Makete mbabe wa baridi Tanzania nzima

Makete mbabe wa baridi Tanzania nzima

Hi ni asubuhi ya makete. Just imagine mwanao anaenda shule hapo.
IMG-20180820-WA0047.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubali, Nimekaa Uwanji pale kwa wiki mbili, nilikua naichakaza ile milima nafika hadi kwenye Escarpment naiona Igurusi na Usangu basin zile.Pamoja hio kazi ngumu ila kulala na Female ilikua lazima anisaidie kupambana na baridi.UWANJI SALUTE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Mufindi sijafika japo nimepita sana Mafinga nahisi panafanana sana kwa hali ya hewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna sehemu inaitwa Mwakaleli -Tukuyu huko balaa mwezi wa sita miaka ya1985 Tulikuwa tunaingia Darasani saa tatu, kuogamara moja kwa weekmbili. Ukitaka wanafunzi wafeli waulize maswali kama vile, mbu ni nini? Friji ni? Maralia ni nini? Watakujibu hatuwafahamu.
 
Hii nay
Makete ya enzi hizo barabara masika usafiri unasimama yaani hakuna kusafiri kutokana na barabara mbovu siku basi likakwama siku7 na kuziba barabara yote basi kuna mzungu alikuwa anasafiri na Land cruiser hardtop mpya mbele ina ile winch na kaishaambiwa kuwa basi limekwama sehemu Fulani akasema nitapita,kufika eneo la tukio kakuta basi limejaa njia nzima akawaambia fungeni Winch wakafunga na kuanza kulivuta.Dadeki land cruiser inavuta scania bus kubwa akatia gia zake 4WD ngoma hata kutikisika hamna ile hamad mzungu kaunguza clutch ikabidi nae akae aagizie mpya mjini ilipofika kesho yake ikabidi akubali matokeo na kurudi nyumbani sasa sijui tiketi ya ndege alifanyaje maana alikuwa anaenda kwao Mara moja
Hiyo ndo makete

Sent using Jamii Forums mobile app
mwikale mwibhute
 
Mkuu ningesema mi peke yangu ningeonekana nanogesha Uzi.
Miaka ya 94 nilipokuwa primary 95% ya watoto walikuwa wanapenda shule peku na barabara zina kokoto basi unamkuta dogo anaona bora atembee kwenye nyasi zenye barafu kuliko kokoro.Dah wengine leo hii nikiwaangaliaga huwa nafurahi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee hiyo ya Kokoto umenikumbusha mbali sana maana hata Mie ni mhanga wa hilo nashukuru Mungu Wakati nimefika Darasa la tano kulikuwa na mashindano ya Hifadhi Mazingira (HIMA/DANIDA) ndo tulinunuliwa viatu,toka hapo ilikuwa lazima Kila mtu avae kiatu.
Kitu Kokoto we acha kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapajua punga kwenye mashamba ya Chai ya mo dewji....utawaona wamama wanavyo piga mwendo pale wa kazi wanatoka umbali wa km 5 kwenda kazini hapo shambani na kurudi.......wale ndy wanawake wa Shoka malkia wa nguvu syo malkia wa nguvu wa clouds

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Wababa wana kuwa wapi wamama wakipiga mzigo?
 
Huko ni balaa! Ukilala nje na nguo nyepesi asubuhi tutaokota maiti.
 
Kule mkuu nyumba ya mwenye uwezo lazima aweke Dohani lile jiko la kuotea moto sebuleni then moshi unatokea juu yaani tulikuwa tunakata vigogo vya miti inaitwa miwati(wattle trees)ndo tunakoka ndani mnakuwa na moto.Yaani kama ulaya vile

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilisoma mahali, kutokana na uhaba wa ardhi Ulaya nyumba nimejengwa kwenye mstari. Miaka ya 1950 mpaka 60 walitumia kuni kuleta joto kwenye nyumba. Mitaa ilifuka moshi ukitanda na misitu ilitokomea.

Ndipo walipokuja na wazo la kusambaza mabomba ya gas kwenye nyumba na kuwekeza central heating system majumbani.
 
A,alleykum

Wadau katika maeneo yoote nilikwisha kutembelea katika nchi hii,nimejiridhisha kuwa wilaya ya MAKETE iliyoko mkoani Njombe ndio sehemu yenye baridi zaidi nchini Tanzania.

Hebu na ww tuambie ni sehemu gani unahisi ina baridi kushinda wilaya hii ya maker.

Hebu tazama hii ni hali ya kawaida katika wilaya hii kuanzia mwezi Juni-Agosti kukuta nyasi zote zimefunikwa na barafu na jua likishakolea na barafu kuyeyuka basi nyasi huonekana kama zimeungua.

Sincerely, Bachelor Sugu.View attachment 845768

Sent using Jamii Forums mobile app
Unazungumzia Baridi au UKIMWI?
 
Back
Top Bottom