Makapuku Forum

Makapuku Forum

172f3f1fa2446e98e08cf34fc16302f3.jpg
Aaaah!!!
 
Kweli kabisa mkuu.Ikitokea New comer ameanzisha uzi utasikia....peleka fb,...chuo kimefunguliwa?....jf imevamiwa na Division 5....Vi.laza wa Gram wameibukia JF.Lakini kama ni mkongwe ameanzisha uzi hata kama ni pumba, wazee wenzake watajitutumua kwenye comments ili uzi uonekane una maana.

Hayo ni tisa, kumi KE anzishe uzi.Yaani ata kama ni tusi, mizee mizima itajipendekeza na michango uchwara...utaona wakipost....hiyo avatar ni ya kwako?....njoo PM tumalizane....Upo maeneo gani?..n.k.

Lengo langu siyo kuleta matabaka kati ya ME na KE, ama kati ya wakongwe na wageni, la hasha!...Kama ikitokea mtu amepost kitu na anahitaji ushauri/maoni asaidiwe bila kujali kuwa ni KE ua ME, mkongwe ama mgeni....tushirikiane kwa pamoja ili jamii yenye uelewa ianzie hapa JF.

Jambo lingine dharau sii kitu kizuri, kama upo jf toka kuanzishwa kwake haimanishi kuwa wewe ni wa maana kuliko ambaye profile yake inasomeka...joined yesterday...Kila mtu kwa nafasi yake anaweza kutoa au kupokea mawazo ya kujenga kutoka kwa watu mbali mbali.

MWISHO: WADUMU MAKAPUKU....FIKRA ZA MAKAPUKU ZIISHI DAIMA....MILELE LIDUMU JINA LA MAKAPUKU.
Viva makapuku
 
NUKUU NO 1#

Kuna watu hapa duniani ambao wanaishi katika njaa kali kiasi kwamba Mungu hawezi kuwatokea katika njia nyingine isipokuwa kama chakula

Maneno haya yalitamkwa na Mohandas Karamchand Gandhi (Mahatma Gandhi)
Aliyeishi Kati ya mwaka 1869 hadi mwaka 1948.

Gandhi alikuwa kiongozi wa vuguvugu la kudai uhuru wa India kutoka kwa wakoloni wa Uingereza
Kuna hadi mitaa inaitwa Gandhi...duuuh wahindi hawatomsahau huyu.
 
NUKUU NO 2#

Katika maisha nimejifunza vitu vingi.
Nimejifunza kwamba watu watasahau mambo uliyowahi kuyasema, watasahau ulichowafanyia lakini hawatasahau ulichowafanyia namna ulivyowafanya wajisikie


Maneno haya yalisemwa na mtunzi, mshairi, mcheza muziki na mwanaharakati wa Marekani, Maya Angelou
Aliyeishi Kati ya mwaka 1928 hadi 2014
Alikula chumvi ya kutosha. RIP
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom