Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,018
- 144,377
Raisi Samia, japo umetukwaza sana na hii issue ya bandari, kuna mambo mazuri umefanya hasa katika kurekebisha baadhi ya mambo yaliyofanyika wakati wa utawala Marehemu Magufuli. Moja ya eneo ulilogusa ni kuboresha masilahi ya wafanyakazi kama kupandisha watumishi vyeo, kuongeza mishahara ingawa ni kwa kiwango kidogo na sasa ahadi ya kurudisha annual increments kwenye mishahara ya wafanyakazi kila mwaka.
Hata hiyo, kuna jambo moja muhimu na linagusa sana wafanyakazi(linaumiza) na hili si lingine bali ni uamuzi wa serikali ya awamu iliyopita kuongeza makato ya kulipia deni la Bodi ya Mikopo(HESLB), kutoka asilimia 8 mpaka asilimia 15 bila kujali mkataba wanufaika walioingia wakati wa kuomba mkopo(kukatwa asilimia 8), na pia makato haya kutozingatia sheria inayotaka Mfanyakazi abaki walau na moja ya tatu(theluthi moja) ya mshara ghafi wake(basic salary) baada ya makato yote ya lazima na mengineo kama mikopo ya mabenki n.k.
Kwa bahati mbaya, hata kama mtumishi ameshafikia ukomo wa hiyo moja ya tatu kwenye take home yake, makato ya HELSB hayazingatii hii sheria bali wanakata tu na matokeo yake mtumishi anabaki na take home iliyo chini ya moja ya tatu ya basic salary yake huku mishahara yenyewe ikiwa ni duni kabisa kwa wafanyakazi wengi wa nchi hii hasa wa serikali na pia hata wale wa sekta binafsi.
Kumbekuni hata CAG aliepita, aliwahi pinga haya makato na akatamka kabisa kuwa yanavunja sheria.
Binafsi sio muumini sana wa hii sheria ya kulazimisha mtumishi abaki na moja ya tatu kwasababu ina mapungufu mengi(niliwahi andika kuhusu haya mapungufu siku za nyuma) na pia sheria hii haikufanyiwa utafiti wa kutosha, ila kwakuwa serikali yenyewe sasa ndio kinara wa kuivunja, basi hii inangeza sababu ya kuona ni bora tu sheria hii ifufutwe kabisa au ifanyiwe marekebisho.
Mtumishi akitaka kukopa, anabanwa na hii sheria, ila ukidaiwa na Bodi ya Mikopo, sheria haizingatiwi wanakata tu. Hii sio sawa kabisa na ni bora hii sheria ifutwe ijulikane moja.
Kuongoza ni kuonyesha njia.
Talk the talk and walk the walk.

CAG: Makato ya Bodi ya Mikopo toka 8% - 15% yanakiuka Sheria; kuna watumishi wanateseka na makato makubwa
Jumla ya makato ya kila mwezi kwangu ni PAYE = 19% na point kidogo HESLB = 15% NHIF = 3% hifadhi za jamii = 10% Trade union = 2% Jumla: 49% Mbaya zaidi kila kitu kinakatwa kwenye gross. Narudi nyumbani na less than 51% (benki nao wanamakato yao ya ajabu ajabu) Better werw colonial days!
www.jamiiforums.com