 
Wwewe jifunze kusoma kwanza, tafuta mwalimu wa logic akufundishe truth table ni nini, p ni nini, negation ya p ni nini, tautology ni nini, contradiction ni nini, fallacy ni nini.

Halafu ni jinsi gani unaweza kuivunja sentensi ukaipitisha katika truth table.

Halafu, ukimaliza somo hilo, njoo tujadiliane tena hapa.

Kwa sasa naona naweza kubishana na ngumbaru asiyejua kusoma.

Pata darasa la bure hapa kuhusu Truth Table, Boolean Aalgebra, Venn Diagram etc

Hakuna mtu asiyejua Logic na mambo ya Truth Table, hata mtoto wa O Lev aliyesoma Additional Mathematics anaijua.
 
Back
Top Bottom