Makapuku Forum

Makapuku Forum

1967 - Ndege ya kwanza ya Boeing 737 yaanza safari yake ya kwanza.
161bd092bbda99f0ee0d3608ee5b0a2e.jpg
7c3cf32fa15dac2de5675a6ef1e3a3db.jpg
ee20a07f68d811542ca98c0023820f40.jpg
 
- Leo ni Mwaka Mmoja wa Makapuku Forum.

Iliasisiwa na Bitoz na Bailly5 bila kumsahau Jimena ikiwa na lengo la kuleta umoja na usawa kwa baadhi ya members ambao sio wakongwe waliokuwa wanabaguliwa na kutengwa pindi wanapochangia katika threads za wanaojiita wakongwe.

Binafsi sikuwepo wakati inaanza nilikuja kujiunga nayo mwezi mmoja baadae lakini mpaka leo sijawahi kujuta, kwani imenikutanisha na watu wengi ambao nimejifunza mengi kwao bila chuki yoyote zaidi ya upendo wa hali ya juu.

Changamoto ni nyingi lakini tunapambana nazo na ndio maana leo tunatimiza mwaka mmoja kwa kishindo cha hali ya juu.

Kwani hakuna aliyeamini kama KF ingefikia hapa ilipo wengi walidhani ingekufa kibudu wakidhani ni nguvu ya soda.

Hivyo basi, leo tukiwa tunasherehekea mwaka mmoja, tufarahi, turukeruke, tujidai kwani haikuwa rahisi kufika hapo.

Nitoe tena pongezi kwa waasisi ambao ni;
Bitoz
Bailly5
Jimena

Pengine bila wao leo hii tusingekuwa hapa.

Heri ya Mwaka Mmoja kwa Makapuku Forum.
Ni jambo la kujivunia katika hili

Aluta kontinyua
 
Asalaam aleykum Kapuku's
Tumsifu Yesu kristo Kapuku's
Bwana Yesu asifiwe Kapuku's
Shalom Kapuku's

Sina mengi ya kuzungumza hapa katika kuadhimisha siku yetu ya leo

Napenda tu kutoa rai kwa Makapuku wenzangu kwamba tudumishe amani, upendo na mshikamano ndio silaha kuu ili kuzidi kuwa bora.

Happy birthday to all Kapuku's for one year.
Amen
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom