Makapuku Forum

Makapuku Forum

Pole sana mkuu Mussolin5 naungana nawe katika kumuombea binamu mpendwa

NAMUOMBA MUNGU ATUPE UVUMILIVU WA KIMAPENDO,BWANA ALITOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE NA DAIMA TUWE NA MATUMAINI,SINA NENO ZURI LA KUSEMA BALI NAOMBA TUUNGANE HAPA :

1 WATHESALONIKE 4

13.Lakini ,ndugu zangu,hatutaki msijue habari zao waliolala mauti,msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.

14.Maana ,ikiwa twaamini ya kwamba,Yesu alikufa akafufuka vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu Mungu atawaleta pamoja naye.

15. Kwakuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana ,kwamba sisi tulio hai tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana,hakika hatutawatangulia wao walioisha kulala mauti.

16. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko ,na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya Mungu,nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

17.Kisha sisi tulio hai tuliosalia ,tutanyakuliwa pamoja nao mawinguni,ili tumlaki Bwana hewani na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

18.Basi farijianeni kwa maneno haya.

Naomba tuamini kuwa Binamu mpendwa wetu amelala na tutaonana siku ya mwisho,nafsi yake ipokelewe na Mungu wetu

"Wale tunaowapenda hawaendi milele,wanatembea pembeni yetu daima,hatuwasikii,hatuwaoni
Lakini wapo daima nasi,tunawapenda,tunawahitaji,tunawakumbuka wanadumu mioyoni mwetu....upendo wetu kwao ni ishara ya uwepo wao maana walituachia upendo"
Amen, nashukuru sana.
 
Hakuna kitu kinacholeta faraja na furaha kama kusaidia wahitaji hata kama huna kitu,kushare kidogo ulichonacho na wale ambao hawana kabisa imagine unaenda hospital kumtembelea ndugu yako amelazwa mnajikuta mko 20 mmezunguka kitanda ,lakini next bed kuna mtu kapata referal kuja muhimbili hana ndugu hebu sogea tumia muda nae,ongea nae mpe kidogo ulichonacho aaah huwezi amini utakuwa unatafuta safari a kutembelea watu wa aina hii na hutapungukiwa,nauli,cha kuwapa hata neno la kuwatia moyo .hata majumbani wapo wengi wanahitaji faraja ,kutiwa moyo,kusikilizwa pata muda wa kuwaona watu hawa wapo wengi sana Mungu atutie nguvu

Nehemia 8

10b....furaha ya BWANA ni nguvu zenu.

Haleuiya

MATENDO YA MITUME 20

35.Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge,na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu ,jinsi alivyosema mwenyewe. Ni heri kutoa kuliko kupokea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom