Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mdau shedede , kwanza niseme tu, mwanzo umeanza nao ni mzuri. Ni kitu umekaa chini ukaona na kuamini unaweza kufanya kitu na watu wakapata nafasi ya kukisoma kwa uzuri kabisa. Na ndicho nilichofanya.

Nimeipitia yote na utaona kuna sehemu nimekoleza maandishi, hapo namaanisha sarufi haijakaa sawa na kuna haja ya kuangalia sintaksia na semantikia ya kile unachoandika ili tunaosoma tusiwe na tafasiri mbili mbili (tata).

Najua kabisa unaandika hadithi ya kubuni (fiction) inayohusisha si vitu halisi bali vya kubuni na hisia zaidi. lakini changamoto yangu tu moja kwako, ukiweka vitu vya kubuni halafu ukajidai kuweka miaka basi wapo watu wanasoma sana fition na non-fiction na mmoja wapo ni mimi. Huo mwaka unaosema 1890 unaiongelea karne ya 19 na Amerika haikuwahi kuwa taifa kubwa duniani kipindi hicho, hapo tunaongelea dola la Waingereza, Wafaransa, na Warusi.

Kuwa makini sana, umewahi kusoma vitabu vya Musiba (Wily Gamba) alikuwa akiielezea dola fulani basi utadhani anachoandika si cha kubuni, ni cha kweli kumbe la.
Sikumbuki title ya kitabu lakini aliwahi kuuelezea mji na barabara za Maganzo Shinyanga na kwa kuwa nimewahi kupita maeneo hayo basi nikawa naamini ile hadithi si ya kubuni.

Nadhani umenielewa kwenye kuhakikisha unaweka ukweli kwenye hisia zako unazotaka tuzisome.

Mengine kakuelezea Bitoz na ukiyafuatilia hakyanani utatoka na kitu kizuri na kutufanya Makapuku tujisikie vizuri.

Love
Obe
Ndomana sikui-post kule J_I kule hakuna washauri bali wapondaji nashukuruni jamani
Ndiyo vizuri kumwambia mapema mapungufu yake ili awe bora baadaye
Ni bora ingekuwa kaandika mwaka 1135 kuliko hivyo

Watu wanaokubali kukosolewa na kuyafanyia kazi mapungufu yao mbele ni huwa watu bora pengine kuwazidi hata waliowakosoa
............
 
Ooh sorry! Hii part two sikupata muda wa kuihariri. Naona Shedede ameamua kuishusha bila input yangu and sadly makosa yale yale ambayo niliyakemea katika sehemu ya kwanza yamejirudia tena katika part two.

Please ignore hiyo comment yangu ya juu ️. Sihusiki na hii part two...
 
Tatizo tupo nyuma kimaendeleo hata magazeti/vyombo vya habari gavijisgughilishi kututangaza mambo yenye kuvutia(Huyu nilishawahi kumsoma) ila hapa tunaongelea mume na mke mmojamonogous family) au wanawake waliozalishwa na wanaume tofauti
.
Source Ni vyombo vya habari vya wazungu hivyo Ni lazima wajipendelee
Ni km segment ya Dikteta inavyokuwa wengi tunatamani historia za kikwetu lakini hazipatikani mtandaoni tunaishia kuwaongelea wazungu tu ila siyo kwa kupenda
........

Mdau, kuna jambo moja la msingi ambalo sisi tunalimiss sana. Kuweka kumbukumbu (documentation). Ni wachache sana ambao kwanza tu huwa wana tabia ya kuweka kumbukumbu.

Hakyanani kuna matukio mazuri tu hapa nchini tena yametokea miaka ya 1980 lakini ukiyasaka huyaoni hata kidogo maana hayajatunzwa kwa kila mmoja ayaone.

Fikiria sasa haijulikani mbunifu wa nembo/ngao ya taifa? Yule aliyepandisha mwenge kileleni kaanza kujulikana juzi juzi tu hapa baada ya watu kupiga kelele. Tuna upuuzi wa kutoweka kumbukumbu na wkijitokeza aina ya watu kama kina Mohd Said basi tunawavika label, yes, wanakusanya wanachodhani ni chao, lakini sisi kama jamii tunafanya nini?

Ajali inatokea, watu wanakufa. Hebu jiulize, sikusoma (ninaruhusu kukosolewa) hata sehemu moja ambapo majina ya watoto waliofariki kwenye ajali ya gari kule Arusha walitajwa kwa majina? Unawezaje kuweka kumbukumbu kama hutaji jina na tukio?

Au huwa yanawekwa sehemu ambayo wengine hatuna access. Ni hayo tu
 
Ooh sorry! Hii part two sikupata muda wa kuihariri. Naona Shedede ameamua kuishusha bila input yangu and sadly makosa yale yale ambayo niliyakemea katika sehemu ya kwanza yamejirudia tena katika part two.

Please ignore hiyo comment yangu ya juu ️. Sihusiki na hii part two...
Habar yako ??
Editor:SHUMBA YA BUYENSE
 
Na mimi editor nilipaswa kuliona hilo. Asanteni sana jamani. Upendo huu wa Makapuku yaani mpaka raha.

Notion niliyoipata katika kile kipande cha kwanza ni kwamba pengine alikiandika kwa haraka na hakuwa na muda. Na mimi kama editor nilishughulika zaidi na makosa madogo madogo tu ya kisarufi, na pia sikutaka kumkatisha tamaa. Ngoja sasa kama editor niende full throttle kwake. Naamini kazi zake zitakuwa bora zaidi na huko mbele ya safari anaweza hata kutoa kitabu. Kumbe yote yameanzia hapa Makapuku. Asante sana Obe na Madenge kwa moyo wenu huu. Mbarikiwe sana!

Ooh sorry! Hii part two sikupata muda wa kuihariri. Naona Shedede ameamua kuishusha bila input yangu and sadly makosa yale yale ambayo niliyakemea katika sehemu ya kwanza yamejirudia tena katika part two.

Please ignore hiyo comment yangu ya juu ️. Sihusiki na hii part two...
Pamoja sana mdau
.......
 
THE LITTLE MAGIC ANGEL

Sehemu ya 2

Ilipoishia
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

.
.
Kwakua Chief commander anajua anapambana na kiumbe asichokijua na kwa taarifa alizozipata nikwamba kimedondoka kutoka juu aliwaza labda anaweza kuwa alien au kiumbe cha aina gani alitumia ujuzi wa kijeshi kwa kujaribu kuwaambia wanajeshi wake wazime tochi pia wakae kimya inamaana alitaka kujua hicho kiumbe je kinaona?? Je kinasikia?? Na mashambulizi kinatumia siraha gani........ hayo yalikuwa ni mawazo yake chief commander Mcclaw

Je nikiumbe gani icho???

Story inaturudisha nyuma kabisa takribani miaka 120 iliyopita ndani ya nchi Nevada hapo zamani ilikuwa ni Nevada lakini kwakua kuna uvutano ndani wa pande mbili ikagawanyika ikawa Paradise na North nevada

Hapo ni baada ya mfalme wa Paradise nevada kutaka kumiliki miliki kubwa yaani kuongeza mapana ya utawala wake ndipo akaamua kukusanya jeshi la vijana hili kumsaidia kutimiza adhima yake

Hivyo ilimlazimu kukodi wanajeshi na kuingia mitaani kutafuta vijana wenye nguvu na kuwaingiza katika kikosi chake kwaajili ya mazoezi kwa ufupi alitaka kuifanya nevada iwe yake yote

Mwaka 1890 America ndo lilikuwa bara lenye nguvu zaidi kuwahi kutokea duniani ivyo kuweza kujitawala yenyewe na kuitawala dunia

Mfalme wa paradise nevada aitwaye Lucas Angelique alifanikiwa kukusanya vijana 6300 ndani ya wiki moja na kujenga jeshi kubwa kiasi ambacho alitamani hata kutaka kuitawala marekani nzima

Mwaka 1910 Mfalme huyo alikuja kuangushwa na waziri wake aitwaye Samuel viel kwa kupigwa Lisasi ya ubavuni wakati alikuwa akihutubia hali iliyompelekea kuwa mgonjwa na kushindwa kuendelea na vita dhidi ya mfalme wa North Nevada hivyo madaraka ya Lucas Angelique kuyashika samuel viel alikuwa ni mjerumani,kama unavyojua wajerumani kwa roho mbaya

Samuel viel
Mfalme aliyeitikisa marekani pamoja na dunia nzima ni baada ya kupata madaraka ya mapinduzi aliyoyafanya,anaanza kwa kufanya ukatili kueneza udini,ubaguzi na Ukilitimba.

Alikiwa akiua watu bila hatia kosa kwake ni hakuna msamaha anakuua kikatili kwa mkono wake yeye mwenyewe

Hali iliyofanya wananchi wamchukie na wamwogope hivo kupanga njama za kumuua kumuulia mbali

Baada ya kuona usalama wake umekuwa mdogo kiasi cha kupoteza maisha yake aliamua kuongeza wanajeshi ambapo ilifikia idadi 11,000 hapo akajilizisha kwamba yuko salama na ndo lilikuwa jeshi kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani na lenye ukatili wa hali juu zaidi

Hiyo ilimfanya mfalme Samuel Viel kuwa mfalme mwenye nguvu sana duniani kote
Hali hiyo ilipelekea mfalme wa North Nevada aitwaye Jacob d.c kuogopa alijua fika vita kati yake na Sam haiwezi

Jacob d.c
Alikuwa ni mfalme pekee aliye rithi mikoba ya babaake Michael d.c ndani ya miliki yake kuna dhahabu,almasi,rubby na madini mengine mengi sana kiufupi King
Jacob alikuwa ni tajiri kuliko King sam

Ulinzi aliokuwa nao pamoja na jeshi zima ni takribani 1200 ndicho kilicho mfanya haone nikama ameshindwa vita alisahau kuwa (it doesn't matter the size of the weapon but furry of attacks)

"Yaani haijalishi ukubwa wa siraha katika vita hila kwa uwezo wa mapambano"

Ndani ya miaka kumi paradise nevada ilikuwa ndo nchi pekee yenye mabavu ya dunia nzima kifupi ilikuwa ikitawala kwakila kitu miongo ikaenda mpaka sasa ndo nchi pekee yenye kupewa kipaumbele zaidi ndani ya bara la America kwaiyo majeshi au wazamizi wakipanga kuiangamiza dunia lazima waanze na taifa kubwa kama America

Tukutane sehemu ya 3 tujue nini kiliendelea pale Miam7i Beech
Shedede unaniangusha. Kama editor wako ulipaswa kunitonya kuwa sehemu ya pili iko tayari.

Cha kusikitisha zaidi ni kwamba bado unarudia makosa yale yale ambayo nilikuandikia kwa kina katika sehemu ya kwanza na kukuomba sana kuwa usiyarudie tena. Miami7i Beech ni nini? Sikulizungumzia suala hili? Vipi kuhusu common nouns pamoja na titles kuwa ni lazima zianze kwa herufi kubwa? Vipi kuhusu kuepuka misentesi mirefu yenye korogesheni na kuzingatia alama za uandishi. Tazama kwa mfano sentensi ya mwisho ambayo kimsingi ni aya nzima

"Ndani ya miaka kumi paradise nevada ilikuwa ndo nchi pekee yenye mabavu ya dunia nzima kifupi ilikuwa ikitawala kwakila kitu miongo ikaenda mpaka sasa ndo nchi pekee yenye kupewa kipaumbele zaidi ndani ya bara la America kwaiyo majeshi au wazamizi wakipanga kuiangamiza dunia lazima waanze na taifa kubwa kama America"

Ni nini hichi ️? Aya yenye sentensi moja? nevada?

Kaa utulie. Andika kwa kituo. May be kwa vile ni makapuku basi hujali sana. Ungekuwa unaipeleka kule kwingine ungeipeleka ikiwa na makosa haya ya wazi? Hakuna kitu kinachopoteza credibility ya mwandishi kama makosa ambayo hata mtoto wa darasa la tatu anayakwepa. Maadam umeamua kuandika basi please kuwa siriazi.

Nategemea kuona mabadiliko makubwa huko mbele ya safari. Ni afadhali hadithi zichelewe lakini zitoke zikiwa zimekamilika. Blessings!
 
Mdau, kuna jambo moja la msingi ambalo sisi tunalimiss sana. Kuweka kumbukumbu (documentation). Ni wachache sana ambao kwanza tu huwa wana tabia ya kuweka kumbukumbu.

Hakyanani kuna matukio mazuri tu hapa nchini tena yametokea miaka ya 1980 lakini ukiyasaka huyaoni hata kidogo maana hayajatunzwa kwa kila mmoja ayaone.

Fikiria sasa haijulikani mbunifu wa nembo/ngao ya taifa? Yule aliyepandisha mwenge kileleni kaanza kujulikana juzi juzi tu hapa baada ya watu kupiga kelele. Tuna upuuzi wa kutoweka kumbukumbu na wkijitokeza aina ya watu kama kina Mohd Said basi tunawavika label, yes, wanakusanya wanachodhani ni chao, lakini sisi kama jamii tunafanya nini?

Ajali inatokea, watu wanakufa. Hebu jiulize, sikusoma (ninaruhusu kukosolewa) hata sehemu moja ambapo majina ya watoto waliofariki kwenye ajali ya gari kule Arusha walitajwa kwa majina? Unawezaje kuweka kumbukumbu kama hutaji jina na tukio?

Au huwa yanawekwa sehemu ambayo wengine hatuna access. Ni hayo tu
Ajali ya Arusha majina yaliwekwa hadharani
Tatizo hatuna uzalendo
Ipo siku kitajitokeza kibabu tapeli na kusema yeye ndo aliyeshiriki kuwaokoa watu wengi kwa mtumbwi wakati wa ajali ya MV Bukoba au alimfundisha Nyerere na hakuna atakayembishia maana matukio muhimu hayakutunzwa

......
 
.
.
.Mdau ni simulizi nzuri sana na inavutia ila nakusistiza jitahidi kurekebisha makosa
Naona tatizo kubwa lipo kwenye nomino(majina,sehemu n.k)
Ni lazima yaanze kwa herufi kubwa hata kama ni mawili yote yaanze hivyo hivyo
Mfano
North Nevada
Paradise
Chief Commander
Samuel Viel
Jacob D.C n.k

Ukikazia hilo suala na baadhi ya makosa madogo km l badala ya r na z badala ya dh utafika mbali na kuvutia watu wengi

Rekebisha makosa kabla SHIMBA hajaja

............
Too late. I am mad as hell !
fa5b7adac8105d37f7f3e4f78dffec7a.jpg
 
Na mimi editor nilipaswa kuliona hilo. Asanteni sana jamani. Upendo huu wa Makapuku yaani mpaka raha.

Notion niliyoipata katika kile kipande cha kwanza ni kwamba pengine alikiandika kwa haraka na hakuwa na muda. Na mimi kama editor nilishughulika zaidi na makosa madogo madogo tu ya kisarufi, na pia sikutaka kumkatisha tamaa. Ngoja sasa kama editor niende full throttle kwake. Naamini kazi zake zitakuwa bora zaidi na huko mbele ya safari anaweza hata kutoa kitabu. Kumbe yote yameanzia hapa Makapuku. Asante sana Obe na Madenge kwa moyo wenu huu. Mbarikiwe sana!

Part 1 niliisoma na ilikuwa vizuri nadhani uhariri uliifanya isiwe na makosa mengi. Ila hii , kuna watu huwa tunajifunza kuhoji hata hisia 😀😀😀😀😀😵
 
Mdau, kuna jambo moja la msingi ambalo sisi tunalimiss sana. Kuweka kumbukumbu (documentation). Ni wachache sana ambao kwanza tu huwa wana tabia ya kuweka kumbukumbu.

Hakyanani kuna matukio mazuri tu hapa nchini tena yametokea miaka ya 1980 lakini ukiyasaka huyaoni hata kidogo maana hayajatunzwa kwa kila mmoja ayaone.

Fikiria sasa haijulikani mbunifu wa nembo/ngao ya taifa? Yule aliyepandisha mwenge kileleni kaanza kujulikana juzi juzi tu hapa baada ya watu kupiga kelele. Tuna upuuzi wa kutoweka kumbukumbu na wkijitokeza aina ya watu kama kina Mohd Said basi tunawavika label, yes, wanakusanya wanachodhani ni chao, lakini sisi kama jamii tunafanya nini?

Ajali inatokea, watu wanakufa. Hebu jiulize, sikusoma (ninaruhusu kukosolewa) hata sehemu moja ambapo majina ya watoto waliofariki kwenye ajali ya gari kule Arusha walitajwa kwa majina? Unawezaje kuweka kumbukumbu kama hutaji jina na tukio?

Au huwa yanawekwa sehemu ambayo wengine hatuna access. Ni hayo tu
Oral tradition bado ndiyo njia yetu kuu nadhani. Ukijumlisha na umbea wetu huu basi ni kazi kweli kweli. Na kwa taifa la watu wasiopenda hata kusoma vitabu hili halishangazi. Kama sikosei kuna idara kabisa inayopaswa kujishughulisha na mambo haya japo haitashangaza kama haijafanya lolote haijalishi hata kama ina bajeti ya mamilioni kila mwaka. Hata viongozi huwa nawashangaa. Kuinyoosha nchi kama hii unaanzia wapi kwanza?
 
Shedede unaniangusha. Kama editor wako ulipaswa kunitonya kuwa sehemu ya pili iko tayari.

Cha kusikitisha zaidi ni kwamba bado unarudia makosa yale yale ambayo nilikuandikia kwa kina katika sehemu ya kwanza na kukuomba sana kuwa usiyarudie tena. Miami7i Beech ni nini? Sikulizungumzia suala hili? Vipi kuhusu common nouns pamoja na titles kuwa ni lazima zianze kwa herufi kubwa? Vipi kuhusu kuepuka misentesi mirefu yenye korogesheni na kuzingatia alama za uandishi. Tazama kwa mfano sentensi ya mwisho ambayo kimsingi ni aya nzima

"Ndani ya miaka kumi paradise nevada ilikuwa ndo nchi pekee yenye mabavu ya dunia nzima kifupi ilikuwa ikitawala kwakila kitu miongo ikaenda mpaka sasa ndo nchi pekee yenye kupewa kipaumbele zaidi ndani ya bara la America kwaiyo majeshi au wazamizi wakipanga kuiangamiza dunia lazima waanze na taifa kubwa kama America"

Ni nini hichi ️? Aya yenye sentensi moja? nevada?

Kaa utulie. Andika kwa kituo. May be kwa vile ni makapuku basi hujali sana. Ungekuwa unaipeleka kule kwingine ungeipeleka ikiwa na makosa haya ya wazi? Hakuna kitu kinachopoteza credibility ya mwandishi kama makosa ambayo hata mtoto wa darasa la tatu anayakwepa. Maadam umeamua kuandika basi please kuwa siriazi.

Nategemea kuona mabadiliko makubwa huko mbele ya safari. Ni afadhali hadithi zichelewe lakini zitoke zikiwa zimekamilika. Blessings!
Paragraph nimekuelewa mkuu next time ni improvement story lazima ipite kwako mkuu blessings
 
Ooh sorry! Hii part two sikupata muda wa kuihariri. Naona Shedede ameamua kuishusha bila input yangu and sadly makosa yale yale ambayo niliyakemea katika sehemu ya kwanza yamejirudia tena katika part two.

Please ignore hiyo comment yangu ya juu ️. Sihusiki na hii part two...
 
Too late. I am mad as hell !
fa5b7adac8105d37f7f3e4f78dffec7a.jpg
Anatakiwa yeye mwenyewe aifanye kazi yake kwa mapenzi na moyo km Mussolini na One kwenye segment zao
Kitu cha kwanza kabisa ili ufanikiwe ni lazima ukipende kile unachokifanya
.
.
Ukichunguza hata kwenye historia anazoleta Dikteta huwa simwekei tu picha ilimradi bali nahahakikisha zina ubora/mvuto au kuakisi maudhui na hata zinazoongeza kujifunza
Tukutane kesho
........
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom