Makapuku Forum

Makapuku Forum

Asante sana mkuu Transcend ubarikiwe.
Hakika umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

Pumzika kwa amani Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere..daima tutakukumbuka..hekima zako na usemi wako tutautumia daima.

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
Amina mama mchungaji..

Umoja ni kitu muhimu sana.

Kwenye biblia utakumbuka wana wa izrael na umoja wao..

Siku wanaingia nchi ya ahadi..( the land of milk and honey). Utakumbuka mji wa yeriko ulivyotwaliwa..( the fall of Jericho) Joshua; 6:1-

Walivyozunguka mji mara moja kwa umoja wao wakiongozwa na Joshua...

Hapa ndo utajua kwanini Taifa linatakiwa liwe na umoja..

Kwanini Tz tunatakiwa tuwe na umoja...!

Wananchi tungekuwa na umoja leo hii Tz isingikuwa inafanya blundering za ajabu hivi..

Anyway! Ngoja niishie hapa kwa leo.
 
Leo katika Historia:

1946 - Syria yapata Uhuru wake toka kwa Ufaransa.
24cf9349d4242ed3af8826e796d9f92f.jpg
94c88c8ac5892768dbe820d08f67ad6a.jpg
532c60416891d90c00182c709862ee8f.jpg
bora wangenyimwa Uhuru maana kila siku kwao vita japo kuna mkono wa MTU
.....
.
 
1972 - Rais wa Zanzibar Abeid Amani Karume anauwawa kwa kupigwa risasi 8 mwilini mwake alipokuwa anacheza bao makao makuu ya ASP huko Kisiwandui.

Risasi hizo nane alizopihwa ni sawa na miaka 8 ya utawala wake.

Inasemekana aliuwawa na Luteni Humoud ambaye ni kama alikuwa analipiza kisasi cha kuuwawa kwa baba yake.

Wapo wanaosema kuuwawa kwa Karume ni Jaribio lililoshindwa kupindua serikali yake hivyo wakaamua kumuua tu.

Pia wapo wanaosema kupishana kwake kauli na JK Nyerere kuligharimu uhai wake kwani aligoma kuhusu muundo wa Muungano ambapo alidiriki kusema Muungano ni kama koti likikubana unalivua, pia aligoma kabisa kuunganisha vyama vya ASP na TANU ili izaliwe CCM. Kauli hizo zinadaiwa kumchefua Nyerere.
f0fdbc700d2b2c388cf086971941ad13.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom