Makapuku Forum

Makapuku Forum

Asante mkuu sikuona update mapema

Epl mambo matamuuuu

Twende sawa wakuu ukiwaacha wale wawili wa juu waende zao..... Basi huku kwenye top four ni pagumu sana kujua nani anabaki na Nani anatoka maana 63, 61, 57 na 54 hizi ni nambari za alama mujarabu kabisa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Sunderland ni kama teyari keshakufa ila Bado anasubiriwa Bradley tu kupeleka maua mwisho wa Msimu..... Sijawahi kukata tamaa ila kwa namna wanavyojikongoja Msimu ujao hakutakuwa na EPL pale Stadium of light....... David Moyes the Choosen one naona survival black cat wanafia mikononi mwako mzee.

Pamoja na red card ila Bado Sunderland hakuwa na mawazo ya kumzuia Mourinho kwa ....

Sunderland 0-3 Manchester united

Leo sijui mzee wetu Wenger anamshusha jirani yake ??

Kama kumuua mhindi weekend hii najua braza mwekahazina ulifanya chaguo sio sahihi ...
Mimi kwa EPL ya mda huu m-bet wanipe likizo kwanza.... Kwa maana timu nyingi zinapambana kujiweka mahari pazr...

Kuna zile za big four kwa UEFA

Kuna zile nafasi 5-7 kwa UEROPA

Na zile za kupambana kujiokoa zisipotee kwenye EPL

Hakakika hii ni vita tosha!!!!
 
73c4b1176d9aca742bfdb0db50c8a975.jpg
 
Don't cry!

Huyu mama alikuwa na uraia wa karibia nchi saba,

Serbia
Albania
Macedonia
India
Yugoslavia
Na nchi zingine za ulaya..

Mama Teresa aliondoka kwao akiwa na miaka 18 baada ya kifo cha baba yake..

Toka alivyondoka nyumbani kwa hakuwa kumuona dada yake wala mama yake mzazi tena..

Mama Teresa aliamini katika kutoa na kusaidia wasio jiweza hasa wagonjwa na yatima..

Mtakumbuka mwaka 1979 alipewa Tuzo ya Nobel ( Nobel peace prize)

Ninukuu maneno ya speech yake siku ya kupewa tuzo..

Around the world, not only in the poor countries, but I found the poverty of the West so much more difficult to remove. When I pick up a person from the street, hungry, I give him a plate of rice, a piece of bread, I have satisfied. I have removed that hunger. But a person that is shut out, that feels unwanted, unloved, terrified, the person that has been thrown out from society—that poverty is so hurtable

Duniani kote, sio kwa nchi maskini tuu, ila kuondoka umaskini wa magharibi ni vigumu, nikimpata mgonjwa mtaani ana njaa ,nampa sahani ya wali, kipande cha mkate na nina ridhika, lakini hali ya kutengwa, kutokukubalika, kutokupendwa, kutishwa, kutengwa na jamii yako... HUU UMASKINI UNAUMA SANA

Hela ambayo alipewa kiasi cha 129,000 Usd, alisema kikasaidie maskini nchini india..

Huyu mama alikuwa na mtu wa pekee sana..
Pia pale Kanisa katoliki Kigogo Mburahati kuna kituo chake cha kulelea watoto yatima nafikiri aliwahi kuja miaka ya 90's japo sina kumbukumbu wala uhakika wa ujio wake
....
.
 
Ni kweli mzee Wenger anaweza kukumbana na ya mzee wa blues ila kumbuka Chelsea biashara walishafanya mpaka kwenye alama 72 sasa kilichobaki na wanachokifanya kwa sasa ni mahesabu tu..... Walianza na hesabu ya alama +18 na sasa wanaendelea kuhesabu +15 zilizobaki.

Biashara ni hasubuhi na jioni ni mahesabu tu....

Sio mbaya tukamuacha Chelsea auwaze ubingwa uku wengine tukigombea top 4
Mkuu kweli nyie gombanieni huko na mkiwa mnajiandaa kuja kutuvisha medali blues!!!
 
Big up mkuu nimeipenda sana nukuu ya leo inagusa sana
Aliyetegwa>>>>Aliyetengwa.
Mkuu

Hizi nukuu mimi siweki tuu kwa kuwa nilisema nitaweka nukuu..

Nataka hizi nukuu zibadilishe maisha ya members humu..

Yaani, kila siku ujifunze kupitia hizi nukuu..

Ni muhimu sana kama unaweza kuzifanyia kazi at leat kwa 51% if not 100%

Nawapenda makapuku..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom