THE LITTLE MAGIC ANGEL
Sehemu ya 2
Ilipoishia
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Kwakua Chief commander anajua anapambana na kiumbe asichokijua na kwa taarifa alizozipata nikwamba kimedondoka kutoka juu aliwaza labda anaweza kuwa alien au kiumbe cha aina gani alitumia ujuzi wa kijeshi kwa kujaribu kuwaambia wanajeshi wake wazime tochi pia wakae kimya inamaana alitaka kujua hicho kiumbe je kinaona?? Je kinasikia?? Na mashambulizi kinatumia siraha gani........ hayo yalikuwa ni mawazo yake chief commander Mcclaw
Je nikiumbe gani icho???
Story inaturudisha nyuma kabisa takribani miaka 120 iliyopita ndani ya nchi Nevada hapo zamani ilikuwa ni Nevada lakini kwakua kuna uvutano ndani wa pande mbili ikagawanyika ikawa Paradise na North nevada
Hapo ni baada ya mfalme wa Paradise nevada kutaka kumiliki miliki kubwa yaani kuongeza mapana ya utawala wake ndipo akaamua kukusanya jeshi la vijana hili kumsaidia kutimiza adhima yake
Hivyo ilimlazimu kukodi wanajeshi na kuingia mitaani kutafuta vijana wenye nguvu na kuwaingiza katika kikosi chake kwaajili ya mazoezi kwa ufupi alitaka kuifanya nevada iwe yake yote
Mwaka 1890 America ndo lilikuwa bara lenye nguvu zaidi kuwahi kutokea duniani ivyo kuweza kujitawala yenyewe na kuitawala dunia
Mfalme wa paradise nevada aitwaye Lucas Angelique alifanikiwa kukusanya vijana 6300 ndani ya wiki moja na kujenga jeshi kubwa kiasi ambacho alitamani hata kutaka kuitawala marekani nzima
Mwaka 1910 Mfalme huyo alikuja kuangushwa na waziri wake aitwaye Samuel viel kwa kupigwa Lisasi ya ubavuni wakati alikuwa akihutubia hali iliyompelekea kuwa mgonjwa na kushindwa kuendelea na vita dhidi ya mfalme wa North Nevada hivyo madaraka ya Lucas Angelique kuyashika samuel viel alikuwa ni mjerumani,kama unavyojua wajerumani kwa roho mbaya
Samuel viel
Mfalme aliyeitikisa marekani pamoja na dunia nzima ni baada ya kupata madaraka ya mapinduzi aliyoyafanya,anaanza kwa kufanya ukatili kueneza udini,ubaguzi na Ukilitimba.
Alikiwa akiua watu bila hatia kosa kwake ni hakuna msamaha anakuua kikatili kwa mkono wake yeye mwenyewe
Hali iliyofanya wananchi wamchukie na wamwogope hivo kupanga njama za kumuua kumuulia mbali
Baada ya kuona usalama wake umekuwa mdogo kiasi cha kupoteza maisha yake aliamua kuongeza wanajeshi ambapo ilifikia idadi 11,000 hapo akajilizisha kwamba yuko salama na ndo lilikuwa jeshi kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani na lenye ukatili wa hali juu zaidi
Hiyo ilimfanya mfalme Samuel Viel kuwa mfalme mwenye nguvu sana duniani kote
Hali hiyo ilipelekea mfalme wa North Nevada aitwaye Jacob d.c kuogopa alijua fika vita kati yake na Sam haiwezi
Jacob d.c
Alikuwa ni mfalme pekee aliye rithi mikoba ya babaake Michael d.c ndani ya miliki yake kuna dhahabu,almasi,rubby na madini mengine mengi sana kiufupi King
Jacob alikuwa ni tajiri kuliko King sam
Ulinzi aliokuwa nao pamoja na jeshi zima ni takribani 1200 ndicho kilicho mfanya haone nikama ameshindwa vita alisahau kuwa (it doesn't matter the size of the weapon but furry of attacks)
"Yaani haijalishi ukubwa wa siraha katika vita hila kwa uwezo wa mapambano"
Ndani ya miaka kumi paradise nevada ilikuwa ndo nchi pekee yenye mabavu ya dunia nzima kifupi ilikuwa ikitawala kwakila kitu miongo ikaenda mpaka sasa ndo nchi pekee yenye kupewa kipaumbele zaidi ndani ya bara la America kwaiyo majeshi au wazamizi wakipanga kuiangamiza dunia lazima waanze na taifa kubwa kama America
Tukutane sehemu ya 3 tujue nini kiliendelea pale Miam7i Beech