Makapuku Forum

Makapuku Forum

Come on Mukongoman! Una batophobia? Ndege huwa unapanda na huogopi? Ulianza anzaje kuogopa haya majengo marefu?

Ila hizi phobia zingine hizi hata sijui zinaanzaje. Mimi siku hizi nikiona mende chumbani silali aisee mpaka nimtafute nimuue. Nikilala bila kumuua basi nitaota limende likuuuubwa linaninyemelea sasa hata kulikimbia siwezi. Hapo mwanaume ni kutoka jasho balaa. Ajabu wadudu wengine na hata nyoka sina tatizo nao kabisa. Huwa nashangaa sana kwa sababu nimekulia kijijini na mende kibao and it was no big deal.
Kemea utaisha,kuna wakati nulijua naogipa sana nyoka kila nikiingia ndani nawaza nyoka huwezi amini siku moja alfajiri nilijikuta nimebeba nyoka mgongoni nakung'uta akaanguka haa nikaitaa jina la Yesu nilipambana hadi kumuua,na nikaanza rasmi kukemea mfululizo limeisha hili jambo namshukuru Mungu
 
Nisikudanganye Mtumishi. Mimi siyo mwanasheria na kusema kweli mbali na kujua haki zangu za msingi kama raia wa Jamhuri ya Tanzania sijui cho chote kuhusu sheria.

Umesema kuwa walifeli kidato cha nne wakafanya mbinu wakabadili matokeo yao kinyemela (wakagushi vyeti) na matokeo hayo feki ndiyo yakawafanya wapate nafasi ya kuendelea na masomo yao mpaka wakapata ajira; na leo kosa lao walilofanya zamani ndiyo limesababisha watumbuliwe. Sijui tafsiri ya kisheria lakini nadhani kubadili matokeo kinyemela ni kosa. Kama kuna kapuku mwanasheria anaweza kutufafanulia zaidi.

Nimesikia TLS chini ya Tundu Lissu imewashauri wafanyakazi wote wanaoamini kuwa wametumbuliwa kimakosa waungane wafungue class action suit dhidi ya serikali na TLS itawapa msaada wa kisheria bure. Wanaweza kupata ufafanuzi wa kosa lao kisheria (kama wametenda kosa) na watajua cha kufanya baada ya hapo. Washauri wawasiliane na TLS au mwanasheria ye yote angalau wajue kosa lao limekaaje kisheria...and then they can go from there.

Bashite yeye alipiga ziro form 4 akanunua cheti cha mtu mwingine. Hawa matokeo hayakutosha wakajazia jazia kinyemela kwa majina yao yale yale. Sijui yupi ana kosa kubwa zaidi ya mwingine. Uwe na amani mtumishi na wape pole sana. Waambie wasikate tamaa. Maisha ni lazima yaendelee ati! Mungu Atawafungulia milango mingine!
Ndugu yangu mmoja yeye alijionggeza, alianza kufanya biashara zake huku anaffanya kazi lakini akijua kuwa hana chake tena kazini, alijitengenezea mazingira ya kutokuwa na pressure baada ya kutumbuliwa
 
Naunga mkono hoja yako.

Pele amechukua World Cup mara 3 lakini hakuwahi kuwa mfungaji bora au hata mchezaji bora.

Mwaka 1958 wanachukua kombe la Dunia Pele alikuwa ndio chipukizi.

Mwaka 1962 wanachukua Kombe la Dunia staa wa michuano alikuwa Mane Garrincha. Pele alicheza mechi mbili tu.

Mwaka 1970 wanachukua tena Kombe la Dunia pale Mexico. Staa wa michuano alikuwa Jaizinho ambaye alifunga goli kila mechi.

Lakini Maradona alikuwa ndio staa wa michuano pale alipoibeba Argentina mwaka 1986 na kutwaa Kombe la Dunia.

Pele alibebwa na mastaa wengine. Wakati Maradona ilibidi aibebe timu kwenye mgongo wake.
Ila mess kashindwa kuibeba Argentina

Kuna baadhi ya raia wa Argentina wanaamini mess ni mkatarunya na si muargentina
 
c934fd18b0a8aa7ea4e08e6f79c42db8.jpg
726bf503032bceb2f9d711036eb7552f.jpg

Barca dk 180 bila bao
.....
Huyu na yule kipala, Barcelona hawawezi kuwasahau
 
KUMTEGEMEA MUNGU KUNA FAIDA

ISAYA 40

29 Huwapa nguvu wazimiao ,humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo

Pale unapochoka fikra unapowaza sana unapokata tamaa ndipo Mungu anapokupa nguvu na kinga za kila shambulizi pia kukuvusha juu ya hali uliyo nayo ,hivyo pambana na hali hiyo kwani Bwana anatamalaki na kukupa utulivu na ushindi ili kumshinda adui anapotaka kukudhuru

Tumuombe Mungu atusaidie tumkabidhi Mungu njia zetu zote naye hatatuacha

TUOMBE

MUNGU BABA MWENYEZI tunakushukuru sana kwa ulinzi wako na yote unayotutendea,Mungu,umetutoa mbali tunakushukuru sana.

Ponya wagonjwa,fariji wafiwa,fariji wajane na yatima,tembea nasi Baba nyoosha mapito yetu,peke yetu hatuwezi

Tunajikabidhi miili na roho zetu tukinge na hatari zote za mwili na roho.

Roho Mtakatifu Mfariji wetu tufundishe ,tuongoze,tuonyeshe njia sahihi ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu

Asante kwa kila linakotokea maishani mwetu

Tunaomba yote kwa jina la Yesu mpatanishi na mwokozi wetu .

Amen

Muwe na siku njema,wiki njema,mwezi mwema.....MBARIKIWE
Amen mama mtumishi
 
Kemea utaisha,kuna wakati nulijua naogipa sana nyoka kila nikiingia ndani nawaza nyoka huwezi amini siku moja alfajiri nilijikuta nimebeba nyoka mgongoni nakung'uta akaanguka haa nikaitaa jina la Yesu nilipambana hadi kumuua,na nikaanza rasmi kukemea mfululizo limeisha hili jambo namshukuru Mungu
Aisee, hakukuuma?
 
Come on Mukongoman! Una batophobia? Ndege huwa unapanda na huogopi? Ulianza anzaje kuogopa haya majengo marefu?

Ila hizi phobia zingine hizi hata sijui zinaanzaje. Mimi siku hizi nikiona mende chumbani silali aisee mpaka nimtafute nimuue. Nikilala bila kumuua basi nitaota limende likuuuubwa linaninyemelea sasa hata kulikimbia siwezi. Hapo mwanaume ni kutoka jasho balaa. Ajabu wadudu wengine na hata nyoka sina tatizo nao kabisa. Huwa nashangaa sana kwa sababu nimekulia kijijini na mende kibao and it was no big deal.
Mkuu mm naogopa kupanda gari na hua natapika sana..
Naweza tibu hili tatizo ki vipi
 
Kemea utaisha,kuna wakati nulijua naogipa sana nyoka kila nikiingia ndani nawaza nyoka huwezi amini siku moja alfajiri nilijikuta nimebeba nyoka mgongoni nakung'uta akaanguka haa nikaitaa jina la Yesu nilipambana hadi kumuua,na nikaanza rasmi kukemea mfululizo limeisha hili jambo namshukuru Mungu
Mm kidogo ninshike kwenye kitasa asubuhi alikua kajivingirisha
 
NUKUU YA LEO

The first World Cup I remember was in the 1950 when I was 9 or 10 years old. My father was a soccer player, and there was a big party, and when Brazil lost to Uruguay, I saw my father crying.

Kombe la Dunia la kwanza nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1950 nikiwa na miaka 9 au 10. Baba yangu alikuwa mwanasoka na kulikuwa na sherehe kubwa, na Brazil ilipofungwa na Uruguay nilimuona Baba yangu akilia

7347ff9c26678277d442ca3b9cd9d875.jpg
8fd50d8f710b43893a6f399c6d667f79.jpg

Hayo ni maneno yaliyopatwa kutamkwa na mwanasoka wa Brazil Edson Arantes do Nascimento almaarufu kama PELE.

Pele alizaliwa 23/10/1940 katika mji mdogo wa minas Girais na kukulia ktk jiji la Sao Paulo.

Mwaka 1999 Pele alipigiwa kura ya kuwa mchezaji bora wa karne ya 20.

Pele amefunga magoli 1281 katika michezo yote 1363 aliyocheza ktk maisha yake ya soka.

Pele anashika nafasi ya pili kwa ufungaji wa magoli katika maisha ya soka akiwa nyuma ya mbrazil mwenzie Arthur Friedenreich aliyefunga magoli 1329 katika michezo 1239.

Kuna mengi sana kuhusu pele..lakini baba yake mzazi alilia machozi baada ya Brazili kupokea kipigo cha goli 2 kwa 1 toka kwa uruguay na inakuwa mara ya kwanza uruguay kuchukua kombe hilo baada ya Vita ya pili ya dunia.

Brazil wanakunywa mpira, Brazil wanakula mpira,
Brazil wanavaa mpira,
Brazil wanaishi mpira,
Brazil wanapenda mpira.

77c5433ab81c2785664ba1dc7fb52e87.jpg
Thanks T. wa Sakayo

eti Brazil wanakula mpira.....wanakunywa mpira.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom