Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tatizo tupo nyuma kimaendeleo hata magazeti/vyombo vya habari gavijisgughilishi kututangaza mambo yenye kuvutia(Huyu nilishawahi kumsoma) ila hapa tunaongelea mume na mke mmojamonogous family) au wanawake waliozalishwa na wanaume tofauti
.
Source Ni vyombo vya habari vya wazungu hivyo Ni lazima wajipendelee
Ni km segment ya Dikteta inavyokuwa wengi tunatamani historia za kikwetu lakini hazipatikani mtandaoni tunaishia kuwaongelea wazungu tu ila siyo kwa kupenda
........
Hata record za mchoraji wa nembo ya taifa tu hamna
 
THE LITTLE MAGIC ANGEL

Sehemu ya 2

Ilipoish
.
.
.Mdau ni simulizi nzuri sana na inavutia ila nakusistiza jitahidi kurekebisha makosa
Naona tatizo kubwa lipo kwenye nomino(majina,sehemu n.k)
Ni lazima yaanze kwa herufi kubwa hata kama ni mawili yote yaanze hivyo hivyo
Mfano
North Nevada
Paradise
Chief Commander
Samuel Viel
Jacob D.C n.k

Ukikazia hilo suala na baadhi ya makosa madogo km l badala ya r na z badala ya dh utafika mbali na kuvutia watu wengi

Rekebisha makosa kabla SHIMBA hajaja

............
 
Muziki sio Ajali

Habari za mapumziko ya usiku huu Makapuku wenzangu, ninajua tumekuwa na mwanzo mzuri wa wiki na wale wote ambao tumekutwa na ya kukutwa, basi kesho ni siku nyingine na jua litawaka tena. Kipindi cha pili tunaweza kusaidiwa na upepo, tusichoke.

Turudi tena kwenye muziki na hasa kuangalia udonoaji wa gitaa bila kujali ni gitaa la kawaida au la umeme ilmradi lina nyuzi 12, au 6 au 4 sisi tutalifurahia katika muziki.

Kwa mnaofunga Ramadhani, mnatenda haki na kwa wasiofunga wanatenda haki pia. Ndiyo maisha na kupanga ni kuchagua.

Gitaa. wikend ya jana Sweetiepie alileta wimbo uliopigwa na The Mountain band, wimbo wa reggae na nikasema nitareta orijino version yake iliyopigwa na kuimbwa na Peter Frampton. 'Baby I Love Your Way ndo jina la wimbo na aliucheza miaka ya kati 1970s.

Pamoja na kupigwa miaka hiyo, wimbo na mipigo haikubadilishwa sana maana Peter aliutengeneza kuishi wakati wote hata ukirudiwa.

Japo alipiga gitaa la nyuzi sita, lakiini Peter katika wimbo 'bebi i lavu yua wai' alijikita katika kugusa nyuzi nne tu za mwanzo na hakujisumbua sana na nyuzi mbili za juu ambazo huwa zina kijibass cha kishikaji

Mcheki hapa katika clip ya YouTube uone 'tenor' na sauti zinavyoendana..

Hata record za mchoraji wa nembo ya taifa tu hamna
ec04c327fb9bc2093445e36e6203f1f6.jpg

Kila kitu tufanyiwe na Wazungu ndiyo maana tunaambiwa mtu wa kwanza kuliona Ziwa Victoria ni Mzungu utafikiri mababu zetu walikuwa vipofu(Mimi sijawahi kujaza hivyo kwenye mtihani hata km nimefundishwa hivyo nilikuwa radhi nikose maksi km ni ndogo) maana nilijua ni uongo mtupu tena uliopitiliza na dharau na matusi kwa mababu zetu
......
 
.
.
.Mdau ni simulizi nzuri sana na inavutia ila nakusistiza jitahidi kurekebisha makosa
Naona tatizo kubwa lipo kwenye nomino(majina,sehemu n.k)
Ni lazima yaanze kwa herufi kubwa hata kama ni mawili yote yaanze hivyo hivyo
Mfano
North Nevada
Paradise
Chief Commander
Samuel Viel
Jacob D.C n.k

Ukikazia hilo suala na baadhi ya makosa madogo km l badala ya r na z badala ya dh utafika mbali na kuvutia watu wengi

Rekebisha makosa kabla SHIMBA hajaja

............
Lazima atiririke SHIMBA YA BUYENZE
 
THE LITTLE MAGIC ANGEL

Sehemu ya 2

Ilipoishia
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
Kwakua Chief commander anajua anapambana na kiumbe asichokijua na kwa taarifa alizozipata nikwamba kimedondoka kutoka juu aliwaza labda anaweza kuwa alien au kiumbe cha aina gani alitumia ujuzi wa kijeshi kwa kujaribu kuwaambia wanajeshi wake wazime tochi pia wakae kimya inamaana alitaka kujua hicho kiumbe je kinaona?? Je kinasikia?? Na mashambulizi kinatumia siraha gani........ hayo yalikuwa ni mawazo yake chief commander Mcclaw

Je nikiumbe gani icho???

Story inaturudisha nyuma kabisa takribani miaka 120 iliyopita ndani ya nchi Nevada hapo zamani ilikuwa ni Nevada lakini kwakua kuna uvutano ndani wa pande mbili ikagawanyika ikawa Paradise na North nevada

Hapo ni baada ya mfalme wa Paradise nevada kutaka kumiliki miliki kubwa yaani kuongeza mapana ya utawala wake ndipo akaamua kukusanya jeshi la vijana hili kumsaidia kutimiza adhima yake

Hivyo ilimlazimu kukodi wanajeshi na kuingia mitaani kutafuta vijana wenye nguvu na kuwaingiza katika kikosi chake kwaajili ya mazoezi kwa ufupi alitaka kuifanya nevada iwe yake yote

Mwaka 1890 America ndo lilikuwa bara lenye nguvu zaidi kuwahi kutokea duniani ivyo kuweza kujitawala yenyewe na kuitawala dunia

Mfalme wa paradise nevada aitwaye Lucas Angelique alifanikiwa kukusanya vijana 6300 ndani ya wiki moja na kujenga jeshi kubwa kiasi ambacho alitamani hata kutaka kuitawala marekani nzima

Mwaka 1910 Mfalme huyo alikuja kuangushwa na waziri wake aitwaye Samuel viel kwa kupigwa Lisasi ya ubavuni wakati alikuwa akihutubia hali iliyompelekea kuwa mgonjwa na kushindwa kuendelea na vita dhidi ya mfalme wa North Nevada hivyo madaraka ya Lucas Angelique kuyashika samuel viel alikuwa ni mjerumani,kama unavyojua wajerumani kwa roho mbaya

Samuel viel
Mfalme aliyeitikisa marekani pamoja na dunia nzima ni baada ya kupata madaraka ya mapinduzi aliyoyafanya,anaanza kwa kufanya ukatili kueneza udini,ubaguzi na Ukilitimba.

Alikiwa akiua watu bila hatia kosa kwake ni hakuna msamaha anakuua kikatili kwa mkono wake yeye mwenyewe

Hali iliyofanya wananchi wamchukie na wamwogope hivo kupanga njama za kumuua kumuulia mbali

Baada ya kuona usalama wake umekuwa mdogo kiasi cha kupoteza maisha yake aliamua kuongeza wanajeshi ambapo ilifikia idadi 11,000 hapo akajilizisha kwamba yuko salama na ndo lilikuwa jeshi kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani na lenye ukatili wa hali juu zaidi

Hiyo ilimfanya mfalme Samuel Viel kuwa mfalme mwenye nguvu sana duniani kote
Hali hiyo ilipelekea mfalme wa North Nevada aitwaye Jacob d.c kuogopa alijua fika vita kati yake na Sam haiwezi

Jacob d.c
Alikuwa ni mfalme pekee aliye rithi mikoba ya babaake Michael d.c ndani ya miliki yake kuna dhahabu,almasi,rubby na madini mengine mengi sana kiufupi King
Jacob alikuwa ni tajiri kuliko King sam

Ulinzi aliokuwa nao pamoja na jeshi zima ni takribani 1200 ndicho kilicho mfanya haone nikama ameshindwa vita alisahau kuwa (it doesn't matter the size of the weapon but furry of attacks)

"Yaani haijalishi ukubwa wa siraha katika vita hila kwa uwezo wa mapambano"

Ndani ya miaka kumi paradise nevada ilikuwa ndo nchi pekee yenye mabavu ya dunia nzima kifupi ilikuwa ikitawala kwakila kitu miongo ikaenda mpaka sasa ndo nchi pekee yenye kupewa kipaumbele zaidi ndani ya bara la America kwaiyo majeshi au wazamizi wakipanga kuiangamiza dunia lazima waanze na taifa kubwa kama America

Tukutane sehemu ya 3 tujue nini kiliendelea pale Miam7i Beech

Mdau shedede , kwanza niseme tu, mwanzo umeanza nao ni mzuri. Ni kitu umekaa chini ukaona na kuamini unaweza kufanya kitu na watu wakapata nafasi ya kukisoma kwa uzuri kabisa. Na ndicho nilichofanya.

Nimeipitia yote na utaona kuna sehemu nimekoleza maandishi, hapo namaanisha sarufi haijakaa sawa na kuna haja ya kuangalia sintaksia na semantikia ya kile unachoandika ili tunaosoma tusiwe na tafasiri mbili mbili (tata).

Najua kabisa unaandika hadithi ya kubuni (fiction) inayohusisha si vitu halisi bali vya kubuni na hisia zaidi. lakini changamoto yangu tu moja kwako, ukiweka vitu vya kubuni halafu ukajidai kuweka miaka basi wapo watu wanasoma sana fition na non-fiction na mmoja wapo ni mimi. Huo mwaka unaosema 1890 unaiongelea karne ya 19 na Amerika haikuwahi kuwa taifa kubwa duniani kipindi hicho, hapo tunaongelea dola la Waingereza, Wafaransa, na Warusi.

Kuwa makini sana, umewahi kusoma vitabu vya Musiba (Wily Gamba) alikuwa akiielezea dola fulani basi utadhani anachoandika si cha kubuni, ni cha kweli kumbe la.
Sikumbuki title ya kitabu lakini aliwahi kuuelezea mji na barabara za Maganzo Shinyanga na kwa kuwa nimewahi kupita maeneo hayo basi nikawa naamini ile hadithi si ya kubuni.

Nadhani umenielewa kwenye kuhakikisha unaweka ukweli kwenye hisia zako unazotaka tuzisome.

Mengine kakuelezea Bitoz na ukiyafuatilia hakyanani utatoka na kitu kizuri na kutufanya Makapuku tujisikie vizuri.

Love
Obe
 
.
.
.Mdau ni simulizi nzuri sana na inavutia ila nakusistiza jitahidi kurekebisha makosa
Naona tatizo kubwa lipo kwenye nomino(majina,sehemu n.k)
Ni lazima yaanze kwa herufi kubwa hata kama ni mawili yote yaanze hivyo hivyo
Mfano
North Nevada
Paradise
Chief Commander
Samuel Viel
Jacob D.C n.k

Ukikazia hilo suala na baadhi ya makosa madogo km l badala ya r na z badala ya dh utafika mbali na kuvutia watu wengi

Rekebisha makosa kabla SHIMBA hajaja

............
mkuu narekebisha kabula hajaja
 
Mdau shedede , kwanza niseme tu, mwanzo umeanza nao ni mzuri. Ni kitu umekaa chini ukaona na kuamini unaweza kufanya kitu na watu wakapata nafasi ya kukisoma kwa uzuri kabisa. Na ndicho nilichofanya.

Nimeipitia yote na utaona kuna sehemu nimekoleza maandishi, hapo namaanisha sarufi haijakaa sawa na kuna haja ya kuangalia sintaksia na semantikia ya kile unachoandika ili tunaosoma tusiwe na tafasiri mbili mbili (tata).

Najua kabisa unaandika hadithi ya kubuni (fiction) inayohusisha si vitu halisi bali vya kubuni na hisia zaidi. lakini changamoto yangu tu moja kwako, ukiweka vitu vya kubuni halafu ukajidai kuweka miaka basi wapo watu wanasoma sana fition na non-fiction na mmoja wapo ni mimi. Huo mwaka unaosema 1890 unaiongelea karne ya 19 na Amerika haikuwahi kuwa taifa kubwa duniani kipindi hicho, hapo tunaongelea dola la Waingereza, Wafaransa, na Warusi.

Kuwa makini sana, umewahi kusoma vitabu vya Musiba (Wily Gamba) alikuwa akiielezea dola fulani basi utadhani anachoandika si cha kubuni, ni cha kweli kumbe la.
Sikumbuki title ya kitabu lakini aliwahi kuuelezea mji na barabara za Maganzo Shinyanga na kwa kuwa nimewahi kupita maeneo hayo basi nikawa naamini ile hadithi si ya kubuni.

Nadhani umenielewa kwenye kuhakikisha unaweka ukweli kwenye hisia zako unazotaka tuzisome.

Mengine kakuelezea Bitoz na ukiyafuatilia hakyanani utatoka na kitu kizuri na kutufanya Makapuku tujisikie vizuri.

Love
Obe
Ndiyo vizuri kumwambia mapema mapungufu yake ili awe bora baadaye
Ni bora ingekuwa kaandika mwaka 1135 kuliko hivyo

Watu wanaokubali kukosolewa na kuyafanyia kazi mapungufu yao mbeleni huwa watu bora pengine kuwazidi hata waliowakosoa
............
 
Ndiyo vizuri kumwambia mapema mapungufu yake ili awe bora baadaye
Ni bora ingekuwa kaandika mwaka 1135 kuliko hivyo

Watu wanaokubali kukosolewa na kuyafanyia kazi mapungufu yao mbele ni huwa watu bora pengine kuwazidi hata waliowakosoa
............
Na mimi editor nilipaswa kuliona hilo. Asanteni sana jamani. Upendo huu wa Makapuku yaani mpaka raha.

Notion niliyoipata katika kile kipande cha kwanza ni kwamba pengine alikiandika kwa haraka na hakuwa na muda. Na mimi kama editor nilishughulika zaidi na makosa madogo madogo tu ya kisarufi, na pia sikutaka kumkatisha tamaa. Ngoja sasa kama editor niende full throttle kwake. Naamini kazi zake zitakuwa bora zaidi na huko mbele ya safari anaweza hata kutoa kitabu. Kumbe yote yameanzia hapa Makapuku. Asante sana Obe na Madenge kwa moyo wenu huu. Mbarikiwe sana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom