Oltung'anyi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 284
- 197
Ni ukomo wa kufikiri kwa sababu tunaona changamoto tunazokutana nazo zinatatuliwa kirahisi mno na imani ya Mungu. Mtu anaumwa Ukimwi, badala ya kutumia sawa, anatumia maombi. Mtu anahitaji kuongezewa damu anakataa akiamini atapona.Unasema msingi wa dhana ya Mungu ni ukomo wetu wa kufikiri.
Una maanisha nini unaposema ukomo wetu wa kufikiri?
Uzembe wa kujaza kivuko kupitia kiasi kukapelekea watu kupoteza maisha, tunasema ni mipango ya Mungu. Huoni kuwa tumeamua kuacha kutumia akili na tumejipa majibu rahisi ambayo kimsingi hayana maana yoyote? Huoni tupo utumwani ndugu?
Unafikiri ni kwa nini tumepewa utashi? Tukariri tu maandiko na kuyatumia kama yalivyo? Hatuhoji! Huyo Mungu kama alitupa akili, ya kasi gani? Kwa mini tunafurahia teknolojia za simu au magari kwa mfano lakini linapokuja suala LA kuongezewa damu kama sehemu ya Tina iwe imani inakataza?
Muulize ndugu anayesema wanaomkataa Mungu hawana akili, haya wanayoyafanya ndio akili with these double standards?