shululu
JF-Expert Member
- Jan 26, 2015
- 28,137
- 109,911
Amen mama mchungajiZABURI 121
1.Nitayainua macho yangu niitazame milima,Msaada wangu utatoka wapi?
2.Msaada wangu u katika BWANA,Aliyezifanya mbingu na nchi.
3.Asiuache mguu wako usogezwe,Asisisinzie akulindaye.
4.Naam,hatasinzia wala hatalala usingizi.Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5.BWANA ndiye mlinzi wako;BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.
6.Jua halitakupiga mchana,Wala mwezi wakati wa usiku.
7.BWANA atakulinda na mabaya yote ,Atakulinda nafsi yako.
8.BWANA atakulinda utokapo na uingiapo,Tangu sasa na hata milele.
TUOMBE
Mwenyezi Mungu
Asante kwa ajili ya leo
Tunaomba uzidi kuwa nasi
Tutakase makosa yetu
Kutana na haja za mioyo yetu
Tukumbatie kama kuku akumbatiavyo vifaranga
Malaika walinzi waweke vituo katika nyumba na vitanda vyetu ,watuzunguke
Wakeshe pamoja nasi
Naenda kinyume na nguvu zote za giza
Damu ya Yesu itufunike
Asante maana utatenda zaidi ya tunavyoomba
Katika jina la Yesu Kristo
Tunaomba na kuamini
Amen
USIKU MWEMA WAPENDWA![]()
![]()
Nawe pia usiku mwema
ZABURI 121