1989 - James Bond anafariki Dunia.
Alikuwa ni mtaalam wa viumbe hai hasa ndege. Alikuwa ni raia wa Marekani.
Jina lake lilichukuliwa na kuanza kutumika katika mfululizo wa Filamu za Kijasusi zijulikanazo kama James Bond.
Mtunzi wa filamu za James Bond, ndugu Ian Fleming alipenda sana kufatilia kazi za James Bond hasa kwa kutazama Vipindi vyake na kusoma vitabu vyake hasa vinavyohusu Ndege, hali hiyo ilipelekea akalipenda sana Jina la James Bond na kuliomba alitumie katika Filamu zake alizozitunga akianza na ile Casino Royale ya mwaka 1953.
Hivyo mwenye jina la James Bond alikuwa ni mtaalam wa ndege ambapo jina lake likaenda kutumika katika filamu za kijasusi.