KUMTEGEMEA MUNGU KUNA FAIDA

ISAYA 40
29 Huwapa nguvu wazimiao ,humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo

Pale unapochoka fikra unapowaza sana unapokata tamaa ndipo Mungu anapokupa nguvu na kinga za kila shambulizi pia kukuvusha juu ya hali uliyo nayo ,hivyo pambana na hali hiyo kwani Bwana anatamalaki na kukupa utulivu na ushindi ili kumshinda adui anapotaka kukudhuru
Tumuombe Mungu atusaidie tumkabidhi Mungu njia zetu zote naye hatatuacha
TUOMBE
MUNGU BABA MWENYEZI tunakushukuru sana kwa ulinzi wako na yote unayotutendea,Mungu,umetutoa mbali tunakushukuru sana.
Ponya wagonjwa,fariji wafiwa,fariji wajane na yatima,tembea nasi Baba nyoosha mapito yetu,peke yetu hatuwezi
Tunajikabidhi miili na roho zetu tukinge na hatari zote za mwili na roho.
Roho Mtakatifu Mfariji wetu tufundishe ,tuongoze,tuonyeshe njia sahihi ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu
Asante kwa kila linakotokea maishani mwetu
Tunaomba yote kwa jina la Yesu mpatanishi na mwokozi wetu .
Amen
Muwe na siku njema,wiki njema,mwezi mwema.....MBARIKIWE