Makapuku Forum

Makapuku Forum

1992 - Mahakama nchini Marekani inamtia hatiani na kumuhukumu miaka 30 jela Kiongozi wa zamani wa Panama, Manuel Noriega kwa kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya enzi za utawala wake.

Noriega alikuwa ni kibaraka wa CIA lakini walivyotofautiana tu wakamtoa madarakani.
CIA ni hatari sana kwenye hii dunia
 
LEO KATIKA HISTORIA:

1937 - Ndege aina ya Kamikaze yatua katika uwanja wa ndege wa Croydon uliopo London.

Inakuwa ndege ya kwanza kutengenezwa Japan kutua Ulaya.
e9e79f960dce9fb13ed90e6b2fa59236.jpg
1c1a2d4c19f5b2dd945b364077d3e8f2.jpg
9cb219076719332b1e991aaee6df36bb.jpg
d764c3fd5dbed8c3e7fc43ad98eb96bb.jpg
Kipindi hicho ilionekana km bonge la dege la kijanja
......
 
- Leo ni Mwaka Mmoja wa Makapuku Forum.

Iliasisiwa na Bitoz na Bailly5 bila kumsahau Jimena ikiwa na lengo la kuleta umoja na usawa kwa baadhi ya members ambao sio wakongwe waliokuwa wanabaguliwa na kutengwa pindi wanapochangia katika threads za wanaojiita wakongwe.

Binafsi sikuwepo wakati inaanza nilikuja kujiunga nayo mwezi mmoja baadae lakini mpaka leo sijawahi kujuta, kwani imenikutanisha na watu wengi ambao nimejifunza mengi kwao bila chuki yoyote zaidi ya upendo wa hali ya juu.

Changamoto ni nyingi lakini tunapambana nazo na ndio maana leo tunatimiza mwaka mmoja kwa kishindo cha hali ya juu.

Kwani hakuna aliyeamini kama KF ingefikia hapa ilipo wengi walidhani ingekufa kibudu wakidhani ni nguvu ya soda.

Hivyo basi, leo tukiwa tunasherehekea mwaka mmoja, tufarahi, turukeruke, tujidai kwani haikuwa rahisi kufika hapo.

Nitoe tena pongezi kwa waasisi ambao ni;
Bitoz
Bailly5
Jimena

Pengine bila wao leo hii tusingekuwa hapa.

Heri ya Mwaka Mmoja kwa Makapuku Forum.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom