Makapuku Forum

Makapuku Forum

Awamu hii, kama vile zilizotangulia, nayo itapita na maisha yataendelea. By the way, mkuu mwenyewe alishasema kuwa watu wafyatue tu kwa sababu watoto watasoma bure
Kila jambo na wakati wake

MHUBIRI 3

1.Kwakila jambo kuna majira yake,Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

2.Wakati wa kuzaliwa,na wakati wa kufa,wakati wa kupanda na wakati wa kung'oa yaliyopandwa.

3.Wakati wa kuua ,na wakati wa kupoza Wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga.

4.Wakati wakulia na wakati wa kucheka,wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza.

5.Wakati wa kutupa mawe nawakati wa kukusanya mawe,Wakati wa kukumbatia na wakati wa kutokumbatia.

6.Wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza,Wakati wa kuweka na wakati wa kutupa.

7.Wakati wa kurarua na wakati wa kushona;Wakati wa kunyamaza na wakati wa kunena.

8.Wakati wa kupenda na wakati wa kukuchukia;Wakati wa vita na wakati wa amani

9.Je!Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo?

Hakika hiyo ndiyo kanuni ya maisha mkuu,tukiijua na kuifuata ,hatutapata shida.

Kila jambo na wakati wake na majira yake.
 
Muziki sio Ajali

Habari za mapumziko ya usiku huu Makapuku wenzangu, ninajua tumekuwa na mwanzo mzuri wa wiki na wale wote ambao tumekutwa na ya kukutwa, basi kesho ni siku nyingine na jua litawaka tena. Kipindi cha pili tunaweza kusaidiwa na upepo, tusichoke.

Turudi tena kwenye muziki na hasa kuangalia udonoaji wa gitaa bila kujali ni gitaa la kawaida au la umeme ilmradi lina nyuzi 12, au 6 au 4 sisi tutalifurahia katika muziki.

Kwa mnaofunga Ramadhani, mnatenda haki na kwa wasiofunga wanatenda haki pia. Ndiyo maisha na kupanga ni kuchagua.

Gitaa. wikend ya jana Sweetiepie alileta wimbo uliopigwa na The Mountain band, wimbo wa reggae na nikasema nitareta orijino version yake iliyopigwa na kuimbwa na Peter Frampton. 'Baby I Love Your Way ndo jina la wimbo na aliucheza miaka ya kati 1970s.

Pamoja na kupigwa miaka hiyo, wimbo na mipigo haikubadilishwa sana maana Peter aliutengeneza kuishi wakati wote hata ukirudiwa.

Japo alipiga gitaa la nyuzi sita, lakiini Peter katika wimbo 'bebi i lavu yua wai' alijikita katika kugusa nyuzi nne tu za mwanzo na hakujisumbua sana na nyuzi mbili za juu ambazo huwa zina kijibass cha kishikaji

Mcheki hapa katika clip ya YouTube uone 'tenor' na sauti zinavyoendana..


Asante sana One ubarikiwe wimbo mzuri sana

Sent from my itel it1406 using JamiiForums mobile app
 
THE LITTLE MAGIC ANGEL

Sehemu ya 2

Ilipoishia
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.



.
.
Kwakua Chief commander anajua anapambana na kiumbe asichokijua na kwa taarifa alizozipata nikwamba kimedondoka kutoka juu aliwaza labda anaweza kuwa alien au kiumbe cha aina gani alitumia ujuzi wa kijeshi kwa kujaribu kuwaambia wanajeshi wake wazime tochi pia wakae kimya inamaana alitaka kujua hicho kiumbe je kinaona?? Je kinasikia?? Na mashambulizi kinatumia siraha gani........ hayo yalikuwa ni mawazo yake chief commander Mcclaw

Je nikiumbe gani icho???

Story inaturudisha nyuma kabisa takribani miaka 120 iliyopita ndani ya nchi Nevada hapo zamani ilikuwa ni Nevada lakini kwakua kuna uvutano ndani wa pande mbili ikagawanyika ikawa Paradise na North nevada

Hapo ni baada ya mfalme wa Paradise nevada kutaka kumiliki miliki kubwa yaani kuongeza mapana ya utawala wake ndipo akaamua kukusanya jeshi la vijana hili kumsaidia kutimiza adhima yake

Hivyo ilimlazimu kukodi wanajeshi na kuingia mitaani kutafuta vijana wenye nguvu na kuwaingiza katika kikosi chake kwaajili ya mazoezi kwa ufupi alitaka kuifanya nevada iwe yake yote

Mwaka 1890 America ndo lilikuwa bara lenye nguvu zaidi kuwahi kutokea duniani ivyo kuweza kujitawala yenyewe na kuitawala dunia

Mfalme wa paradise nevada aitwaye Lucas Angelique alifanikiwa kukusanya vijana 6300 ndani ya wiki moja na kujenga jeshi kubwa kiasi ambacho alitamani hata kutaka kuitawala marekani nzima

Mwaka 1910 Mfalme huyo alikuja kuangushwa na waziri wake aitwaye Samuel viel kwa kupigwa Lisasi ya ubavuni wakati alikuwa akihutubia hali iliyompelekea kuwa mgonjwa na kushindwa kuendelea na vita dhidi ya mfalme wa North Nevada hivyo madaraka ya Lucas Angelique kuyashika samuel viel alikuwa ni mjerumani,kama unavyojua wajerumani kwa roho mbaya


Samuel viel
Mfalme aliyeitikisa marekani pamoja na dunia nzima ni baada ya kupata madaraka ya mapinduzi aliyoyafanya,anaanza kwa kufanya ukatili kueneza udini,ubaguzi na Ukilitimba.

