Makapuku Forum

Ukipenda chongo utaliita kengeza. ManSix. Manure.
 
Ni kweli. Madalali ndiyo wananufaika zaidi. Kilimo, kwa maoni yangu, ndiyo mkakati mama utakaoikomboa nchi hii na kuitoa hapo ilipokwama. Hata Wachina walipoweza kuleta mabadiliko ya kilimo ndiyo milango mingine ikafunguka. Sisi tunataka kurukia viwanda. Sijui viwanda bila malighafi za kuaminika itakuwaje. Inatakiwa unaleta mapinduzi ya kilimo kwanza unakuwa na umma unaoshiba na kuzalisha malighafi unazozitaka kwa ajili ya viwanda vyako. Kwa hali hii unainua maisha ya wakulima kwa kuwapatia soko la kuaminika la mazao yao na wakati huo huo unalisha viwanda vyako. Sisi nadhani tunakwenda kinyume nyume....
 
Ahsante mkuu, ila ni vizuri uwe unatuwekea na tarehe kabisa, mfano leo tarehe 28/1/2017 ili ieleweke hata baada ya tarehe ya leo kupita!
 
Mkinga, asante kwa kazi nzuri ila ukiendelea hivi nitaacha kazi kama wewe ulivyoacha kazi yako ya ulinzi. Kuna mambo kadhaa hukuzingatia.

Nilisema kuwa jina la hadithi lote ni lazima lianze na herufi kubwa yaani The Little Magic Angel. Sijui kwa nini umempuuza editor wako.

Pia proper names zote ni lazima zianze na herufi kubwa mf. Shimba ya Buyenze. Bado unafanya kosa hili. Halafu unakosea jina langu mimi mhariri wako. Kweli?

Kuwa siriazi bana kama mimi msaidizi wako nilivyo siriazi vinginevyo tutaparaganyika. Sehemu ya pili lini? Editor niko tayari!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…