Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Katika mishahara ya watumishi wa umma, kuna makato ya lazima ambayo ni PAYE, Bima ya Afya, Makato ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii na makato mengine ya kujiunga kwa hiari kama ya vyama vya wafanyakazi, nk.
Nachojiuliza, ni sahihi mshahara unapopanda na makato haya kupanda automatically?
kwa maneno mengine, mshahara wa mtumishi unapopanda kwa mtumishin kupandishewa cheo au serikali inapoongeza mshahara, gharama za kuendesha mfuko wa Bima ya Afya au taasisii kama vya wafanyakazi nazo zinaongezeka?
Binafsi nafikiri wakati umefika utaratibu huu wa kukata mishahara kwa asilimia ya mshahara ghafi(basic salary), utazamwe upya na kuwe na restrictions fulani na sio makato kuongezeka automatically kila mshara wa mtumishi unapopanda kwani kwa kufanya hivi, kuna muathiri mtumishi kama ambavyo anaathirika na kupanda kwa bei ya unga, mkate, mafuta, nk.
Makato pekee ambayo naona yanafaa kupanda automatically kila mshahara unapoongezeka, ni labda PAYE tu ili kuiongezea serikali uwezo wa kulipa hiyo mishahara ingawa PAYE nayo teyari iko juu mno katika nchi yetu.
Hakuna uhusiano wowote wa kuongezeka kwa mshara kwa mfanyakazi na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa Vyama vya Wafanyakazi, Mifuko ya Hifadhi ya jamii, Bima ya Afya n.k, na tukumbuke mifuko ya hifadhi ya Jamii imekuwa ikijidendesha kibiashara kwa kufanya uwekezaji ingawa kuna kasoro zimejitokeza na kuathiri mifuko hii na kusababisha iunganishwe lakini ilikuwa inatengeneza fedha na hivyo kuondoa ulazima wa kuongeza makato yanayokwenda katika mifuko hii kila mara mishahara inapoongezwa.
Mifuko na taasi hizi zinapohitaji kuongezewa makusanyo kutoka kwenye makato ya wafanyakazi, ziwe zinapeleka maombi serikalini kama ambavyo TANESCO wanatakiwa kupeleka maombi ya kupandisha bei ya umeme EWURA kabla ya kupandisha bei hizo na si kwa kutumia huu utaratibu unaotumika hivi sasa.
Uholela au kukosekana kwa udhibiti katika makato ya wafanyakazi, kuna changia sana kufanya mishahara duni ya watumishi wa umma kuwa duni zaidi na pia ni matokeo ya watu kuongezewa shilingi 3000/= na wengine shilingi 12,000/= katika take home yao kama ilivyotokea mwezi July mwaka huu.