Alikiwa akiua watu bila hatia kosa kwake ni hakuna msamaha anakuua kikatili kwa mkono wake yeye mwenyewe

Hali iliyofanya wananchi wamchukie na wamwogope hivo kupanga njama za kumuua kumuulia mbali

Baada ya kuona usalama wake umekuwa mdogo kiasi cha kupoteza maisha yake aliamua kuongeza wanajeshi ambapo ilifikia idadi 11,000 hapo akajilizisha kwamba yuko salama na ndo lilikuwa jeshi kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani na lenye ukatili wa hali juu zaidi


Hiyo ilimfanya mfalme Samuel Viel kuwa mfalme mwenye nguvu sana duniani kote
Hali hiyo ilipelekea mfalme wa North Nevada aitwaye Jacob d.c kuogopa alijua fika vita kati yake na Sam haiwezi


Jacob d.c
Alikuwa ni mfalme pekee aliye rithi mikoba ya babaake Michael d.c ndani ya miliki yake kuna dhahabu,almasi,rubby na madini mengine mengi sana kiufupi King
Jacob alikuwa ni tajiri kuliko King sam

Ulinzi aliokuwa nao pamoja na jeshi zima ni takribani 1200 ndicho kilicho mfanya haone nikama ameshindwa vita alisahau kuwa (it doesn't matter the size of the weapon but furry of attacks)

"Yaani haijalishi ukubwa wa siraha katika vita hila kwa uwezo wa mapambano"

Ndani ya miaka kumi paradise nevada ilikuwa ndo nchi pekee yenye mabavu ya dunia nzima kifupi ilikuwa ikitawala kwakila kitu miongo ikaenda mpaka sasa ndo nchi pekee yenye kupewa kipaumbele zaidi ndani ya bara la America kwaiyo majeshi au wazamizi wakipanga kuiangamiza dunia lazima waanze na taifa kubwa kama America

Tukutane sehemu ya 3 tujue nini kiliendelea pale Miam7i Beech
Asante

Sent from my itel it1406 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu..

Naleta ombi kwenu..

Nilikuwa nataka nimpe mtu jukumu la NUKUU YA LEO.

Nilichukua hii segment from April, lakini nahisi nashindwa kuifanyia kazi ..nashindwa kudeliver hiki kitu kwa members hapa kutokana na Ratiba zangu kubadilika kidogo na ndio sababu haka kuingia humu nasua sua kidogo..

Ile segment ni nzuri sana, sikupenda tuikose kwa kweli..

So natoa nafasi kwa member ambaye anaweza kunisaidia aendelee nayo...siku akiwa yuko tight maybe i can take over for sometimes again..

Ni wazo tuu lakini .
Pole sana na majukumu

Sent from my itel it1406 using JamiiForums mobile app
 
Kila jambo na wakati wake

MHUBIRI 3

1.Kwakila jambo kuna majira yake,Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

2.Wakati wa kuzaliwa,na wakati wa kufa,wakati wa kupanda na wakati wa kung'oa yaliyopandwa.

3.Wakati wa kuua ,na wakati wa kupoza Wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga.

4.Wakati wakulia na wakati wa kucheka,wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza.

5.Wakati wa kutupa mawe nawakati wa kukusanya mawe,Wakati wa kukubatia na wakati wa kutokumbatia.

6.Wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza,Wakati wa kuweka na wakati wa kutupa.

7.Wakati wa kurarua na wakati wa kushona;Wakati wa kunyamaza na wakati wa kunena.

8.Wakati wa kupenda na wakati wa kukuchukia;Wakati wa vita na wakati wa amani

9.Je!Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo?

Hakika hiyo ndiyo kanuni ya maisha mkuu,tukiijua na kuifuata ,hatutapata shida.

Kila jambo na wakati wake na majira yake.
Mhubiri. Kitabu kimojawapo kizito sana katika Biblia. Mfalme Suleman mpaka anatisha aisee. Nadhani alikiandika uzeeni mwishoni mwa maisha yake. Baada ya kuwa Bill Gates wa dunia ya wakati ule, kuoa wanawake 700 na masuria 300; pamoja na kuponda raha za kila aina katika Mhubiri anahitimisha kuwa bila kumcha Bwana na kuzishika njia zake, yote haya ni UBATILI mtupu na kujilisha upepo. Hakukosea!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom