Makapuku Forum

Makapuku Forum

Za asubuhi mkuu umeamkaje?vipi hali yako?pole Mungu aendelee kukuimarisha.

Nimesoma ujumbe wako natamani kuelewa zaidi,unisaidie kufafanua hapo,khs kesi kufanana na Bashite,napenda kujifunza ili pia nipate maneno ya kuwaeleza wanielewe na wachukukuliw hili suala kwa kulielewa,hivi wapo njiani wanakuja,nadhani usiku nitakuwa nao hapa
Nisikudanganye Mtumishi. Mimi siyo mwanasheria na kusema kweli mbali na kujua haki zangu za msingi kama raia wa Jamhuri ya Tanzania sijui cho chote kuhusu sheria.

Umesema kuwa walifeli kidato cha nne wakafanya mbinu wakabadili matokeo yao kinyemela (wakagushi vyeti) na matokeo hayo feki ndiyo yakawafanya wapate nafasi ya kuendelea na masomo yao mpaka wakapata ajira; na leo kosa lao walilofanya zamani ndiyo limesababisha watumbuliwe. Sijui tafsiri ya kisheria lakini nadhani kubadili matokeo kinyemela ni kosa. Kama kuna kapuku mwanasheria anaweza kutufafanulia zaidi.

Nimesikia TLS chini ya Tundu Lissu imewashauri wafanyakazi wote wanaoamini kuwa wametumbuliwa kimakosa waungane wafungue class action suit dhidi ya serikali na TLS itawapa msaada wa kisheria bure. Wanaweza kupata ufafanuzi wa kosa lao kisheria (kama wametenda kosa) na watajua cha kufanya baada ya hapo. Washauri wawasiliane na TLS au mwanasheria ye yote angalau wajue kosa lao limekaaje kisheria...and then they can go from there.

Bashite yeye alipiga ziro form 4 akanunua cheti cha mtu mwingine. Hawa matokeo hayakutosha wakajazia jazia kinyemela kwa majina yao yale yale. Sijui yupi ana kosa kubwa zaidi ya mwingine. Uwe na amani mtumishi na wape pole sana. Waambie wasikate tamaa. Maisha ni lazima yaendelee ati! Mungu Atawafungulia milango mingine!
 
494b075b8dcf22f13c72fed2c35b3202.jpg
d660247b947e6a4148474d38f88fa59e.jpg
Ndo babu yake Kim
Alikuwa katili ...sasa ili kumuiga kaanza kwanza kunyoa panki
Yaani mjukuu anamuiga babu na kufuara nyayo zake
......
Aisee kuna vitu havitokei kwa bahati mbaya.
 
Pele hakuwa na kipaji chochote labda kupiga danadana tu
Hata wakati Brazil inachukua makombe mchano wa Pele haukuwepo kivile
Maradona Ndo fundi

Pia enzi hizo kipa akirudishiwa mpira anataka
.....
Naunga mkono hoja yako.

Pele amechukua World Cup mara 3 lakini hakuwahi kuwa mfungaji bora au hata mchezaji bora.

Mwaka 1958 wanachukua kombe la Dunia Pele alikuwa ndio chipukizi.

Mwaka 1962 wanachukua Kombe la Dunia staa wa michuano alikuwa Mane Garrincha. Pele alicheza mechi mbili tu.

Mwaka 1970 wanachukua tena Kombe la Dunia pale Mexico. Staa wa michuano alikuwa Jaizinho ambaye alifunga goli kila mechi.

Lakini Maradona alikuwa ndio staa wa michuano pale alipoibeba Argentina mwaka 1986 na kutwaa Kombe la Dunia.

Pele alibebwa na mastaa wengine. Wakati Maradona ilibidi aibebe timu kwenye mgongo wake.
 
Nisikudanganye Mtumishi. Mimi siyo mwanasheria na kusema kweli mbali na kujua haki zangu za msingi kama raia wa Jamhuri ya Tanzania sijui cho chote kuhusu sheria.

Umesema kuwa walifeli kidato cha nne wakafanya mbinu wakabadili matokeo yao kinyemela (wakagushi vyeti) na matokeo hayo feki ndiyo yakawafanya wapate nafasi ya kuendelea na masomo yao mpaka wakapata ajira; na leo kosa lao walilofanya zamani ndiyo limesababisha watumbuliwe. Sijui tafsiri ya kisheria lakini nadhani kubadili matokeo kinyemela ni kosa. Kama kuna kapuku mwanasheria anaweza kutufafanulia zaidi.

Nimesikia TLS chini ya Tundu Lissu imewashauri wafanyakazi wote wanaoamini kuwa wametumbuliwa kimakosa waungane wafungue class action suit dhidi ya serikali na TLS itawapa msaada wa kisheria bure. Wanaweza kupata ufafanuzi wa kosa lao kisheria (kama wametenda kosa) na watajua cha kufanya baada ya hapo. Washauri wawasiliane na TLS au mwanasheria ye yote angalau wajue kosa lao limekaaje kisheria...and then they can go from there.

Bashite yeye alipiga ziro form 4 akanunua cheti cha mtu mwingine. Hawa matokeo hayakutosha wakajazia jazia kinyemela kwa majina yao yale yale. Sijui yupi ana kosa kubwa zaidi ya mwingine. Uwe na amani mtumishi na wape pole sana. Waambie wasikate tamaa. Maisha ni lazima yaendelee ati! Mungu Atawafungulia milango mingine!
Mkuu SHIMBA
Kuhusu lile suala la kuleta historia za nyumbani limeshindikana maana Waafrika hatuna kawaida ya kutunza kumbukumbu...tunazitafuta hazionekani

Labda mtu aanzishe segment awe anaelezea historia za mashujaa wetu km Chifu Mkwawa na n.k

Kuhusu suala la hao mabashite wana kosa la jinai wanatumia vyeti visivyo vyao na wengine wamechakachua matokeo pia wapo waliotengeneza tu vyeti
..........
 
Me ni mwoga kwenye majengo marefu.....yaani naweza ota hata kwa miaka 5!!!
Come on Mukongoman! Una batophobia? Ndege huwa unapanda na huogopi? Ulianza anzaje kuogopa haya majengo marefu?

Ila hizi phobia zingine hizi hata sijui zinaanzaje. Mimi siku hizi nikiona mende chumbani silali aisee mpaka nimtafute nimuue. Nikilala bila kumuua basi nitaota limende likuuuubwa linaninyemelea sasa hata kulikimbia siwezi. Hapo mwanaume ni kutoka jasho balaa. Ajabu wadudu wengine na hata nyoka sina tatizo nao kabisa. Huwa nashangaa sana kwa sababu nimekulia kijijini na mende kibao and it was no big deal.
 
Mkuu SHIMBA
Kuhusu lile suala la kuleta historia za nyumbani limeshindikana maana Waafrika hatuna kawaida ya kutunza kumbukumbu...tunazitafuta hazionekani

Labda mtu aanzishe segment awe anaelezea historia za mashujaa wetu km Chifu Mkwawa na n.k

Kuhusu suala la hao mabashite wana kosa la jinai wanatumia vyeti visivyo vyao na wengine wamechakachua matokeo pia wapo waliotengeneza tu vyeti
..........
Hapo sasa. Basi tusiwalalamikie wazungu kwa kupotosha historia yetu wakati sisi wenyewe wala hatujui tuanzie wapi.

Hapa maktabani kwangu nina vitabu vya Mashujaa wa Tanzania, Historia ya Wasukuma na Mila na Desturi za Wachaga lakini vyote vimeandikwa na wazungu kabla ya uhuru. Naweza kuwa na-scan na kuviweka pole pole kufuatia topic. Havina copyrights.
 
KUMTEGEMEA MUNGU KUNA FAIDA

ISAYA 40

29 Huwapa nguvu wazimiao ,humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo

Pale unapochoka fikra unapowaza sana unapokata tamaa ndipo Mungu anapokupa nguvu na kinga za kila shambulizi pia kukuvusha juu ya hali uliyo nayo ,hivyo pambana na hali hiyo kwani Bwana anatamalaki na kukupa utulivu na ushindi ili kumshinda adui anapotaka kukudhuru

Tumuombe Mungu atusaidie tumkabidhi Mungu njia zetu zote naye hatatuacha

TUOMBE

MUNGU BABA MWENYEZI tunakushukuru sana kwa ulinzi wako na yote unayotutendea,Mungu,umetutoa mbali tunakushukuru sana.

Ponya wagonjwa,fariji wafiwa,fariji wajane na yatima,tembea nasi Baba nyoosha mapito yetu,peke yetu hatuwezi

Tunajikabidhi miili na roho zetu tukinge na hatari zote za mwili na roho.

Roho Mtakatifu Mfariji wetu tufundishe ,tuongoze,tuonyeshe njia sahihi ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu

Asante kwa kila linakotokea maishani mwetu

Tunaomba yote kwa jina la Yesu mpatanishi na mwokozi wetu .

Amen

Muwe na siku njema,wiki njema,mwezi mwema.....MBARIKIWE
 
Naunga mkono hoja yako.

Pele amechukua World Cup mara 3 lakini hakuwahi kuwa mfungaji bora au hata mchezaji bora.

Mwaka 1958 wanachukua kombe la Dunia Pele alikuwa ndio chipukizi.

Mwaka 1962 wanachukua Kombe la Dunia staa wa michuano alikuwa Mane Garrincha. Pele alicheza mechi mbili tu.

Mwaka 1970 wanachukua tena Kombe la Dunia pale Mexico. Staa wa michuano alikuwa Jaizinho ambaye alifunga goli kila mechi.

Lakini Maradona alikuwa ndio staa wa michuano pale alipoibeba Argentina mwaka 1986 na kutwaa Kombe la Dunia.

Pele alibebwa na mastaa wengine. Wakati Maradona ilibidi aibebe timu kwenye mgongo wake.
129ad60b5414de5ecf47c0673e38e2c3.jpg
Jaizinho
5da38b031347a274025f326cd439c65e.jpg
Garrincha
a39f83e9c96aec0b8b7cd74418300cd9.jpg
Naradona na Shilton 1966
Maradona alifunga kwa mkono wa Mungu kisha akapoga goli la sina yake kwa kuwapunguza mabeki karibia wote kisha kipa wao

Pia Pele nasikia hajawai kucheza Ulaya hivyo goli zake ni km za Amissi Tambwe wa VPL
......
 
1968 - Oliver Bierhoff anazaliwa.

Mshambuliaji wa zamani wa Ac Milan na timu ya taifa ya Ujerumani.

Ndio mchezaji wa kwanza kufunga goli la dhahabu toka lilipoanzishwa. Alifanya hivyo katika michuano ya Euro mwaka 1996 pale England ambapo Ujerumani ilitwaa ubingwa huo.

Mmoja kati ya wanasoka wa Kijerumani ambao hawajawahi kuchezea Bayern Munich.

Kwasasa ni meneja wa timu ya taifa ya Ujerumani.
Oliver alikuwa jembe
 
KUMTEGEMEA MUNGU KUNA FAIDA

ISAYA 40

29 Huwapa nguvu wazimiao ,humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo

Pale unapochoka fikra unapowaza sana unapokata tamaa ndipo Mungu anapokupa nguvu na kinga za kila shambulizi pia kukuvusha juu ya hali uliyo nayo ,hivyo pambana na hali hiyo kwani Bwana anatamalaki na kukupa utulivu na ushindi ili kumshinda adui anapotaka kukudhuru

Tumuombe Mungu atusaidie tumkabidhi Mungu njia zetu zote naye hatatuacha

TUOMBE

MUNGU BABA MWENYEZI tunakushukuru sana kwa ulinzi wako na yote unayotutendea,Mungu,umetutoa mbali tunakushukuru sana.

Ponya wagonjwa,fariji wafiwa,fariji wajane na yatima,tembea nasi Baba nyoosha mapito yetu,peke yetu hatuwezi

Tunajikabidhi miili na roho zetu tukinge na hatari zote za mwili na roho.

Roho Mtakatifu Mfariji wetu tufundishe ,tuongoze,tuonyeshe njia sahihi ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu

Asante kwa kila linakotokea maishani mwetu

Tunaomba yote kwa jina la Yesu mpatanishi na mwokozi wetu .

Amen

Muwe na siku njema,wiki njema,mwezi mwema.....MBARIKIWE
Amen
 
Hapo sasa. Basi tusiwalalamikie wazungu kwa kupotosha historia yetu wakati sisi wenyewe wala hatujui tuanzie wapi.

Hapa maktabani kwangu nina vitabu vya Mashujaa wa Tanzania, Historia ya Wasukuma na Mila na Desturi za Wachaga lakini vyote vimeandikwa na wazungu kabla ya uhuru. Naweza kuwa na-scan na kuviweka pole pole kufuatia topic. Havina copyrights.
Shida kwelikweli
Itabidi ajitokeze mtu awe anatuandikia
Ni vitu vyenye mvuto
......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom