DOKEZO Ni aibu Kawe - Dar kuwa na Kituo cha Daladala cha hali hii. Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mbunge wajitafakari

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Anonymous

Senior Member
Feb 3, 2006
125
321
Kawe ni moja ya Kata zilizopo ndani ya Wilaya ya Kinondoni na katika Jimbo la Kawe ikiwa ni moja ya Kata maarufu sana lakini hali ya Kituo cha daladala katika Kata hiyo inahuzunisha sana.

photo_4_2024-01-15_14-14-03.jpg
photo_6_2024-01-15_14-14-04.jpg
photo_8_2024-01-15_14-14-04.jpg
photo_14_2024-01-15_14-14-04.jpg


Kituo hicho kilichopo Tanganyika Packers kina magari ya kwenda Segerea, Bunju, Mbezi, Mloganzila.

Kawe haijawahi kuwa na Kituo kizuri cha Daladala kwa muda mrefu sana. Awali Daladala zilikuwa zikitumia eneo la Ukwamani ambalo halikuwa Kituo rasmi kwasababu Magari yalikuwa yanaegeshwa Barabarani tu.

Baadaye Daladala zikahamishiwa Tanganyika Packers sehemu ambapo kuna eneo kubwa, lakini cha kushangaza bado Kituo hicho kimefinywa eneo huku kikiwa na miundombinu mibovu, isiyo salama na ya kufedhehesha.

Nakumbuka baada ya kuhamishia magari katika Kituo hicho, waligawanya magari tena. Kwamba yanayotumia route ya barabara ya Mwai Kibaki yalirudishwa Ukwamani na yanayotumia route ya barabara ya New Bagamoyo yakabaki Tanganyika packers.

Ni jambo jema kusaidia Wananchi lakini kupunguza magari ili kupunguza ukubwa wa Kituo ni jambo la kushangaza sana la linaonesha ufinyu wa kufikiria wa Viongozi.

Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima; Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila (na Waliopita) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule wanatakiwa kuona aibu sana kwa Kawe kuwa na Stendi ya namna hii huku mapato yakikusanywa kila Uchwao.

photo_3_2024-01-15_14-14-03.jpg
photo_9_2024-01-15_14-14-04.jpg
photo_13_2024-01-15_14-14-04.jpg


Kituo magari kupishana tu inakuwa shida wakati huo huo kuna wafanyabiashara pembezoni kabisa wa Kituo ambao wangeweza kusogezwa.

Tena hawa wafanyabiashara waliwahamishwa kipindi Fulani, kipindi cha kuondoa Wanachinga nae neo lilikuwa safi lakini kwa sasa wamerudi kwa kasi na hadi kazi za upishi wa chakula zinafanyika kwenye maeneo hayo ya kituo yaliyojaa matope, matakataka na maji machafu jambo linalihatarisha Maisha ya watu kwa kiwango kikubwa sana.

Nyuma ya wafanyabiashara hawa kuna eneo kubwa (huenda linamilikiwa na NHC) lakini lingeweza kutumika na kujenga kituo cha daladala bora kabisa na cha kisasa lakini kwa kuwa Viongozi wanaona Wananchi sio kitu hawajawahi hata kujaribu kuwajengewa Wakazi wa Kawe Kituo bora na cha Kisasa cha Daladala

photo_10_2024-01-15_14-14-04.jpg
photo_12_2024-01-15_14-14-04.jpg
photo_16_2024-01-15_14-14-04.jpg
photo_17_2024-01-15_14-14-04.jpg


Soma Makonda kutoa Katapila 20 kusaidia kurekebisha barabara za Jimbo la Kawe
 
Kituo Cha haja gani wakati wananchi wanasubiri kuperekwa Birmingham kula Bata...ya nini wateseke na daladala. Kwangu sioni haja ya stendi wana kawe muda umefikia wa kuondoka,andaeni nguo mpasi vizuri ni muda wenu Sasa..Askofu Gwaji boi hajawai kusema uongo ..hata Ile Xxx alisema ni ya bonsa.
 
Back
Top Bottom