Makapuku Forum

Makapuku Forum

- Leo ni Mwaka Mmoja wa Makapuku Forum.

Iliasisiwa na Bitoz na Bailly5 bila kumsahau Jimena ikiwa na lengo la kuleta umoja na usawa kwa baadhi ya members ambao sio wakongwe waliokuwa wanabaguliwa na kutengwa pindi wanapochangia katika threads za wanaojiita wakongwe.

Binafsi sikuwepo wakati inaanza nilikuja kujiunga nayo mwezi mmoja baadae lakini mpaka leo sijawahi kujuta, kwani imenikutanisha na watu wengi ambao nimejifunza mengi kwao bila chuki yoyote zaidi ya upendo wa hali ya juu.

Changamoto ni nyingi lakini tunapambana nazo na ndio maana leo tunatimiza mwaka mmoja kwa kishindo cha hali ya juu.

Kwani hakuna aliyeamini kama KF ingefikia hapa ilipo wengi walidhani ingekufa kibudu wakidhani ni nguvu ya soda.

Hivyo basi, leo tukiwa tunasherehekea mwaka mmoja, tufarahi, turukeruke, tujidai kwani haikuwa rahisi kufika hapo.

Nitoe tena pongezi kwa waasisi ambao ni;
Bitoz
Bailly5
Jimena

Pengine bila wao leo hii tusingekuwa hapa.

Heri ya Mwaka Mmoja kwa Makapuku Forum.
Mkuu umeelezea vizuri
Sina cha kuongea
Mafanikio ya huu uzi ni ya wote
Kila mtu ana umuhimu wake
............
 
Kwaherini Bandugu ngoja nirudi kwenye uwanja wetu wapenda Stress, BTW nimeinjoi kuwa nanyi tangu jana. Ila kama kuna shughuli basi nitarudi maana Shughuli ni watu na watu ndiyo sisi. Kama ikibidi nitabeba na rambo kabisa. Ndizi na pilipili huwa ni kawaida natembea nazo!!
hahahhahh unapenda kula ww inaonekana
 
Leo ni tarehe April 9, 2017 huu Uzi uliandikwa tarehe kama ya leo ambayo ni April 9, 2016.

Uzi umetimiza mwaka mmoja na comments 160K.

Makapuku oyeeeeeee
ebwana kweli mnaweza kulisongesha, struggle zote na competion ya wakongwe lakin kombe limeenda kwa MAKAPUKU kwa kweli
nimeousoma mchezo since game inaanza Aprl 9 2016.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom