- Leo ni Mwaka Mmoja wa Makapuku Forum.
Iliasisiwa na
Bitoz na
Bailly5 bila kumsahau
Jimena ikiwa na lengo la kuleta umoja na usawa kwa baadhi ya members ambao sio wakongwe waliokuwa wanabaguliwa na kutengwa pindi wanapochangia katika threads za wanaojiita wakongwe.
Binafsi sikuwepo wakati inaanza nilikuja kujiunga nayo mwezi mmoja baadae lakini mpaka leo sijawahi kujuta, kwani imenikutanisha na watu wengi ambao nimejifunza mengi kwao bila chuki yoyote zaidi ya upendo wa hali ya juu.
Changamoto ni nyingi lakini tunapambana nazo na ndio maana leo tunatimiza mwaka mmoja kwa kishindo cha hali ya juu.
Kwani hakuna aliyeamini kama KF ingefikia hapa ilipo wengi walidhani ingekufa kibudu wakidhani ni nguvu ya soda.
Hivyo basi, leo tukiwa tunasherehekea mwaka mmoja, tufarahi, turukeruke, tujidai kwani haikuwa rahisi kufika hapo.
Nitoe tena pongezi kwa waasisi ambao ni;
Bitoz
Bailly5
Jimena
Pengine bila wao leo hii tusingekuwa hapa.
Heri ya Mwaka Mmoja kwa Makapuku Forum.