Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,568
Katibu wa Itikadi , Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda leo Januari 19, 2024 ameahidi kukabidhi katapira 20 kwa mbunge wa jimbo la Kawe, Josephat Gwajima kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa barabara.
Makonda ametoa ahadi hiyo kutokana na wananchi wa jimbo hilo kulalamikia ubovu wa barabara, huku akiagiza katapila hizo zianze kazi mapema wiki inayokuja.
Sambamba na hilo, Makonda amempa maagizo Waziri wa Ardhi, Jerry Slaa kufika Bunju leo hii ili kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi katika eneo hilo.
Hii ni awamu ya pili ya ziara yake kitaifa ambapo anaangazia kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Pia Soma:
- DOKEZO - Ni aibu Kawe - Dar kuwa na Kituo cha Daladala cha hali hii. Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mbunge wajitafakari
My Take:
Barabara na Kituo cha Kawe zimekuwa zikilalamikiwa miaka yote lakini sioni jitihada zozote zilizofanywa na na Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima. Au ndiyo mambo ya Uchaguzi?